Saturday, July 11, 2015


Mfahamu Bernard Kamilius Membe, mmoja wa wagombea watano. Ni mbunge wa jimbo la Mtama (2000 - 2015), na waziri wa mambo ya nje Tanzania (2007-2015). Mhe. Membe amesomea Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na Mahusiano ya Kimataifa katika chuo cha Johns Hopkins, na amepitia mafunzo ya kijeshi (nationa service) kwa mwaka mmoja katika kambi la kijeshi la Oljoro (Arusha) #KaribuDodoma UMOJA NI USHINDI!Mfahamu John Pombe Magufuli, mmoja wa wagombea watano. Ni mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki Tanzania, na ni waziri wa ujenzi (2010-2015). Amesomea shahada ya uzamivu ya Kemia katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam. #KaribuDodoma UMOJA NI USHINDI!

Mfahamu Asha-Rose Migiro, mmoja wa wagombea watano. Ni Mbunge wa kuteuliwa katika bunge, na waziri wa sheria na katiba Tanzania. Mhe. Migiro amesomea sheria katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na shahada ya uzamivu yake katika chuo cha Konstanz (Ujerumani). Kabla ya kujiunga na siasa, alikua mhadhiri mkuu wa mafunzo ya sheria Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam. Pia aliwahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (2007-2012) #KaribuDodoma UMOJA NI USHINDI!

Mfahamu Amina Salum Ali, mmoja wa wagombea watano. Aliwahi kuwa waziri wa Fedha (Zanzibar; 1990-2000), na ni balozi wa Umoja wa Mataifa ya Afrika nchini Marekani (2007-2015). Amesomea uchumi katika chuo cha Delhi na pia ana MBA ya Masoko kutoka chuo cha Pune. #KaribuDodoma UMOJA NI USHINDI!
Mfahamu January Makamba, mmoja wa wagombea watano. Ni Mbunge wa Bumbuli (2010-2015), na naibu waziri wa mawasiliano, sayansi, na teknolojia Tanzania (2012-2015). Amesomea shahada ya uzamivu katika diplomasia na usuluhishi wa migogoro katika chuo cha George Mason, kabla ya kuwa msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete. #KaribuDodoma UMOJA NI USHINDI!

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog