Monday, September 21, 2015

 Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua mumewe Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kwenye  uchaguzi mkuu unaotarajiwa wa Oktoba 25 mwaka huu. Mara bada ya kuhutubia chumba chetu cha habari kilihemewa na simu za wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuelezea furaha yao sio tu kwa kumuona jukwaani bali pia kwa kuongea kwa kujiamini. Mama Magufuli amekuwa haonekani sana kwa sababu ya kuuguza mgonjwa nyumbani kwao Chato. Wamesema wametiwa moyo sana na haiba ya Mama Magufuli na wameshangazwa kwa uwezo wake mkubwa wa kuongea mbele za watu bila woga na bila kumung'unya maneno. Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu. Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano Wananchi wa Chato wakimshangilia Mama Magufuli kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato  mkoani Geita.
Vijimambo

Mgombea urais wa Tbanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za urais, ubunge na udiwani kwenye Uwanja wa Michezo mjini Chato, mkoani Geita, jimbo alilokuwa Mbunge. Pia alitumia fursa hiyo kuwaaga wapiga kura wake.Mkutano huo wa kampeni ulijaza watu kupita kiasi  jambo ambalo wenyeji wa wilaya hiyo pamoja na mgombea amesema haijawahi kutokea.PICHA ZOTE NA RICHARD BMWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mbuzi huyu aliyechorwa maandishi hayo aliletwa kwenye mkutano huo na mmoja wa wafuasi wa CCM kwa lengo la kuwakebehi Ukawa.
Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi wa Wilaya ya Chato ili wampigie kura nyingi yeye pamoja na mbunge na diwani wa CCM.
Dk Magufuli akiwahidi wananchi kuwa akipewa ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha  elimu ya bure inatolewa kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne Mke wa  Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Janeth Magufuli akipongezwa na mumewe, Dk Magufuli baada ya kutoka kumuombea kura 
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitumbuiza wakati wa mkutano huo
Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti
Baadhi ya wapigapicha za habari wakiwa juu ya magari kwa lengo la kupata picha nzuri wakati msafara wa Dk Magufuli ulipokuwa ukitokea nyumbani kwao kwenda kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Michezo mjini Chato leo
Dk Magufuli akiingia kwenye mkutano wa kampeni mjini Chato   Kikundi cha ngoma za asili cha Mchele Mchele kikitumbuiza katika mkutano huo
Wanamuziki wa Yamoto Band wakitumbuiza  wakati wa mkutano huo
Wafuasi wa CCM wakionesha dole gumba ikiwa ni ishara ya kumkubali Dk Magufuli kuwa rais
Msanii Khadija Kopa wa Kikundi cha Sanaa cha CCM cha TOT, AKITUMBUIZA KWA WIMBO WA TAARABU WAKATI WA KAMPENI HIZO
Wasanii wengine wakiendelea kuunga mkono Malkia wa Mipasho Khadija Kopa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Abdallah Bulembo akielezea wasifu wa Dk. Magufuli uliomfanya ateuliwe na CCM kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Tanzania.
Dk Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Josph Musukuma wakati wa kampeni hizo
Mwakilishi wa watu wenye ulemavu wana CCM na wasio wanaCCM, Amon Mpanju akihutubia kwa kuelezea ubaya wa Ukawa na kusifia CCM ambayo alidai inawajali walemavu nchini.



Nimepita kwenye page ya Facebook ya BBC Swahili nikakutana na hii stori ambayo nimeguswa kuishare hata hapa millardayo.com kuhusu nchi ya Ethiopia kuzindua Treni za umeme.
ET 3 
Ripoti inasema Treni hizi ambazo zimezinduliwa September 20 2015 zinaanza kubeba abiria na zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa watu kwenye mji mkuu wa Addis Ababa, Ethiopia nchi ambayo mpaka mwaka huu wanasema idadi ya watu wake ni zaidi ya MILIONI 90.
ET 2 
BBC wanasema hizi Treni zimetajwa kuwa mfano na za kwanza kusini mwa jangwa la sahara ambapo ujenzi na uendeshaji wa huduma hii ya reli unatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya China.



