Thursday, June 11, 2015


www.bukobasports.comKlabu ya Swansea City inayokipiga Ligi Kuu England imethibitisha kumsaini Mchezaji mpya @AyewAndre na atavaa jezi namba 10 kwa ukamilisho huo wa ujio huo Ligi Kuu katika Klabu hiyo yenye Uwanja unaojulikana Liberty Stadium.
Andre Ayew amesajiliwa kutoka kwenye Klabu ya Marseille.



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premier Lager, kesho siku ya ijumaa jioni inatarajiwa kuondoka Addis Ababa Ethiopia kuelekea nchini Misri tayari kwa mchezo wa siku ya jumapili.
Stars ambayo imeweka kambi ya mazoezi takribani kwa wiki moja sasa jijini Addis Ababa leo imeendelea na raiba yake ya mazoezi katika uwanja wa Taifa, amabpo leo imefanya mazoezi yake asububuhi tu.
Kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema, anashukuru maendeleo ya kambi ni mazuri timu yake inafanya mazoezi katika viwanja viwili vizuri vilivyopo Addis Ababa, uwanja wa Taifa na uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia.
Nooij amesema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake kucheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji wameonyesha kufuata vizuri maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.

Akiongelea mchezo dhidi ya Misri siku ya jumapili, Nooij amesema timu inakwenda kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo, nafahamu tunaenda cheza ugenini, nimewaelekeza vijana wangu wanaocheza nafasi ya ushambuliaji kutumia vizuri nafasi tutakazozipata katika mchezo huo.



kuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita katikati akiwa katika picha ya pamoja na mabingwa wa mashindano ya kombe la Muungano Mufindi timu ya Mucoba Fc ,wa kwanza kulia ni mratibu wa mashindano hayo aliyestaafu rasmi Daud Yassin na mdau mkubwa wa soka mkoa wa Iringa Feisal Asas
Na MatukiodaimaBlog
MASHINDANO ya kombe la Muungano Mufindi yamefikia tamati baada ya timu ya benki ya wananchi wilaya ya Mufindi (MUCOBA FC) kuibukwa mabingwa wa fainali ya mashindano hayo kwa kuigagadua (kuifunga) timu ya Academ kutoka Dodoma kwa jumla ya magoli 2-0
Huku mratibu wa mashindano hayo Daud Yassin akitangaza kustaafu rasmi nafasi yake hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 19 hivi sasa .
Mratibu huyo aliweza kuwaaga rasmi wapenzi wa mpira wa miguu katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa wa shule ya msingi wambi mjini Mafinga.
Yassin aliwashukuru wadau wote wa soka waliomsaidia kwa namna moja au nyingine kwa miaka 19 aliyoratibu mashindano hayo.
Alisema pia anawashukuru viongozi mbalimbali, chama cha soka wilaya ya Mufindi, chama cha soka mkoa wa lringa, shirikisho la soka nchi TFF, na ZFA kwa kuonyesha ukaribu wao kwa kipindi chote cha mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano na Masoko,Consitantine Magavila akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Fleva George Mdemu (Gnako),Afisa mipango wa kampuni ya Open Society Intiative for Eastern Africa(OSIEA),Adam Antony,Afisa Elimu NEC,Rose Malo pamoja na Snura Mushi(Snura).
Afisa Elimu wa NEC,Rose Malo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vijana walioona umhimu wa kupiga kura na kuhamasisha vijana wengine kwa njia ya nyimbo,kutokana na mwaka huu kuwa ni mwaka wa Uchaguzi mkuu hapa nchini akizungumza katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam leo. kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano na Masoko,Consitantine Magavila na Afisa mipango wa kampuni ya Open Society Intiative for Eastern Africa(OSIEA),Adam Antony.

kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Fleva George Mdemu (Gnako), Snura Mushi (Snura),Kala Masanja (Kala Jeremiah) pamoja na Boniventure Kabogo(Stamina) wakiimba kipande cha wimbo ambao utakuwa ukielimisha jamii kuhusiana na umhimu wa upigaji kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
VIJANA wamekuwa na changamoto ya kutoshiriki katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na kushindwa kupata haki yake msingi ya kupiga kura katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini.


