Thursday, July 10, 2014


Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boyz) inacheza mechi ya kujipima nguvu kesho (Julai 11 mwaka huu) dhidi ya Azam U-20 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la Serengeti Boyz likiongozwa na kocha Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa 2 kamili asubuhi.
Serengeti Boyz itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) siku ya Ijumaa, Julai 18 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.
Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boyz ni Abdallah Shimba, Abdulrasul Bitebo, Abutwalibu Mshery, Adolf Bitegeko, Ally Mabuyu, Ally Mnasi, Amin Noren, Athanas Mdamu, Badru Othman, Baraka Baraka, Hatibu Munishi na Issa Athuman.
Wengine ni Juma Yusuf, Kelvin Faru, Kelvin Kamalamo, Martin Luseke, Mashaka Ngajilo, Mechata Mnata, Mohamed Abdallah, Mussa Vicent, Nazir Barugire, Omary Omary, Omary Wayne, Prosper Mushi, Seif Seif na Yahya Hafidh.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Wesley Sneijder anaweza kuwa huru kujiunga na Manchester United ikiwa Dau la Pauni Milioni 15.9 litatolewa ambacho ndio Kiwango kilichopo kwenye Mkataba wa Mchezaji huyo wa Netherlands kuruhusiwa kuihama Galatasaray ndani ya muda wa Mkataba wake. 
Inasadikiwa Man United, baada kumchukua Meneja mpya Louis van Gaal ambae sasa yuko pamoja na Sneijder huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia wakiwa na Netherlands, inataka kumsaini Kiungo huyo wa Miaka 30 kufuatia mapendekezo ya Van Gaal.
Mwezi uliopita, huko Brazil, Sneijder alifichua kuwa itakuwa ngumu kwake kuikataa nafasi ya kucheza chini ya Van Gaal.
Akiongea kwenye Mahojiano na Wanahabari wakati wa kumtambulisha Meneja wao mpya Cesare Prandelli, Rais wa Galatasaray, Unal Aysal, amesema: “Sneijder ni Mchezaji mzuri. Tunataka abaki Galatasaray lakini tukipata Euro Milioni 20 hatuwezi kumzuia. Hilo lipo kwenye Mkataba wake.”
Man United tayari imeshatumia Pauni Milioni 60 kuwanunua Wachezaji wapyya wawili Ander Herrera na Luke Shaw huku Thomas Vermaelen wa Arsenal akitajwa kuwafuata hao na Juventus kuitaka Man United kulipa Pauni Milioni 45 ikiwa wanamtaka Kiungo wa Chile Arturo Vidal.


NIGERIA imesimamishwa na FIFA baada ya Shirikisho la Soka la Nigeria, NFF, kuingiliwa shughuli zake.
Hii Leo FIFA imetoa taarifa kwamba Kamati ya Dharura imeamua kuisimamisha Nigeria mara moja baada Mahakama Kuu ya Jos, Plateau State, kusimamisha shughuli za NFF na kumtaka Waziri wa Michezo wa Nigeria kumteua Mtu kuendesha shughuli za NFF.
FIFA imesema maamuzi hayo ni kinyume na Kanuni ya 13, Aya ya 1 na Kanuni ya 17, Aya ya 1 ya Sheria za FIFA ambazo zinataka Vyama vya Wanachama wake kuendeshwa huru na kutoingiliwa na upande mwingine wowote.

Hapo Julai 4, Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, aliiandikia Nigeria na kuipa hadi Julai 8 kuirudisha Madarakani NFF na kutoingiliwa tena kwa namna yeyote.
Barua ya Valcke iliikumbusha Nigeria wajibu wake wa kuiruhusu NFF kuendesha shughuli zake bila kuingiliwa na Mtu yeyote kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya Sheria za FIFA.
Pia Barua hiyo iliionya Nigeria kuwa endapo NFF haitarejeshwa madarakani ifikapo Julai 8 basi Vyombo husika vya FIFA vitachukua hatua zaidi ikiwa pamoja na kuisimamisha Nchi hiyo kwenye shughuli zote za Kimataifa za Soka ikimaanisha kufungiwa kwa Timu yao ya Taifa na Klabu zao zote kucheza michuano ya Kimataifa.
Uamuzi huu wa Leo utaifaya Nigeria isiweze kushiriki Mashindano yeyote ya Kimataifa.