ET 4 

ETPicha zote ni kutoka BBC.
ET 6Treni hizi za umeme zitakua na uwezo wa kuhudumia Abiria elfu kumi na tano ndani ya dakika 60 ambapo Treni moja inaweza kubeba abiria 286 kwa wakati mmoja.
ET 5



Weekend iliyopita mtoto wa Diamond na Zari aitwaye Tiffah alitimiza siku 40 na sura yake kuonyeshwa LIVE kwa mashabiki wao..255 ikaamua kupiga stori na mama Diamond kujua anazungumzia nini kuhusu mjukuu wake kudaiwa si damu yake..amesema yale yalikuwa ni maneno ya Magazeti..anasema Mungu kawafedhehesha wote waliokuwa wakisema hivyo kwa kuwa mjukuu wake ni kopy ya Diomond kuanzia pua, mdomo macho na pia anatabia zote alizokuwa nazo Diamond.
T4
Sura ya mtoto wa Diamond na Zari
Diamond amesema kama mzazi lazima ajue jinsi ya kuwa mbunifu kwa kutumia kampuni kubwa kama ambavyo amefanya kwa mwanaye, anasema mtoto akiwa balozi wa kampuni yoyote inasaidia sana katika kupunguza gharama na hata kumsaidia katika maisha yake ya baadaye.
T2
Diamond akiwa amembeba Tiffah
Mahakama ya mwanzo ya Ilala leo imemwachia huru Mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha ambaye alikuwa na tuhumu za kesi ya kumbaka shemeji yake…amefunguka na kusema Mungu ni mwema ameshinda kesi, anamshukuru sana Mungu, anawashukuru Watanzania wote kwa kumuombea kwa kuwa alikua kwenye mapito magumu sana katika maisha yake.
Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.28 AM
Emannuel Mbasha

David Robert Joseph Beckham ni staa wa Soka ambaye kastaafu Soka na kuacha Rekodi kubwa na nzuri zinazoheshimika Duniani, yako maneno kwamba maji hufuata mkondo, mtoto wa Beckham na Soka la Baba yake je?
Stori ni vice versa, David Beckham kathibitIsha kwamba mtoto wake na Mchezo wa Mpira wa Miguu hata haviendani >>> “Mwanangu mmoja aliniambia kwamba haoni kama atakuja kuwa Mchezaji wa Mpira wa Miguu kwenye maisha yake, ilinivunja moyo kwa upande mwingine“- David Beckham.
BECKHAM_main_1473299a
Beckham akiwa na Familia yake kwenye matembezi yao.
Kwenye sentensi nyingine Beckham anasema mtoto wake ana hofu kwamba wapo watakaolinganisha kiwango chake na baba yake >>> “Kila nikiingia uwanjani najua watu wanasema ‘yule ni mtoto wa Beckham’, nisipokuwa na kiwango kizuri kama wewe hata haipendezi“- David Beckham.
David-and-his-sons
Story iko pia kwenye kipande cha video hapa mtu wangu.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imewawezesha vijana wajasiriamali wa kikundi cha MINARACO kutoka mkoani Mbeya wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki. Kikundi hicho kinaundwa na vijana 76 walioamua kuungana na kujihusisha katika ufugaji wa nyuki ili kujikwamua na changamoto za maisha. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa vya kinga ya nyuki 2, chupa za lita 1, 400, chupa za asali za lita 5, 200 na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki

Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema, “vitendea kazi waliopatiwa ni vyakisasa zaidi na vitasaidia kuboresha ufugaji huo na kuwawezesha vijana hao kupata mavuno zaidi ya waliokuwa wakipata awali”.
Akiongezea amesema, “mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali vifaa ni sehemu ya mpango wa kampuni ya Airtel wa kuwawezesha vijana ili kuboresha maisha yao na ya watu wanaowazunguka”.

“Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo”.

Wakipokea msaada huo wameishukuru, Airtel kwa kujitoa kwa kuwasaidia vijana katika kutatua changamoto zinazowakabili na kuahidi kutumia vifaa hivyo kwaajili ya kuongeza uzalishaji ili kufikia malengo waliojiwekea katika kikundi hicho.