Rais wa shirikisho la kandanda duniani Sepp Blatter ataachia ngazi ifikapo Desemba 16 ambapo mrithi wa kiti hicho atajulikana.
Blatter aliyetangaza kujiuzulu wadhifa wake ikiwa ni siku nne tangu kuchaguliwa tena kuliongoza shirikisho hilo kwa muhula watano.
Wanachama wote 209 wa Fifa wataalikwa Uswisi kwa ajili ya uchaguzi wa Rais mpya wa shirikisho hilo la soka.
Maamuzi ya mwisho ya tarehe ipi utafanyika uchaguzi itajulikana mwezi Julai ambapo kamati kuu ya Fifa itakapokutana.


Waziri mkuu, Mizengo Pinda akikagua kundi la waamuzi na walimu wa michezo wa shule za sekondari baada ya kufungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10, 2015. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kanda ya ziwa baada ya kufungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10, 2015. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga mpira wakati alipofungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Juni 10, 2015.
Msanii wa ngoma ya Kisukuma akicheza na nyoka aina ya chatu wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza amabko Juni 10, 2015 alifungua michezo ya UMISETA.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya UMISETA wakipita kwa mandamano mbele ya mgeni rasmi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika ufunguzi wa mashindano hayo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10, 2015.
Waziri mkuu, Mizengo Pinda akikagua kundi la waamuzi na walimu wa michezo wa shule za sekondari baada ya kufungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kanda ya ziwa baada ya kufungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10, 2015.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga mpira wakati alipofungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Juni 10, 2015.
 Waziri mkuu, Mizengo Pinda akirusha mpira wa kikapu wakati alipozindua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba Juni 10, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil Marta Vieira da Silva almaarufu Marta ameweka historia ya kuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia la wanawake baada ya kufikisha mabao 15.
Marta amefikisha idadi hiyo ya mabao baada ya kufunga bao moja kwa mkwaju wa penati kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya korea kusini ambapo Brazili waliibuka kidedea kwa mabao 2-0.
Ushindi huo umeifanya Brazil kuwa vinara wa kundi E, Baada ya Hispania na Costa Rica kwenda sare ya kufungana 1-1.

Mshambuliaji huyu ameichezea timu ya taifa jumla ya michezo 137 akiwa kafunga mabao 93. Kwa sasa Marta ni mchezaji wa klabu ya Rosengard FC ya Sweden.


Ukurasa wa mbele wa gazeti la The Sun leo umekuja na stori kwamba Manchester United wanahitaji mshambuliaji wa maana ili kurudi kushindania ubingwa msimu ujao.
Kwa mujibu wa The Currant Bun, “Manchester United wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Mario Mandzukic”.
Mandzukic ameibuka kuwa mchezaji anayewaniwa zaidi na Man United ili kutengeneza muunganiko na Wayne Rooney msimu wa 2015/2016 chini ya kocha Louis van Gaal.
United wanalazimika kutafuta straika baada ya Radamel Falcao kurudi katika timu yake ya Monaco, huku Van Gaal akiwa hana mpango wa muda mrefu na Javier Hernandez na Robin van Persie.
Mario Mandzukic ni jibu kwa Van Gaal?
Mcroatia huyo alianza kuonesha cheche akiwa Bayern Munich na msimu uliopita alicheza vizuri akiwa na Atletico Madrid, lakini wachambuzi wengi wa soka hawamuweki kwenye kundi la washambuliaji wa kiwango cha juu zaidi duniani.


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe 11/06/2015 wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League msimu wa 2014/2015.
Hafla ya utoaji wa zawadi hizo itafanyika katika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio eneo la Posta Mpya jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.
Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :

1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Hussein (Simba SC)
Mrisho Ngasa (Young Africans)
Saimon Msuva (Young Africans)

2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Shaban Hassan (Coastal union)

3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Goran Kopunovic (Simba SC)
Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)

4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Israel Mjuni Nkongo
Jonesia Rukyaa
Samwel Mpenzu

5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mgambo JKT
Mtibwa Sugar
Simba SC

JOHN MAHUNDI MCHEZAJI BORA MWEZI MEI
Wakati huo huo mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei, 2015 na jopo la makocha kufuatia kuwazidi wachezaji wengine 14 aliokuwa anananiwa nao nafasi hiyo.
Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.



