Friday, July 17, 2015


MABINGWA wa Italy Juventus wamesisitiza Kiungo wao Paul Pogba hauzwi licha ya Ofa kutoka Barcelona.
Joan Laporta, Rais wa zamani wa Barca ambae sasa anagombea tena nafasi hiyo, ameweka kwenye ajenda yake kuwa akichaguliwa Urais basi atamnunua Pogba.
Laporta yupo kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais pamoja na Rais wa sasa Josep Maria Bartomeu, August Benedito na Toni Freixa.
Pogba, Kijana wa Miaka 22 wa Kifaransa alietokea Man United kwenda Juve, pia anawindwa na Manchester City na Chelsea.
Mkurugenzi wa Juve, Giuseppe Marotta, amesema: "Yeyote anaemtaka Pogba anapaswa kuongea na sisi na si Wakala Mino Raiola. "

Aliongeza: "Tumezungumza na Barca katika Miezi ya hivi karibuni lakini hauzwi. "
Hata hivyo, hata kama Barca watamnunua Pogba ambae ana Mkataba hadi 2019, hawawezi kumtumia hadi Januari 2016 kutokana na kufungiwa na FIFA kwa kukiuka Kanuni za Usajili wa Wachezaji Chipukizi.
Licha ya Adhabu hiyo, Barca imeshasaini Wachezaji Wawili katika Kipindi hiki cha Uhamisho ambao ni Aleix Vidal kutoka Sevilla na Kiungo wa Uturuki anaetokea Klabu ya Atletico Madrid Arda Turan.



KOCHA wa timu ya APR ya Rwanda, Dusan Dule Suyagic amejigamba kuwa kikosi chake kitafanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua kesho jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya mazoezi na timu yake yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dusan alisema msimu uliopita timu yake ilishika nafasi ya pili baada ya kufungwa na El Merreikh ya Sudan hivyo msimu huu wamekuja wakijua kuna ushindani lakini nao watahakikisha wanatoa ushindani.
“Naheshimu kila timu iliyopo kwenye mashindano haya lakini naamini APR tutaonyesha ushindani kwani lengo letu ni kutwaa ubingwa wa CECAFA”, alisema Dusan.
APR itafungua dimba la mashindano ya Kagame ambayo yanashirikisha klabu toka nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa na Al Shandy ya Sudan kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa saa 8 kabla ya Yanga na Gor Mahia kuingia dimbani saa 10.00 kumaliza ubishi wa mashabiki kuwa nani mkali kati ya hizi timu kongwe Afrika Mashariki.


Mashindano ya CECAFA yanashirikisha vilabu 13 toka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo APR FC ipo kundi B pamoja na Al Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi na Hegaan FC ya Somalia.
Kundi A lina timu za Yanga na KMKM za Tanzania, Telecom ya Djibout, Gor-Mahia ya Kenya na Khartoum ya Sudan wakati kundi C lina timu za Azam ya Tanzania, Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.


Arsene Wenger amesema Arsenal wanalenga kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu unaoanza Agosti 8.
Msimu uliopita Arsenal walimaliza Nafasi ya 3 kwenye Ligi ambayo hawajawahi kutwaa Ubingwa tangu 2003/04 na tangu wakati huo walitoka kapa kila Msimu na kuonja Makombe Mwaka Jana kwa kutwaa FA CUP na kulitetea tena Mwaka huu.
Hadi sasa Arsenal imemsaini Mchezaji mmoja tu, Kipa Mkongwe kutoka Chelsea, Petr Cech, lakini Wenger ana imani kubwa na Kikosi chake.