“Hatukuamini kuwa Airtel itakuja kututembelea, kuangalia mahitaji yetu na hasa kwa kutupatia msaada wa vifaa vya kisasa walivyo tupatia leo, tunawashukuru sana na  tunaahidi kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha tunakuza na kuendeleza ufugaji bora wa nyuki” alisema mwakilishi wa kikundi hicho John Maige.

Akiongezea Maige  alisema, “Awali tulikuwa na changamoto ya uchache wa mizinga, vifungashio vya asali na soko la uhakika, lakini Airtel imetusaidia kwa kutupa mafunzo na vifaa vya kutosha vitakavyo tusaidia kupata Asali ya kutosha na  yenye ubora mzuri “.
Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akiwakabidhi wawakilishi wa kikundi cha MIRANACO mjini Mbeya vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya ufugaji wa nyuki. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa mizinga ya nyuki, mashine za kukamulia asali, vifaa vya kinga ya nyuki na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki. Wakishuhudia kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha FURSA Irine Paul akifuatiwa na Meneja mauzo wa Airtel mkoani Mbeya Saidi Zani
 Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akiongea na wawakilishi wa kikundi cha MIRANACO katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya ufugaji wa nyuki vikiwemo mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa vya kinga ya nyuki 2, chupa za lita 1 400, chupa za asali za lita 5, 200 na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki mjini Mbeya . Wakishuhudia kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha FURSA Irine Paul akifuatiwa na Meneja mauzo wa Airtel mkoani Mbeya Saidi Zani.


bazira.com
CHELSEA iliyokuwa inayumba katika Ligi Kuu England ambayo wao ni mabingwa watetezi, imeibuka na kuitwanga Arsenal kwa mabao 2-0.


Ushindi wa Chelsea huenda haukupewa nafasi kubwa kutokana na timu hiyo kuanza ligi kwa kusuasua, huku kocha wake, Jose Mourinho akionekana kutojielewa.

Lakini sasa imeibuka na kushinda dhidi ya Arsenal iliyoonekana kubadilika na angalau kuanza kushinda dhidi ya Chelsea baada ya ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya vigogo hao wa Stamford Bridge kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.

Ajabu, wakati Chelsea inaibuka na ushindi, juzi, haujawa gumzo, badala yake kila mmoja anazungumzia kuhusiana na mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa.

Kwamba raia huyo wa Hispania mwenye asili ya Brazil, alikuwa tatizo na alipaswa kupewa kadi nyekundu. Gumzo kwamba alisababisha beki Gabriel alambwe kadi nyekundu kwa kuwa aliparura shingoni, alimsukuma, pia alifanya ubabe kwa beki mwingine wa Arsenal, Laurent Koscielny.


Katika purukushani hizo, Costa aliambulia kadi ya njano lakini Kocha Arsene Wenger amesema mshambuliaji huyo alistahili kadi nyekundu kabisa, huku akiamini mwamuzi Mike Dean na wasaidizi wake hawakuwa makini sana ingawa alikataa zaidi kuzungumzia kuhusu waamuzi.

Kinachoweza kushangaza zaidi ni kwamba pamoja na kelele zote, Costa hakupatikana na faulo hata moja ukiachana na ile kadi. Hakuonekana kucheza madhambi au vinginevyo ingawa kweli purukushani zake ziliwavuruga kabisa Arsenal, wakashindwa kufikia malengo yao kiuchezaji.

Nani kasahau ‘footbal is a game of contact’. Mtacheza vipi soka bila ya kugusana, angalau kusukumana au kuangushana? Mourinho alitolea mfano wa mchezo wa ‘badminton’, kwamba watu hawagusani na soka haiko hivyo. Sawa na hapa ungeweza kutolewa mfano wa draft!

Utajiuliza hivi; hawa Arsenal walikuwa wanakutana kwa mara ya kwanza na Costa? Jibu, hapana, sasa vipi iwe ndiyo ishu wakati kuna kadi nyekundu nyingine ya Santi Cazorla ambayo iliwavuruga kabisa.