Ligi kuu ya Tanzania Bara inategemewa kuwa na msisimko zaidi msimu ujao kwa mwaka 2015/16 baada ya bodi ya ligi nchini kupitisha azimio la kusajili wachezaji 10 wa kigeni.
Msimu uliopita wa ligi kuu, kila timu shiriki iliruhusiwa kusajili wachezaji wageni wasiozidi watano lakini azimio jipya, ambalo bado vilabu wamelikubali, litatoa fursa ya kusajili wachezaji 10 katika kile kinachoonekana kuleta ushindani.
Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema azimio hilo litawasilishwa katika kamati ya utendaji kwa ajili ya kupata ridhaa.
Hata hivyo, ongezeko hilo la wachezaji watano limeleta maoni tofauti kwa wadau wa soka, huku wengine wakisema kuwa mbali ya kuleta ushindani, pia litaua vipaji na kunyima fursa ya uchezaji kwa wachezaji wazawa.
Vilabu vikubwa nchini Tanzania kama vile Simba, Yanga na Azam zimekuwa zikisajili wachezaji wageni kwa ajili ya kuleta tija katika ushindani wao wa ndani na ule wa kimataifa.


Hatima ya Kocha Luis Enrique kubakia FC Barcelona sasa imekwisha baada ya kusaini nyongeza kwenye Mkataba wake.
Katika Msimu wake wa kwanza tu na Barca, Enrique alimudu kutwaa Trebo baada kubeba Ubingwa wa Spain La Liga, Copa del Rey na juzi kuzoa Kombe la Ubingwa Ulaya, UEFA CHAMPIONS LIGI.
Lakini licha ya mafanikio hayo ilizigaa imani kubwa ataondolewa.
Lakini kwa kusaini nyongeza ya Mkataba itakayomweka Barca hadi mwishoni mwa Msimu wa 2016/17, utata huo sasa umekwisha.
Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, ndie alietangaza kuongezewa Mkataba Enrique.

Enrique, ambae aliwahi kuzichezea Barca na Real Madrid, aliteuliwa Mwaka jana kumbadili Tata Martino ambae sasa ni Kocha wa Argentina.



Mbunge wa viti maalumu Lucy Owenya (Chadema)akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kibosho Kilima kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali katika mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.

Mratibu a mashindano hayo Charles Mchau akisalimiana na wachezaji.

Mgeni rasmi katika fainali hiz katibu wa Chadema kanda ya kaskazini Aman Golugwa akisalimiana na wachezaji.

Mbunge Lucy Oweya akiwa ameambatana na mgeni rasmi Aman Golugwa mara baada a kukagua timu hizo.

Mgeni rasmi katika mashindano ya Lucy Owenya Cup yaliyoshirikisha timu za jimbo la Moshi vijijini,Aman Glogwa akizungumza na timu zilizoingia fainali za Kibosho Kindi na Kibosho Kilima.


Manahodha wa timu hizo mbili wakipeana mikono kusalimiana.

Timu ya Kibosho Kindi wakiomba Dua.

Timu ya Kibosho Kilima wakiomba Dua.

Waamuzi wakiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu hizo mbili.

Timu ya Kibosho Kindi katika picha ya pamoja.

Timu ya Kibosho Kilima katika picha ya pamoja.


Baadhi ya mashabiki waliohudhulia mchezo huo.

Mchezo ukiendelea.



Moja ya timu iliyoshiriki mashindano hayo Sangiti Sekondari wakifuatilia mchezo wa fainali.

Meza kuu wakifurahi mara baada ya mwamuzi kupuliza kipyenga cha mwisho ambapo timu ya Kibosho Kindi iliibuka na ushindi wa bao 3 kwa 1.

waliotembelea blog