Amenena: "Ubingwa ni lengo letu na tunaamini tuna nafasi ya kuleta changamoto. Hatuko mbali."
Wenger, alietua Arsenal Mwaka 1996, ameweza kuipa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 3 kwenye Misimu ya 1997/98, 2001/02 na 2003/04.
Kipa mpya wa Arsenal Petr CechArsene Wenger akiwaangalia Vijana wake kwenye mazoeziMtu kati!Cazorla wakati wa mapumziko



Kocha wa Mkuu wa Yanga, Hans Van Pluijm (kulia) akisisitiza jambo kwa kuinua kidole juu na kufanya ukumbi kuzizima kwa kicheko alipokuwa akiongea na wandishi wa habari juu ya mchezo wao dhidi ya Gor-Mahia utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni kocha mkuu wa Gor Mahia, Frank Nuttal na kushoto ni Katibu Mkuu wa Vyama vya Soka vya nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicholaus Musonye. (Picha na Rahel Pallangyo)

MAKOCHA wa timu za Yanga na Gor Mahia ya Kenya wametambiana kila mmoja kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya kombe la Kagame utakaochezwa kesho majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Taifa.
Kocha wa mkuu wa Yanga Hans Van Pluijm amesema anawaheshimu wapinzani wake timu ya Gor Mahia lakini haiogopi na ana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
“Nimefundisha soka Afrika tangu mwaka 1996 hivyo nina uzoefu na soka la timu za hapa kwa muda mrefu, lakini pia tumefanya maandalizi ya kutosha lakini mimi sidharau mpinzani wangu kwa sababu kwenye soka lolote linaweza kutokea na hakuna mtu anayejua matokeo”, amesema Pluijm.
Kocha mkuu wa Gor Mahia, Frank Nuttal amesema hana uzoefu mkubwa kwenye soka la Afrika ukilinganisha na mpinzani wake (Van Pluijm) lakini akasisitiza kuwa vijana wake wako vizuri kuikabili Yanga.
“Yanga ni timu kubwa japo sijawahi kuiona ikicheza lakini naamini ni timu yenye ushindani na mechi ya kesho itakuwa ngumu lakini mwisho wa mchezo tutajua matokeo”, amesema Nuttal.
Mchezo huu ambao mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Ujenzi, John Magufuli ambaye pia ni mteule wa kugombea kiti cha urais kupitia chama tawala (CCM) unatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake kutokana na timu zote kuwa na historia inayolingana kwenye mashindano haya kwani kila mmoja ametwaa kombe la Kagame mara tano.


Raheem sterling kwa furaha akiteta jambo na Wenzake alipofanya Mazoezi kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Klabu hiyo ya Manchester City huko Australia kwenye Ziara.Wachezaji wa City wakifanya mazoezi kujiandaa na Msimu mpya wa 2-15/2016Kwa Mara ya KwanzaYaya Toure nae alikuwemo kwenye mazoeziSterling katikati akifanya zoeziNi mazoezi kujiandaa na mechi za kirafiki katika kujiandaa na msimu mpya ujaoMazoezi ya nguvu



Fabian Delph akisaini mkataba kujiunga na Klabu ya  Manchester City

Delph amenunuliwa kwa kitita cha £8million 
Delph wakati anaenda kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na  Manchester City



Kocha wa Real Madrid ya Hispania Rafael Benitez alijikuta anapata wakati mgumu kujibu swali katika mkutano na wahandishi wa habari baada ya kuulizwa kama ana amini Cristiano Ronaldo ni mchezaji bora duniani?
Ni kama Benitez alizuga kutoa jibu la swali hilo na hakutaka kabisa kumtaja Ronaldo kama mchezaji bora zaidi duniani, nafasi ambayo angepewa kocha wa zamani Carlo Ancelotti isingekuwa ishu nzito sana kwake kutoa jibu.
Kocha huyo alimtaja Ronaldo kama mmoja ya wachezaji wenye viwango vya juu kama Bale na Benzema >>>> “Ni ngumu kusema nani ni mchezaji bora duniani, sababu kuna wachezaji wengi wa kiwango hicho kwa muda mrefu… nafikiri Ronaldo, Bale, Benzema na James ni wachezaji wenye viwango vya juu, na kumuweka Ronaldo miongoni mwa wachezaji bora inatosha” >>>Benitez



Klabu ya Bayern Munich imesafiri kwa muda wa masaa tisa kutoka Ujerumani hadi  China kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa Bundesliga, huo huwa ni utaratibu wa vilabu vingi duniani.