Arsenal ni timu yenye mashabiki walalamishi kuliko wote duniani. Kama siyo, sasa vipi wanalialia, kwani hawakujipanga? Au waliingia uwanjani wakiwa hawajui wamejipangaje kukabiliana na jogo feio?

Jina jogo feio kwa Lugha ya Kireno ni mchezaji mwenye mchezo wa vurugu, huo ni uchezaji wa Costa akiwa Hispania, jina ambalo linatambulika sana.

Kuna ‘game plan’, yaani mipango ya mchezo. Arsenal lazima walijua Costa ndiyo atakuwa tatizo na atatumika kuwachanganya mabeki. Sasa vipi walikubali kuchanganywa kweli na kutoa nafasi Mhispania huyo auchukue mchezo wote?

Costa ndiye aliyeipa Chelsea ushindi kwa kuwa ameonekana kuwa ‘profesheno’ zaidi ya wanavyomsema. Kwa sababu hizi tatu.


Moja:
Straika anatakiwa kuisaidia timu yake kupata ushindi kwa mambo matatu. Kufunga, kutoa pasi ya bao au kusaidia kuwavuruga mabeki wa timu pinzani.

Yeye amefanikiwa kuwavuruga mabeki na kikosi kizima cha Arsenal, amepunguza mtu baada ya beki kutolewa.

Mbili:
Amewatoa Arsenal mchezoni, wamepaniki na kushindwa kucheza walivyotakiwa au kama walivyoanza kipindi cha kwanza:

Tatu:
Wenger pia alionekana kuingia kwenye mtego wa Costa. Badala ya kuendeleza mipango, akatumia muda mwingi kulalamika dhidi ya jogo feio akimuacha Mourinho akiendeleza mipango ya kummaliza.

Sasa kwa Costa anataka nini zaidi? Kwa mashabiki na uongozi wa Chelsea anastahili pongezi kwa kazi nzuri.

Ukiangalia hakumuumiza mtu, lakini amevuruga mbinu za wapinzani. Pia amekuwa akicheza hivyo na mifano utaona alipozozana nusura azichape na Steven Gerrard pale Chelsea walipokutana na Liverpool, msimu uliopita.

Unakumbuka vita yake na beki Martin Skrtel wa Livepool au John O’shea wa Sunderland? Najua bado hujasahau vita yake na David Luiz wa PSG na vurugu nyingine kibao.

Siku moja Costa hatakuwa shujaa, kwa kuwa anaweza akakosea hesabu na kusababisha alambwe kadi nyekundu kwa kuwa kwa kipindi hiki waamuzi watamtupia jicho kwa karibu kukwepa lawama anazosukumiwa Dean na wasaidizi wake.

Ukweli ni kwamba sasa Costa ni shujaa wa Chelsea, hasa kwa mechi ya juzi na kama alivyosema Mourinho, kwamba alivyocheza Costa ilikuwa sahihi na ndiyo mipango hasa ya mchezo ilivyotakiwa iwe. Hivyo Arsenal, waache kulialia.



Beki kisiki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, baada ya kusikia tambo za straika wa Simba, Mganda, Hamisi Kiiza, amemjibu kwa kumwambia aache kuchonga sana kwani watakutana uwanjani Jumamosi.


Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Kiiza ameanza kwa kusema atahakikisha anaifunga Yanga kwenye mchezo huo.
CANNAVARO...

Cannavaro alisema anamheshimu Kiiza kutokana na uwezo wake, lakini atahakikisha anamzuia pindi watakapokutana katika mchezo wao.

 “Nimesikia Kiiza anasema kwamba atatufunga, hilo asahau kabisa kwani tunajipanga kuhakikisha hakuna straika yeyote wa Simba atakayeupita ukuta wetu tukikutana Jumamosi.

