Friday, July 4, 2014

MESSI-ARGENTINA2014DIEGO ARMANDO MARADONA, Lejendari wa Argentina, amesema Nchi yao inacheza chini ya kiwango, wanamtegemea sana Lionel Messi na lazima waongeze juhudi ikiwa watataka kuifunga Belgium kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia ambayo watakutana Jumamosi Usiku.
Maradona amesema: “Bado hatujaanza! Lazima watambue wazi, waweke vichwani mwao, si kumtegemea Messi tu. Labda anaweza kufunga Bao safi…lakini kama hakuweza, wasimrukie Kijana huyu na kumfanya ndie mwenye hatia ya maafa ya Argentina!”
Maradona, ambae ndie alikuwa Kocha wa Argentina kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 huko Afrika Kusini walikotolewa Robo fainali, alikuwa akihojiwa na TV ya Venezuela mara baada ya Argentina kuitoa kwa mbinde Switzerland kwa Bao 1-0 la mwishoni la Dakika za Nyongeza 30 lililofungwa na Angel Di Maria baada kazi njema ya Messi.
Akizungumzia Mechi hiyo, Maradona alisema: “Mtu kwa Mtu, na kwa pamoja, Argentina walikuwa bora, Wao [Uswisi] wanatengeneza Saa nzuri sana lakini wana Wanasoka wachache.”
Huko Brazil, Argentina wameshinda Mechi zao zote 4 hadi sasa na kufunga Bao 7 huku Messi akifunga Bao 4 kati ya hizo lakini ushindi wote huo ulikuwa wa tofauti ya Bao 1 tu.
Katika Mechi zote hizo 4, Messi ndie alieibuka na Tuzo ya Mchezaji Bora wa kila Mechi.
Maradona aliongeza “Huyu Kijana [Messi] yuko mpweke..Timu haibadilishi kasi yake, Mastraika hawazunguki. Nasikia uchungu, hasira, fedheha, kwa sababu Argentina inaweza kucheza vizuri zaidi, tena zaidi…Kocha lazima alazimishe hili! Kama hawataongeza ubora dhidi ya Belgium, basi tuko mashakani! ”
Argentina wameshatwaa Kombe la Dunia mara mbili na wakitwaa kwa mara ya 3, tena nyumbani kwa Mahasimu wao Wakuu Brazil, hiyo itakuwa starehe kubwa kwa Mashabiki wa Argentina ambao Maelfu yao wamefurika Brazil kushangilia Timu yao.

RAIS mpya wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, ameanza kazi yake rasmi kwa kuteua Kamati mbalimbali za Klabu hiyo na pia kusimamisha Wanachama 69 waliofungua Kesi Mahakamani.
Aveva alitinga madarakani Simba baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita Jijini Dar es Salaam kwa kuzoa Kura 1455 na kumshinda Andrew Tupa aliepata Kura 388.
Makamu wa Rais alichaguliwa Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliepata Kura 1046 na kuwabwaga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aliepata Kura 412, Swedi Nkwabi, Kura 373 na Bundala Kabula. 25.
Wajumbe wa Kamati Kuu waliochaguliwa kwenye Uchaguzi huo ni Idd Kajuna, Said Tully, Collins Frich, Ally Suru na Mwanamama Jasmine Badour.

Mbali ya Wajumbe hao, Rais Aveva, akitumia mamlaka yake Kikatiba, ameteua Watu watatu kuingia kwenye Kamati Kuu ambao ni Mohammed Nassor, Musleh Al Ruwaih na Salim Abdallah.
Kikao cha kwanza kabisa cha Kamati Kuu kiliamua kuwasimamisha Wanachama 69 ambao waliwasilisha Kesi Mahakamani kutaka kusimamisha Uchaguzi Mkuu na uamuzi wa hatima yao pamoja na ya Michael Wambura, aliezuiwa kugombea kwenye Uchaguzi, utatolewa na Mkutano Mkuu wa Simba utakaofanyika Agosti 3.



KAMATI ALIZOTEUA RAIS AVEVA:
KAMATI YA USAJILI

-Zacharia Hans Pope

- Mwenyekiti
-Kassim Dewji
-Dr Rodney Chiduo
-Musleh Al Ruwaih
-Crescentius Magori
-Said Tully

KAMATI YA VIJANA
-Said Tully - Mwenyekiti
-Ally Suru
-Patrick Rweyemamu
-Mulamu Nghambi
-Amina Poyo
-Madaraka Suleiman

KAMATI YA MASHINDANO

-Mohammed Nassor 

– Mwenyekiti
-Iddi Kajuna
-Jerry Yambi
-Hussein Simba

 -Mohammed Omar


 Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo. Pembeni ni Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli na Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli, Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi na Msimamizi wa shughuli hiyo Sam Odera.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha staili mbali mbali za kucheza mpira mbele ya waandishi wa habari.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana huku ukiwa unacheza mziki staili mbali mbali.
  Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana na kupita katika tundu dogo huku ukiendelea na mchezo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa leo anatarajiwa kuonyesha shoo ya bure ambapo ataonesha umahiri wa kucheza mpira wa mitaani, sarakasi na kucheza dansi.
Mfaransa huyo Sean Garnier ambaye yuko nchini kwa ziara maalum ya kimichezo jana usiku alianza ziara hiyo kwa kuonesha umahiri wake wa kucheza mpira wa mtaani katika viwanja vya ufukwe wa Coco (Coco Beach) jijini Dar es Salaam.
Garnier ambaye anakipaji cha kupiga danadana mpira huku akiweka mapozi mbalimbali alionekana kuwa kivutio mbele ya mkutano na waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo huku akionesha umahiri wake wa kupiga danadana na kucheza na mpira katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi baada ya mkutano huo.
Mwenyeji wa ziara ya Garnier, Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi alisema kwamba huyu ni mwanamichezo mwenye kushikilia taji la kipaji cha kucheza ‘Free Style’ duniani.
“Ameletwa kwa udhamini wa ‘Redbull Street Sytle’ na atakuwa nchini kwa siku tano ambapo ni kati ya Julai 2 hadi Julai 7 ataondoka.
Aidha mbali ya kumudu kucheza na mpira pia nacheza sarakasi katika mitindo mbalimbali huku akiwataka watanzania kuiga baadhi ya michezo ambayo ataionyesha akiwa atakapokuwa mtaani.
Baadhi ya mitaa atakayo pita ni Kariakoo, Mlimani City, Posta, Viwanja vua Sabasaba, Chuo Cha Biashara (CBE) na Sea Clif Jijini Dar es Salaam.

waliotembelea blog