Friday, December 4, 2015


Kamati kuu ya shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, imeidhinisha mageuzi yanayonuiwa kufufua hadhi ya shirikisho hilo lililokumbwa na kashfa nyingi.
Mapendekezo hayo yaliyoidhinishwa wakati wa mkutano wa kamati hiyo mjini Zurich inajumuisha sheria inayosema rais wa shirikisho hilo na maafisa wakuu wanaweza kuhudumu kwa kipindi cha miaka kumi
na miwili pekee na pia kuwepo kwa uchunguzi wa kina kuhusiana na maadili ya maafisa wa shirika hilo.
Uamuzi wa kuongeza idadi ya nchi zinazoshiriki katika fainali ya kombe la dunia kutoka 32 hadi 40 iliahirishwa hadi pale uchunguzi kuhusu athari zake utakapomalizika.

Mapendekezo hayo sasa yatawasilishwa wakati wa mkutano wa kamati kuu ya FiFA Februari mwaka ujao.
Awali maafisa wa polisi mjini Zurich waliwakamata manaibu wa rais wawili wa shirikisho hilo kama sehemy ya uchunguzi wao kuhusiana na madai ya ufisadi na hongo.
Polisi walifika katika hoteli ya kifahari ya Baur au Lac mjini humo na wakaonekana wakiondoka na watu wawili.
Shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema litashirikiana kikamilifu na wachunguzi.
Hii ni mara ya pilikwa hoteli hiyo inayotumiwa na maafisa wa Fifa kuvamia na polisi mwaka huu huku tuhuma za ufisadi zikiendeleakulizonga shirikisho hilo.
Mkutano wa siku mbili wa kamati tendaji ya Fifa unaendelea katika mji huo.


LEO huko Addis Ababa Nchini Ethiopia, Rwanda na Uganda zimefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Chalenji baada ya kushinda Mechi zao za Nusu Fainali kwa Mikwaju ya Penati.
Katika Nusu Fainali ya kwanza, Sudan, waliocheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 23 baada ya Bakri Almadina kupewa Kadi Nyekundu, na Rwanda zilitoka 0-0 katika Dakika 90 na Gemu kwenda Nyongeza za Dakika 30 na ndipo Sudan kutangulia kufunga kwa Bao la Atahir Babakir la Dakika ya 100 lakini Rwanda walisawazisha kupitia Jean Baptiste Mugiraneza kwenye Dakika ya 110.
Rwanda walibaki Mtu 10 katika Dakika ya 121 baada ya Isaie Songa kupewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga Kipepsi Beki wa Sudan.
Hadi Dakika za Nyongeza 30 kumalizika, Bao zilikuwa 1-1 na ndipo ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano ambazo Rwanda walitoka kidedea kwa Penati 4-2.
Nao Uganda na Wenyeji Ethiopia walicheza Dakika 120 bila kufungana na kisha Uganda kuingia Fainali kwa Penati 5-3.

RATIBA/MATOKEO:
Robo Fainali

Jumatatu Novemba 30

Uganda 2 v Malawi 0
Kilimanjaro Stars 1 v Sudan 1 [Ethiopia yasonga kwa Penati 4-3]

Jumanne Desemba 1
South Sudan 0 v Sudan 0 [Sudan yasonga kwa Penati 5-3]
Rwanda 0 v Kenya 0 [Rwanda yasonga kwa Penati 5-3]

Nusu Fainali
Alhamisi Desemba 3

Sudan 1 v Rwanda 1 [Sudan yasonga kwa Penati 4-2]

Uganda 0 v Ethiopia 0 [Uganda yasonga kwa Penati 5-3]

Jumamosi Desemba 5
Mshindi wa Tatu

Ethiopia v Sudan

Fainali
Uganda v Rwanda


Belgium imebaki Nambari Wani kwenye FIFA Listi ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo huku Tanzania ikipanda Nafasi 3.
Mabingwa wa Dunia Germany wameshuka Nafasi 2 na sasa wapo Nafasi ya 4 wakati Argentina wakipinda Nafasi 1 na kushika Nafasi ya Pili na Spain kupanda Nafasi 3 na kukamata Nafasi ya 3.
Brazil nao wapo Nafasi ya 6 baada kupanda Nafasi 2.
Tanzania sasa ipo Nafasi ya 132 baada ya kupanda Nafasi 3 toka Mwezi uliopita.
Kwa Afrika, Timu ya juu kabisa kwenye Listi ya Ubora ni Ivory Coast ambayo ipo Nafasi ya 19 baada ya kupanda Nafasi ikifuatiwa na Algeria ambayo ipo Nafasi ya 28 baada ya kuporomoka Nafasi 2.

10 BORA:
1. Belgium
2. Argentina
3. Spain
4. Germany
5. Chile
6. Brazil
7. Portugal
8. Colombia
9. England

10. Austria


Sir Alex Ferguson amemuunga mkono Mchezaji wa zamani wa Manchester United Gary Neville kufanikiwa kama Meneja mara baada ya kuteuliwa kuiongoza Valencia ya Spain hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Neville, mwenye Miaka 40, alitumia maisha yake yote ya uchezaji Soka akiwa chini ya Sir Alex Ferguson huko Manchester United ambako alicheza Mechi 602 na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Englamnd mara 8, FA CUP mara 3, Kombe la Ligi mara 2 na UEFA CHAMPIONS LIGI wakati akiwa Mchezaji kati ya 1993 na 2011.
Sir Alex anaamini kipaji cha Gary Neville kilichompa mafanikio kama Mchezaji na pia Mchambuzi wa Soka kitamsaidia kupata mafanikio kama Meneja.
Ferguson ameeleza: “Gary ana sifa nyingi zinazoonyesha atafanikiwa kama Meneja. Umahiri kama Kiongozi, uaminifu na uchapa kazi wake. Ni Mtu ambae haogopi kufanya maamuzi makubwa na hiyo ni sifa kubwa kwa Mtu anaeongoza. Nadhani atafanya vizuri na namtakia yeye na Ndugu yake Phil, kila la heri.”

Neville, ambae pia aliichezea England mara 85, aliteuliwa kuwa Meneja mpya wa Valencia hapo Jana na Mmiliki wa Klabu hiyo ya La Liga Peter Lim ambae ni Tajiri kutoka Singapore ambae pia ni Rafiki wa Neville.
Uteuzi huo ulimfanya Neville ajiuzulu kama Mchambuzi wa Sky Sports lakini atabaki kama Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya England chini ya Roy Hodgson.
Baada ya kujiuzulu kwa Kocha Nuno Wikiendi iliyopita baada ya kufungwa 1-0 kwenye La Liga na Sevilla na kutupwa Nafasi ya 9, Valencia iliwekwa chini ya uongozi wa muda wa Phil Neville, mdogo wa Gary Neville ambae aliteuliwa kama Meneja Msaidizi tangu Julai, pamoja na Voro, ambae ndie kaimu Meneja.
Jana Voro na Phil Nevill waliiongoza Valencia kuifunga Barakaldo 3-1 kwenye Copa del Rey na pia wataendelea kuiongoza Jumamosi itakapopambana na Barcelona kwenye La Liga.
Mechi ya kwanza ya Valencia chini ya Gary Neville itakuwa Desemba 9 dhidi ya Lyon ikiwa ni Mechi ya Kundi H la UEFA CHAMPIONS LIGI.

waliotembelea blog