“Tumejipanga kwelikweli kwani tunataka kuivunja rekodi ya kutopata ushindi kila tunapokutana na Simba kwa siku za karibuni, sasa ni zamu yetu,” alisema beki huyo wa kati ambaye kwa muda mrefu amekuwa akicheza pacha na Kelvin Yondani.


Katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara hadi sasa, Yanga imeruhusu bao moja tu kuzitikisa nyavu zake.



Huku presha ikiwa ndiyo inazidi kupanda kuelekea mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga ambao utapigwa wikiendi hii, straika Mzimbabwe wa Yanga, Donald Ngoma, anaandaliwa mpango maalumu na wachezaji wa timu hiyo kwa ajili ya kuzitikisa nyavu za Simba.


Ngoma ambaye mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao matatu, kwa mara ya kwanza atakuwa anashiriki mchezo huo wa Simba na Yanga.

Mshambuliaji mwenye kasi wa timu hiyo, Simon Msuva, alisema kuwa kwa sasa wapo katika mazoezi maalumu ya kuhakikisha wanamng’arisha Ngoma katika mchezo huo kwa kumtengenezea nafasi nyingi za kufunga.

“Sisi kama washambuliaji tupo katika mpango maalumu wa kuhakikisha tunamfanya Ngoma aweze kuifunga Simba pale ambapo tutakutana katika mchezo wetu wa ligi kuu wikiendi hii.

“Mpango huo tumeuandaa na Tambwe ambapo itakuwa ni kuhakikisha tunapiga pasi za mwisho kwa Ngoma, kwani mabeki wa timu pinzani watakuwa wanatutolea macho sisi kutokana na kutujua kwa ukaribu.


“Lakini pia kama mchezo huo ikitokea penalti yoyote ile basi yeye (Ngoma) ndiye atakuwa mpigaji na sisi kukaa pembeni na hata kufunga kwetu itakuwa nadra, labda itokee nafasi ambayo itakuwa inaturuhusu kufanya hivyo,” alisema Msuva.


Anthony Martial Mechi yake ya kwanza tu ya Ligi Kuu England ambayo alianza tangu mwanzo, Amefunga Bao 2 wakati Manchester United inaicharaza Southampaton Bao 3-2 katika Mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu England huko Saint Mary.
Mechi yake ya kwanza kabisa ya Ligi kwa Martial, Kijana wa Kifaransa wa Miaka 19 tu, ilikuwa huko Old Trafford hapo Septemba 12 ambapo aliingizwa toka Benchi na kupachika Bao murua wakati Man United inaitandika Liverpool 3-1.
Hapo Jana, huku Man United wakiwa Bao 1-0 nyuma walipocheza na Southampton, Martial, akicheza Sentafowadi, huku Kepteni Wayne Rooney akiwa nyuma yake, ndie aliesawazisha Bao na kisha kupiga Bao la pili na Man United kwenda Bao 2-1 mbele.
Bao la 3 la Man United lilifungwa na Juan Mata wakati Bao zote za Southampton zikifungwa na Graziano Pelle.
Akimwongelea Martial, Mchezaji wa zamani wa Southampton, Morgan Schneiderlin, ambae Jana alirejea Saint Mary kuikabili Timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza, alisema: “Kama mlivyomwona, ni mtulivu, hana mchecheto. Ana kipaji kikubwa. Amekuja Ligi Kuu England na anafunga. Ni Mchezaji mwenye akili mno, alietulia. Atakuwa Mchezaji Bora mno kwa Man United!”
Nae Meneja wa Man United, Louis van Gaal, ameeleza: “Ni kweli ameanza vizuri lakini tatizo ana Miaka 19 tu na usitegemee kila Siku atacheza vyema lakini amecheza Mechi 3 mfululizo kwa kiwango cha juu na kufunga Mabao, na hilo ni muhimu!”
Jumatano Man United ipo Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup dhidi ya Ipswich Town na Jumamosi ijayo wapo tena Old Trafford kuivaa Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Huenda Mashabiki, ambao sasa wameanza kuwakebehi wapinzani walipochekwa kwa Bei mbaya aliyonunuliwa Martial, wakaendelea kujigamba.

waliotembelea blog