Friday, September 4, 2015





Nahodha mpya wa Uholanzi, Arjen Robben alitoka uwanjani baada ya dakika 27 tu kufuatia kuumia nyonga PICHA ZAIDI GONGA HAPA



TIMU ya taifa ya soka ya Iceland imejisogeza kukata tiketi ya kufuzu kucheza mchuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2016 baada ya ushindi wa penalti ya utata ya Gylfi Sigurdsson w 1-0 dhidi ya Uholanzi waliomaliza pungufu ya mchezaji mmoja usiku wa jana.

Refa Milorad Mazic wa Serbia, aliyemtoa kwa kadi nyekundu Martins Indi dakika ya 33, aliwazawadia mkwaju wa penalti Iceland dakika ya  51 ingawa Gregory van der Wiel alionekana kuuwahi moira wakati anapambana na Birkir Bjarnason. 

Sigurdsson akaenda kufunga penalti hiyo akimtungua kipa Jasper Cillessen na kuiweka Iceland katika mazingira mazuri ya kukata tiketi ya kwanza ya fainali za michuano mikubwa. 

Matokeo hayo yanaiweka Uholanzi katika mazingira magumu kidogo katika kundi hilo A kutokana na Iceland kutimiza pointi 18, mbili zaidi ya Jamhuri ya Czech wanaoshika nafasi ya pili. Uholanzi inabaki na pointi zake 10.

Iceland sasa wanaweza kujihakikishia kucheza Euro 2016 iwapo tu watashinda mchezo wa nyumbani dhidi ya Kazakhstan Jumapili.

Kipigo hicho kinamuweka pabaya kocha mpya wa Uholanzi, Danny Blind. Kocha aliyetangulia Guus Hiddink alilazimika kujiuzulu kwa sababu ya matokro mabaya hususan baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-0 nchini Iceland mwezi Oktoba.

Mshambuliaji Robin van Persie, ambaye aliiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil zaidi ya mwaka mmoja uliopita, jana aliwekwa benchi na kocha Blind. 


MECHI ZILIZOSALIA

Septemba 6; 
Latvia vs Jamhuri ya Czech Uturuki vs Uholanzi
Iceland vs Kazakhstan
Oktoba 10 
Iceland vs Latvia, Kazakhstan vs Uholanzi Jamhuri ya Czech vs Uturuki
Oktoba 13
Latvia vs Kazakhstan; Uholanzi vs Jamhuri ya Czech 
Uturuki vs Iceland

Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen, Van der Wiel, De Vrij, Martins Indi, Blind, Wijnaldum/Promes dk80, Klaassen, Robben/Narsingh dk31, Sneijder, Depay na Huntelaar/Bruma dk40.

Iceland; Halldorsson, Saevarsson, Arnason, Ragnar Sigurdsson, Ari Freyr Skulason, Bodvarsson/Finnbogason dk78, Gylfi Sigurdsson, Gunnarsson/Olafur Ingi Skulason dk86,Birkir Bjarnason, Gudmundsson na Sigthorsson/Gudjohnsen dk64).
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ameonge na vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya timu na hali za wachezaji siku moja kabla ya mechi dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Walitakiwa kuwepo makocha wa timu zote mbili ila kocha wa Nigeria Sunday Oliseh hakutokea.
Timu ya taifa ya Tanzania imefanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mechi dhidi ya Nigeria asubuhi ya Septemba 4 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, lakini wachezaji wote wapo fiti ila Mbwana Samatta amepata majeraha ya kawaida katika mazoezi.
“Wachezaji wapo vizuri ila aliyekuwa majeruhi serious ni Abdi Banda ambaye atakaa nje ya uwanja kwa siku 21 baada ya kuumia nyama za paja, Samatta amepata majeruhi ya kawaida asubuhi ya leo katika mazoezi ya mwisho ila hadi jioni atakuwa yupo sawa”>>> Mkwasa
Timu ya taifa ya Nigeria ambayo inanolewa na kocha mzawa kama ilivyo kwa Tanzania imewasili usiku wa Septemba 3 Uwanja wa ndege wa kimataidfa JKN Dar Es Salaam, ikiwa na kikosi cha wachezaji wake, ila kocha Sunday Oliseh hii itakuwa ni mechi yake ya kwanza toka aanze kuifundisha Super Eagles hivyo presha itakuwa pande zote mbili.



