Thursday, September 24, 2015


Kipa De Gea  amesema anasikia fahari kubwa kufanywa Kepteni wa Manchester United Jana Usiku wakati walipoifunga Ipswich Town 3-0 Uwanjani Old Trafford katika Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup.
David De Gea alirejeshwa Kikosi cha Kwanza cha Man United Mwezi huu baada ya kutupwa nje kutokana na sakata lake la kuhamia Real Madrid.
Jana, baada ya Kepteni Wayne Rooney kutoka Uwanjani alipobadilishwa na Memphis Depay katika Dakika ya 81, utepe wa Kepteni ulipelekwa kwa David De Gea.



Klabu ya soka ya Arsenal ilikuwa ikihusishwa kutaka kuwasajili wachezaji kadhaa katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August lakini haikufanikiwa na hatimaye ilifanikiwa kumsajili kipa wa zamani wa Chelsea Peter Cech kwa dau la pound milioni 10, miongoni mwa majina yaliyokuwa yakitajwa kutaka kusajiliwa na Arsenal ni Karim Benzema, Edinson Cavani na Robert Lewandowski.
hi-res-8c82e974577ebf25df8b128ad56dacb7_crop_north
Robert Lewandowski
September 24 stori kutoka mtandao wa express.co.uk umeandika chanzo cha Arsenal kuwakosa nyota hao, licha ya Robert Lewandowski kutopewa kipaumbele katika klabu yake ya FC Bayern Munich chini ya kocha Pep Guardiola, wakala wa mchezaji huyo Cezary Kucharski alithibitisha kuwa Lewandowski haipendi hali ya hewa ya Uingereza.
Karim-Benzema-celebrates--007
Karim Benzema
Karim Benzema alikuwa ni  mmoja kati ya mastaa wa soka waliokuwa wakisakwa na Arsenal katika kipindi cha usajili cha mwezi August, kwani alikuwa akihusishwa kujiunga na Arsenal kwa dau la poundi milioni 40. Lakini nguli wa zamani wa klabu ya Arsenal Ian Wright alilaumu mipango ya Arsenal kwani kilichofanya Arsenal wamkose Benzema ni kutokwenda kufanya mazungumzo ya awali na mchezaji kwani kufanya hivyo Ian Wright ana amini ingesaidia. Ila amekiri kuumizwa na tweet ya Benzema ya kusema Real Madrid ni nyumbani.
Paris Saint-Germain's Uruguayan forward Edinson Cavani celebrates after scoring a goal during the French League Cup round of sixteen football match between Paris Saint-Germain (PSG) and Saint-Etienne (ASSE) on December 18, 2013 at the Parc des Princes stadium in Paris. AFP PHOTO / THOMAS SAMSON (Photo credit should read THOMAS SAMSON/AFP/Getty Images)
Edinson Cavani
Kwa  upande wa Edinson Cavani licha ya picha ya yeye akiwa pamoja na kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuvuja wakiwa Ufaransa, alinukuliwa kukiri kuhitajika na Wenger katika baadhi ya magazeti ya Ufaransa lakini amekuwa akiuhusishwa kujiunga na vilabu kadhaa katika dirisha la usajili la mwezi August lakini PSG ni mahali sahihi kwake na bado wanamuamini.
Wenger-352204
Wenger

Stori za soka la wanawake kukua zimezidi kuchukua nafasi duniani kote ila kinachovutia ni kuwa utamaduni wa nchi za kiarabu ambazo zimekubali kuunga mkono soka la wanawake lakini kwa baadhi ya masharti kwa washiriki hao kama mavazi na mengineyo.
September 24 ninayo stori kutoka Iran inayohusu soka la wanawake, ambapo timu ya taifa ya Iran ya wanawake ambayo inashiriki michuano ya mpira wa miguu Nilai Malaysia, inashiriki mashindano hayo bila kuwa na nahodha wake Niloufar Ardalan, nahodha huyo hayupo na timu Malaysia kwa sababu mume wake amegoma kusaini nyaraka ili mkewe apate kibali cha kusafiri nje ya Iran.
mideast-iran-ardalan-310x415
Sheria ya nchi ya Iran hairuhusu mwanamke kusafiri nje ya nchi pasipo ruhusa ya mumewe, yaani hii ni tofauti kidogo na kwetu kwani tumezoea kuona wanawake wakikatazwa kufanya vitu flani na wame zao, lakini bado wana nafasi ya kuendelea kufanya kwani sio kosa kisheria kufanya maamuzi yako.
Kwa Iran mwanamke lazima mumewe asaini nyaraka rasmi ili mkewe aweze kusafiri nje ya nchi, hivyo nahodha wa timu hiyo ya Iran Niloufar Ardalan ameshindwa kusafiri kwenda Malaysia kwa sababu ya mumewe lakini hii ndio kauli yake.
201162673751812734_20
“Haya mashindano yalikuwa muhimu sana kwangu kama mwanamke wa kiislamu nilikuwa nataka kupeperusha bendera ya nchi yangu katika mashindano hayo na sio kusafiri kwa kujifurahisha, nafikiri mamlaka husika zingetengeneza sheria za kuwalinda wanamichezo wa kike hususani katika hali kama hi



