Wednesday, September 3, 2014

https://24tanzania.com/wp-content/uploads/2014/03/65df1bcd23_Mbwana-Samatta.jpg

Waswahili hawaishiwi vioja kwa tungo, nahau, mafumbo, methali hata vitendawili. Yote yanaakisi maisha ya jamii pana inayotuzunguka. Kwa leo nimeguswa na msemo usemao, nabii hakubaliki kwao.
Nimesimama peke yangu nikiamini kuwa wapo manabii ambao wanakubalika kwao. Utakubaliana nami kuwa kiwango alichonacho Mbwana Samatta hakuna mtanzania asiyekikubali. Kwa sasa Samatta ndiye chachu na roho ya Tp mazembe. Huwezi kumwambia kitu Moses Katumbi juu ya kijana huyu wa kitanzania.
Anaibeba timu kwa uwezo wake baada ya kuondoka Tresor Mputu aliyetimkia nchini Angola, sasa hakuna kama Samatta . Ukipita kwenye viunga vya mji wa Lubumbashi vijana wanapendeza kwa jezi ya Samatta. Timu yetu ya Taifa Stars jumapili hii iko dimbani kucheza na timu ya Taifa ya Burundi. Ni siku ambayo nabii ata zidhirisha unabii wake. Naamini sasa ni wakati wa Mbwana Samatta kuibeba Taifa Stars.
Tanzania imejaliwa kuwa na vipaji vingi katika medani mbalimbali, lakini kukosekana mipango thabiti na uthubutu miongoni mwa wachezaji ni tatizo katika kupata wachezaji wa kulipwa. Wenzetu Kenya wana nyota kadhaa wanaosukuma kandanda barani Ulaya.
Kama vile kwa Waganda ambao nao hawako nyuma, kwetu Samatta atabaki kuwa kioo cha taifa kwenye mpira wa miguu . Mechi ya jumapili itaamuliwa na ubora wa Mbwana Samatta. Kila la heri Taifa Stars kwenye mchezo huo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya shirikisho la soka duniani Fifa. Uzalendo wetu ni silaha tosha ya kuiangusha Burundi nyumbani kwao.

Continho,jaja kuonyesha vitu uwanja wa taifa leo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYSHw1SJV4mT1nIrmzq2E6seM7Gm024rAUvDIpOf2IUZ9bevfM4Jp81iyTV9KLKEu7kW0w_gaBLC2Olx_7MdmelmzVUfDsAC-d7nWAyXhkq4dV9vv6gi5beLdgdkCH1aJ2o3j48QZTQw7z/s1600/COUTINHO+NA+JAJA.jpg

Na Victor Simon- Mjengwabolg
Timu ya soka ya Yanga siku ya leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Thika United ya nchini Kenya,kwenye mchezo wa kujipima ubavu.
Mchezo huo ni maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara, ambayo inatarajia kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu. Maandalizi ya mchezo huo tayari yamekwisha kamilika,huku timu hizo zikitarajiwa kutoa burudani kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania.
Kumekuwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa timu zote mbili,zikijinasibu kushinda mchezo huo.Huu ni mchezo wa nne wa kocha Marcio Maximo tangu achukuwe mikoba ililoachwa wazi na kocha Hans Der Plujim ambae alifungashiwa virago.Kwenye michezo mitatu ya mwanzo timu ya Yanga imeweza kuibuka na ushindi kwenye michezo yote .
Ushindi huo ukichagizwa na ujio wa wachezaji wa kibrazil, Continho na Jaja ambao wamekuwa kivutio kwa wapenzi wa soka, tayari wapenzi wa soka wa visiwani wamepata fursa ya kuwaona wachezaji hao.Sasa ni zamu ya wapenzi wa soka wa Tanzania bara.Continho,jaja kuonyesha vitu uwanja wa taifa leo

Ushindi huo ukichagizwa na ujio wa wachezaji wa kibrazil, Continho na Jaja ambao wamekuwa kivutio kwa wapenzi wa soka, tayari wapenzi wa soka wa visiwani wamepata fursa ya kuwaona wachezaji hao.Sasa ni zamu ya wapenzi wa soka wa Tanzania bara.

 Keki ndio hii hapa sasa

UHAMISHO uliochelewa wa Kiungo wa Manchester United Tom Cleverley kwenda Aston Villa kwa Mkopo wa Msimu mmoja umebarikiwa hii Leo wakati Lejendari wa Man United David Beckham amesikitishwa kuondoka kwa David Welbeck kutoka Man United kwenda Arsenal.
Dirisha la Uhamisho lilifungwa rasmi Jana Usiku lakini Uhamisho wa Cleverley ulichelewa lakini hivi sasa Bodi ya Ligi Kuu imeubariki. 