Baada ya kuweka headlines nyingi usiku wa tuzo za MTV VMA’s mwaka huu na show iliyoisha kwa machozi, Justin Bieber kaamua kuzungumza sababu zilizompelekea kuangusha machozi akiwa katikati ya show yake  ya MTV VMA’s 2015 jijini Los Angeles Marekani.
Siku ya Jumatano msanii huyo wa R&B Pop alialikwa kwenye kipindi cha ‘The Tonight Show’ cha Jimmy Fallon kuzungumzia maisha yake,video yake mpya pamoja na tukio lililotokea usiku wa MTV VMA’s siku ya jumapili August 30.
Justin Bieber kwenye kipindi cha The Tonight Show siku ya Jumatano 04 September 2015.
>>>“Nilifurahi kupita kiasi, nimefanya utoto mwingi hapa kati kati na wala sikutegemea kama watu wangeonyesha support kubwa sana kwangu siku ile kwa sababu mara ya mwisho mimi kuperform kwenye show nilizomewa sana nikajisikia vibaya”. <<< Justin Bieber.
Justin Bieber alikiri kuwa alikuwa mkorofi bila sababu za msingi, aliwakwaza wengi na alichukulia vitu vingi sana poa kiasi cha yeye kusahau tarehe ya uzinduzi wa moja ya album zake hivyo alihisi kuwa akirudi jukwani watu hawatampokea vizuri na pengine wengi wanamchukia.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametangaza kuwa ana $150,000 (£100,000) kwenye akaunti zake za benki, katika hatua inayolenga kupiga vita ufisadi katika nchi yake.
Kiasi hicho cha fedha kinaonyesha amekuwa akiishi ya kawaida sana tofauti na Makamu wake wa rais  Yemi Osinbajo ambaye ana utajiri wa kiasi cha $900,000 (£600,000) katika akaunti yake ya benki.
Rais huyo aliyeingia madarakani hivi karibuni anamiliki nyumba tano na mbili zikiwa za matope, pamoja na mashamba kadhaa.
Wakati akiingia madarakani aliwaahidi wananchi wake kukabiliana na ufisadi na kupambana na kundi hatari la Kigaidi la Boko Haram.
Taarifa zinasema ana shamba la matunda na ng’ombe 270, kondoo 25, farasi watano na ndege wengi.,Pia anamiliki hisa katika kampuni tatu.



Baada ya kuachia video ya wimbo wake ‘No Sleep’ aliomshirikisha J Cole kutoka kwenye album yake mpya ‘Unbreakable’, Janet Jackson amerudi tena kuziandika headlines zake kwenye kurasa za burudani.
Good news kwako mtu wangu, kama wewe ni miongoni mwa mashabiki wakubwa wa Janet Jackson basi hii ikufikie… Janet ameachia single mpya kutoka kwenye album yake mpya wimbo unaitwa ‘Unbreakable’ na ndio wimbo unaobeba jina la album mpya ya Janet Jackson.
janetJ
Album ya Janet Jackson ‘Unbreakable’ itakuwa sokoni mwezi October tarehe 2, hii ni album ya kwanza ya Janet Jackson ndani ya miaka 7 na utayarishaji wa album nzima umesimamiwa na label ya Janet iitwayo ‘Jackson’s Rhythm Nation Record Label’


SIMBA SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na KVZ usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa kirafiki.
Kocha Muingereza, Dylan Kerr hakumtumia kabisa mshambuliaji mpya, Msenegali Pape Abdoulaye N’daw na kwa mara ya kwanza leo alimuanzisha Joseph Kimwaga aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Azam FC.
Mshambuliaji Mganda Hamisi Kiiza aliisumbua mno ngome ya KVZ, lakini akashindwa kufunga bao, huku kipa Vincent Angban akiokoa michomo kadhaa ya hatari.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban/Dennis Richard, Emery Nimubona/Hassan Kessy, Hussein Rashid, Said Issa, Samih Nuhu, Justuce Majabvi, Issa Ngoa, Peter Mwalianzi/Danny Lyanga, Joseph Kimwaga/Mwinyi Kazimoto na Hamisi Kiiza/Awadh Juma.
KVZ; Ayoub Bakari, Emil Wiliam, Juma Abdallah/Abdillahi Seif, Iddi Mgeni, Makame Ali, Suleiman Abdulsalam, Masoud Abdallah, Isihaka, Salum Akida, Nasir Bakari na Abbas Abdallah.