Viingilio vya mchezo wa watani wa jadi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania utakaochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam vimetangazwa leo ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu saba (7,000).
atika mchezo huo kiingilio cha juu kitakua ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000) kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha shilingi Elfu Saba (7,000) kikiwa ni kwa viti vyenye rangi ya Blu, Kijani na Orange.
Tiketi za mchezo ho zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vifuatavyo: Karume – Ofisi za TFF, Buguruni – Oilcom, Dar Live – Mbagala, Uwanja wa Taifa, Luther House – Posta, Ferry – Kivukoni, Mnazi Mmoja, Ubungo – Oilcom na Makumbusho – Standi ya mabasi ya daladala.
TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchin kununua tiketi katika magari yaliyopo kwenye vituo vya kuuzia tiketi ili kuondokana na kuuziwa tiketi zisizo sahihi.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya FIFA, Israel Nkongo (Dsm) akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Ferdinand Chacha (Mwanza) mwamuzi wa akiba Soud Lila (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo atakua Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku hiyo ya Jumamosi itakua ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Maafande wa jeshi la Magereza (Tanzania Prisons) watawakaribisha maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.



Zimeibuka taarifa kuwa Daktari wa Chelsea Mwanamama Eva Carneiro ameacha kazi Klabuni hapo na yupo mbioni kuifungulia Mashitaka.
Dokta huyo aliondolewa kuihudumia Timu ya Kwanza ya Chelsea baada ya Mechi ambayo Chelsea walitoka 2-2 na Swansea hapo Agosti 8.
Katika Mechi hiyo,Dokta Carneiro na Tabibu wa Viungo Jon Fearn waliingia Uwanjani kumtibu Eden Hazard kwenye Dakika za Majeruhi wakati Chelsea ipo 2-2 na Swansea City huku wakiwa Mtu 10 baada ya mapema Kipa wao Thibaut Courtois kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Kitendo hicho kilimkera Mourinho kwani Mchezaji akihudumiwa na Madokta basi huwajibika kutoka nje ya Uwanja na husubiri amri ya Refa kuingia tena huku Gemu ikiendelea na hilo liliiacha Chelsea iwe Mtu 9 kwa Dakika kadhaa.
Mourinho alimponda Dokta huyo na kumsema hajui mchezo unakwendaje.
Tukio hilo lilizua hisia kali na Juzi Mdau mmoja kuamua kulalamika kwa FA, Chama cha Soka England, kuwa Mourinho alimfokea Dokta Eva Caerneiro kwa kutumia lugha chafu na sasa FA imeamua kuchunguza tukio hilo.
Imeripotiwa kuwa Dokta Eva Carneiro alitakiwa arudi kazini tangu Ijumaa iliyopita lakini hakufanya hivyo na sasa yuko mbioni kusaka Sheria katika mamlaka husika.


Mathieu Flamini  akipeta!Mathieu Flamini alipoifungia bao la pili Arsenal na kufanya 2-1 dhidi ya Spurs 2-1Calum Chambers (21) kajifunga goli na kuwazawadia bao wapinzani wao Tottenham kwa kuisawazishia bao Spurs kwa kufanya 1-1.


Umati wa Wananchi wa Lindi Mjini, wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili, Mkoani Lindi leo Septemba 23, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, LINDI.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia Wananchi, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, akimueleza Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, changamoto mbalimbali za wananchi wa Lindi, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo lake hilo, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.

Sehemu ya Wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, wakimshangilia Mgombea Ubunge wao, Salum Barwany, alipokuwa akihutubia na kukonga nyoyo zao kwa kugusa moja kwa moja changamoto zinazowakabili na namna watakavyoweza kuzitatua iwapo watapata ridhaa ya uongozi.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akifurahi jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany.

Uwanja wa Pilipili ulikuwa ni shangwe tupu, muda wote wa Mkutano.

Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.

waliotembelea blog