Mfahamu Asha-Rose Migiro, mmoja wa wagombea watano. Ni Mbunge wa kuteuliwa katika bunge, na waziri wa sheria na katiba Tanzania. Mhe. Migiro amesomea sheria katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na shahada ya uzamivu yake katika chuo cha Konstanz (Ujerumani). Kabla ya kujiunga na siasa, alikua mhadhiri mkuu wa mafunzo ya sheria Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam. Pia aliwahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (2007-2012) #KaribuDodoma UMOJA NI USHINDI!
Mfahamu Amina Salum Ali, mmoja wa wagombea watano. Aliwahi kuwa waziri wa Fedha (Zanzibar; 1990-2000), na ni balozi wa Umoja wa Mataifa ya Afrika nchini Marekani (2007-2015). Amesomea uchumi katika chuo cha Delhi na pia ana MBA ya Masoko kutoka chuo cha Pune. #KaribuDodoma UMOJA NI USHINDI!
Mfahamu January Makamba, mmoja wa wagombea watano. Ni Mbunge wa Bumbuli (2010-2015), na naibu waziri wa mawasiliano, sayansi, na teknolojia Tanzania (2012-2015). Amesomea shahada ya uzamivu katika diplomasia na usuluhishi wa migogoro katika chuo cha George Mason, kabla ya kuwa msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete. #KaribuDodoma UMOJA NI USHINDI!