Makubaliano kati ya Man United na Aston Villa yana vipengele kwamba Cleverley, mwenye Mkataba na Man United hadi 2015, anaweza kurudi Old Trafford Mwezi Januari au Villa imsaini kwa kudumu katika Kipindi hicho cha Usajili.
Cleverley, mwenye Miaka 25, amekulia toka Vyuo vya Soka vya Man United tangu akiwa mdogo na kuichezea Klabu hiyo Mechi 79.

David Beckham amesikitishwa na kuondoka kwa Danny Welbeck na kuhamia Arsenal.
Beckham amesema Arsenal wamepata dhahabu kwa kumnunua Welbeck na kuonyeshwa kusikitishwa kwake kumpoteza Mchezaji aliekuzwa kipaji toka Chuo cha Soka cha Man United tangu akiwa na Umri wa Miaka 8.

Beckham amesema: “Ni wazi kumwona Danny kuondoka, kwa mimi Shabiki wa Man United, kunasikitisha lakini mie si Meneja!”

Manchester United imekubaliana na AS Monaco ya France kumsaini Straika wa Colombia Radamel Falcao kwa Mkopo na wakati huo huo Straika wao Javier Hernandez anahamia Real Madrid ya Spain pia wa Mkopo.
Falcao anatarajiwa kuwasili Jijini Manchester kupimwa afya yake na tayari Chicharito nae yuko huko Madrid kupimwa afya.
Falcao alijiunga na AS Monaco Mei 2013 kwa Dau la Pauni Milioni 50 kutoka Atletico Madrid na kufunga Bao 11 katika Mechi alizoichezea.
Msimu huu Falcao amefunga Bao 2 katika Mechi 3.
Dili ya Falcao kwenda Man United pia ina makubaliano kuwa wanaweza kumnunua moja kwa moja kwa Dau la Pauni Milioni 43.5
Radamel Falcao of Manchester United poses with Assistant Manager Ryan Giggs after signing for the club on loan on September 1, 2014 in Manchester, England.Radamel Falcao akiwa na Kocha Msaidizi Ryan Giggs kwenye picha ya pamojaWe're still waiting: Marcos Rojo (left) joined United over a week ago but his visa is still not finalisedMarcos Roja aliyesainiwa tangu wiki iliyopita nae tayari alishatua lakini swala la Visa bado ni kitendawili mpaka sasa kitu kilichomkwamisha mpaka sasa kutocheza mechi yoyote na Klabi hiyo ya Mashetani wekundu.

Manchester United imetangaza kumsaini Mchezaji wa Kimataifa wa Netherlands Daley Blind kutoka Ajax kwa Dau la Pauni Milioni 14.
Proud: The 24-year-old cost £14million from Ajax and said 'it is a real honour to sign for Manchester United'Blind, ambae ndie Mchezaji Bora wa Mwaka wa Netherlands, anaungana tena na Meneja wa Man United Louis van Gaal ambae walikuwa pamoja huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia wakati Van Gaal ni Meneja wa Netherlands na kufika Nusu Fainali.
Staa huyo mwenye Miaka 24 amesaini Mkataba wa Miaka Minne wenye kipengele cha Nyongeza ya Mwaka mmoja ukimalizika.
Blind, ambae ni Mtoto wa Mchezaji wa zamani wa Ajax na Netherlands, Danny Blind, anaweza kucheza kama Beki na pia Kiungo.

Fit: Blind  his new United team-mate Van Persie took part in the session despite fears of the latter's injuryMara baada ya kukamilisha Usajili wake, Blind alisema ni heshima kubwa kuichezea Man United.
Nae Van Gaal alisema: “Nimefurahi kumsaini Daley. Ni Mchezaji mwenye akili na anaeweza kucheza Namba nyingi.”
Blind: 'I have been at Ajax since I was seven years old and I will always have very fond memories of the club'

MANCHESTER UNITED
NDANI:
Ander Herrera
(Athletic Bilbao) Ada haikutajwa
Luke Shaw (Southampton) Ada haikutajwa Vanja Milinkovic (Vojovdina) Ada haikutajwa Marcos Rojo (Sporting Lisbon) €20m Angel Di Maria (Real Madrid) £59.7m
Radamel Falcao (AS Monaco) Mkopo £6m NJE:
Federico Macheda
(Cardiff City) Bure
Jack Barmby (Leicester City) Bure Rio Ferdinand (QPR) Bure Ryan Giggs Ameachwa Nemanja Vidic (Inter Milan) Bure Alexander Buttner (Dynamo Moscow) Ada haikutajwa Patrice Evra (Juventus) Ada haikutajwa
Nani
(Sporting Lisbon) Mkopo
Wilfried Zaha (Crystal Palace) Mkopo
Danny Welbeck (Arsenal) £16m
Javier Hernandez (Real Madrid) Mkopo

waliotembelea blog