Head coach Louis van Gaal of the Netherlands looks on prior to the 2014 FIFA World Cup Brazil Semi Final match between Netherlands and Argentina at Arena de Sao Paulo on July 9, 2014 in Sao Paulo, Brazil.
KOCHA wa Netherlands Louis van Gaal ametoboa kuwa alipata shida sana kumpata Mchezaji wa kupiga Penati ya Kwanza ilipofikia hatua ya Mikwaju ya Penati Tano Tano baada Timu yake na Argentina kutoka 0-0 katika Dakika 120 za Nusu Fainali ya Kombe la Dunia hapo Jana.
Kwenye Penati hizo, Argentina waliibuka kidedea kwa kushinda Penati 4-2 baada Holland kukosa Penati mbili zilizopigwa na Ron Vlaar na Wesley Sneijder na Kipa Sergio Romero kuokoa.
Beki Ron Vlaara ndie aliepiga Penati ya Kwanza.
Lakini Louis van Gaal, ambae Timu yake iliitoa kwenye Robo Fainali Costa Rica kwa Penati ambazo mbili kati yake ziliokolewa na Kipa wa Akiba Tim Krul alieingizwa Dakika za Mwishoni kwa ajili tu ya Penati, Jana alishindwa kutumia mbinu hiyo hiyo baada ya kuwa tayari washabadilisha Wachezaji Watatu.
Head coach Louis van Gaal of the Netherlands instructs to Daryl Janmaat before the extra time during the 2014 FIFA World Cup Brazil Semi Final match between Netherlands and Argentina at Arena de Sao Paulo on July 9, 2014 in Sao Paulo, Brazil.Akiongea na Wanahabari mara baada ya Mechi, Van Gaal alisema: “Ile na Costa Rica ingetupa imani kwani tulipiga vizuri sana. Lakini tatizo lilikuwa nani apige ya kwanza na niliwaomba Wachezaji Wawili na mwishoe nikaangukia kwa Vlaar. Yeye ndie alikuwa Mchezaji bora hivyo angekuwa anajiamini mno. Lakini hii inaonyesha jinsi ilivyokuwa ngumu kupiga Penati kwenye Penati Tano Tano.”
Aliongeza: “Ni mbaya mno, kupoteza Mechi kwa Penati. Ukiondoa yote, tulikuwa sawa na wao, kama sio Timu bora. Inahuzunisha sana!”

Lionel Messi of Argentina shoots and scores a goal in a penalty shootout during the 2014 FIFA World Cup Brazil Semi Final match between the Netherlands and Argentina at Arena de Sao Paulo on July 9, 2014 in Sao Paulo, Brazil.Messi akifunga penati
 Kwenye Mikwaju Mitano ya Penati, Lionel Messi alianza kuifungia Argentina na Ron Vlaar kukosa kwa Netherland baada Kipa kuokoa, kisha Arjen Robben akafunga na Ezequiel Garay kuipa Argentina 2-1.
Sergio Romero of Argentina reacts after saving the penalty kick of Wesley Sneijder (not pictured) in a shootout during the 2014 FIFA World Cup Brazil Semi Final match between the Netherlands and Argentina at Arena de Sao Paulo on July 9, 2014 in Sao Paulo, Brazil.Sergio Romeo akiokoa mkwajuWesley Sneijder alikosa penati...!
Maxi Rodriguez of Argentina shoots and scores his penalty kick in a shootout to defeat the Netherlands during the 2014 FIFA World Cup Brazil Semi Final match between the Netherlands and Argentina at Arena de Sao Paulo on July 9, 2014 in Sao Paulo, Brazil.Maxi alifunga penati..
Akaja Wesley Sneijder na kukosa kwa Kipa kuokoa huku Sergio Aguero akifunga na Argentina kuwa 3-1 mbele.
Dirk Kuyt akafunga kwa Netherlands na kuwa 3-2 lakini Maxi Rodriguez akapiga Penati ya 4 na Argentuna kushinda 4-2.
Maxi Rodriguez of Argentina celebrates after scoring a penalty in the penalty shootout to win the 2014 FIFA World Cup Brazil Semi Final match between Netherlands and Argentina at Arena de Sao Paulo on July 9, 2014 in Sao Paulo, Brazil.Maxi akishangilia penati aliyofungaFuraha kwa Wachezaji wa Argentina baada ya kufunga mikwaju ya penatiKipa wa Netherlands hoi!!!

waliotembelea blog