Kizuri zaidi kuhusu safari yao ni mapokezi walioyapata Beijing mtu wangu zilitumika dakika  30 tu kujaza  umati wa watu wasiopungua 1000 kuwapokea huku wakiombwa kusainiwa vitabu vyao vya kumbukumbu (autographs).

Watu ni wengi wanaohudhuria mazoezi yao, uwanja ukafurika kama kuna mechi. Mashabiki wamekuwa wakiomba kupiga picha na wachezaji, lakini pia wachezaji hawakuwa nyuma kuchukua kumbukumbu zao kwa kupiga picha kwa kutumia simu zao.
Wachezaji kama Philipp LahmManuel Neur na wengine wamekiri kitu kama hicho hutokea mara chache tu.
 

 

 

 

 


Hapa ninayo video pia, unaweza ukacheki love ambayo Bayern Munich waliipata wakiwa Beijing.


Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo. Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo.
Diego Costa ndani ya Uzi mpya
Mabingwa wa Ligi kuu England msimu uliopita 2014/2015 wakiwa na Msemo wao wa  'If it's not blue it will be,'
Kumeibuka ripoti ya Liverpool kuja juu kuipiku Manchester United kwa kukubali kutoa Pauni Milioni 32.5 kumnunua Straika wa Aston Villa Christian Benteke.
Liverpool walikuwa wakimsaka Straika huyo wa Belgium tangu Msimu uliopita kumalizika ingawa hawakuwa tayari kulipa zaidi ya Pauni 25 kumnunua lakini hali yao imebadilika ghafla baada ya kusikia Man United nao wana nia na Benteke.
Baada ya kumuuza Winga wao Raheem Sterling kwa Manchester City kwa Pauni Milioni 49, Liverpool sasa wanazo Fedha za ziada kumlipia Benteke mwenye Miaka 24.
Tayari Liverpool imeshanunua Wachezaji wengine 6 kwa ajili ya Msimu ujao ambao ni Nathaniel Clyne, Roberto Firmino, Danny Ings, Adam Bogdan, Joe Gomez na James Milner.



Timu zote zinazoshiriki michuano ya Kombe la Kagame zinatakiwa kufika mjini Dar es Salaam si zaidi ya leo tarehe 16 mwezi wa saba tayari kwa kuanza kipute jumamosi. Kwa hivyo bila shaka hii leo kufikia jioni vikosi vyote vya timu 13 vitakuwa vimefika nchini Tanzania. Timu zote zinatakiwa kujilipia gharama za usafiri huku mambo mengine yakifanywa na waandaaji.
Na kama ndiyo kwanza unasikia basi fahamu tu kuwa vilabu 13 kutoka ukanda wa Afrika masharik na kati vitakuwa vikichuana ili kuutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame ambalo linaenda sambamba na mgawanyo wa dola elfu 60 za kimarekani kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame. Tayari Timu ya wanamichezo wa BBC imeanza kuifuatilia michuano hiyo na tutakuletea mambo yote.

Promota wa Ngumi za Kulipwa, Shomari Kimbau (katikati) akiwa ameshika mkanda ambao utapiganiwa na bondia Abdallah Pazi (kushoto) na Iman Mapambano (kulia) kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni siku ya Idd pili katika uzito wa kilo 76 light heavy raundi 10. (Picha na Rahel Pallangyo)
BONDIA Abdallah Pazi anatarajiwa kupanda ulingoni Idd Pili kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni kuchuana na Iman Mapambao katika pambano la ubingwa wa Taifa lililoandaliwa na promota mkongwe Shomari Kimbau chini ya Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kimbau alisema Pazi atapambana na Mapambao katika uzito wa kilo 76 light heavy raundi 10 ambapo mshindi atapambana na Mkenya Daniel Wanyonyi katika pambano la Afrika Mashariki litakalofanyika mwezi ujao.
“Maandalizi yanakwenda vizuri, tunategemea pambano litakuwa la kuvutia kutokana na kuwaleta mabondia vijana wenye uwezo ambao watakuwa tegemeo baadaye katika mapambano ya kimataifa,”alisema.

waliotembelea blog