KOCHA wa Timu ya Taifa ya Spain amesema Kipa David De Gea atajiamini zaidi kufuatia sakata lake la Uhamisho lililosababisha mvutano kati ya Klabu yake Manchester United na Real Madrid.
Vicente Del Bosque anaamini David de Gea anapaswa kufurahia mvutano huo kati ya Klabu kubwa kabisa Barani Ulaya.
De Gea alikuwa kwenye sakata la kuhamia Real Madrid lakini Uhamisho huo ulikwama Sekunde za mwisho hapo Agosti 31 baada ya Real Madrid kuchelewa kumsajili kwa wakati kwenye Mtandao wa FIFA wa Uhamisho wa Kimataifa, TMS [Transfer Matching System] na pia LFP, La Liga na kuziacha Klabu hizo mbili zikilaumiana.
Del Bosque amesema: “Lazima afurahie kwani Klabu kubwa zilikuwa zikimgombea. Sijaongea nae peke yake. Lakini anapaswa kufanya mazoezi. Yupo sehemu salama.”
Mapema Del Bosque alimuonya De Gea kuwa lazima arejee kuwa Kipa Namba Moja wa Man United ndipo arejeshwe Kikosini Spain baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Kipa wa Argentina Sergio Romero ambae amecheza Mechi zote 6 za Man United Msimu huu.

Hivi sasa De Gea yuko kwenye Timu ya Taifa ya Spain ikijitayarisha kucheza Mechi za Kundi lao la EURO 2016 Wikiendi hii dhidi ya Macedonia na Slovakia.
Akieleza zaidi, Del Bosque alisema: “"Jose Manuel Ochotorena [Kocha wa Makipa wa Spain] ameniambia De Gea yuko hali njema. Yupo amezungukwa na Juan Mata ambae ni Mtu mwema na hii itasaidia sana!”



Kadri siku zinavyo zidi kwenda tuna anza kujua mambo mengi yaliyokuwa nyuma ya pazia la usajili wa vilabu mbalimbali barani Ulaya, vipo vilabu ambavyo vilikosa wachezaji kwa sababu ya dau na mengine mengi. Ila usajili uliyoshindikana kutimia ni Pedro Rodriguez kushindwa kujiunga Man United wakati kila kitu kilikuwa tayari.
Pedro-602777
Ed Woodward alisafiri hadi Barcelona Hispania ili kukamilisha usajili wa Pedro kujiunga na Man United ila klabu ya Chelsea ndio iliizidi kete Man United, licha ya awali kuripotiwa kukubali kujiunga na Man United kwa dau la pound milioni 21.
Habari kutoka katika vyombo vya habari vya Uingereza zinaripoti kuwa Pedro alisitisha mpango wa kujiunga na klabu ya Man United baada ya kuwasiliana na Victor Valdes na David De Gea, baada ya kuwasiliana na hao na walimwambia kuhusu tatizo la Van Gaal na wachezaji Pedro akabadili mawazo.
Barcelona-341349
“Ni kweli sikupenda walivyofanyiwa wachezaji wenzangu hususa kwa Victor ambaye nimewahi kucheza nae timu moja, aliniambia kuhusu Man United kuwa ni klabu nzuri na ina mashabiki wengi ila tatizo ni kocha, nilizungumza vizuri na uongozi wa klabu, lakini na amini nilifanya maamuzi sahii kujiunga na Chelsea”>>> Pedro



Licha ya kuwa alishindwa kutamba katika klabu ya Manchester United kama ilivyokuwa matarajio ya wengi Dimitar Berbatov aliamua kutimkia katika klabu ya Fulham, AS Monaco na sasa kajiunga na klabu ya PAOK ya Ugiriki aliyojiunga nayo msimu huu.
2BF1729700000578-0-image-a-128_1441295520858
Mshambuliaji huyo wa Kibulgaria mwenye umri wa miaka 34 amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea katika klabu ya AS Monaco. Dimitar Berbatov ameingia katika usajili wa kihistoria wa klabu ya PAOK baada ya kusaini mkataba wa miaka 2.
2BF1722B00000578-0-image-a-126_1441295333059
Mara nyingi katika Ligi kubwa duniani mshambuliaji anayefanyiwa utambulisho maalum uwanjani ni yule mwenye jina kubwa pamoja na uwezo mkubwa uwanjani, licha ya Berbatov kuonekana kaisha uwanjani, kwa upande wa Ugiriki Septemba 3 ilikuwa ni siku yake maalum ya kutambulishwa mbele ya mashabiki 10000 katika uwanja wa Toumba.
2BF16D3600000578-0-image-a-127_1441295414401
0B8DC11B00000578-0-image-a-129_1441295673458
Dimitar Berbatov wakati yupo Man United

PIGO! DANNY WELBECK NJE MWEZI MMOJA


straika wa Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja hadi Krismasi baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti lake.
Welbeck, mwenye Miaka 24, aliumia Goti lake mwishoni mwa Aprili baada ya kuifungia Arsenal Bao 8 katika Mechi zake 34 tangu ahamie hapo kutoka Man United. 
Klabu ya Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni.
Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikujiimarisha kwa kununua Mchezaji yoyote wa mbele mbali ya kumnunua Kipa Mkongwe kutoka Chelsea Petr Cech.

waliotembelea blog