Akizungumza baada ya mchezo wa ushindi wa 1-0 wa Barcelona dhidi ya Malaga, Neymar alisema: ‘Ningependa na nataka kuendelea kubaki Barcelona, haijalishi ofa ya mamilioni mangapi ya paundi kutoka England,’ aliiambia TV3.
‘Watu wangu wa Barca wanaweza kutulia na kuwa na amani.
‘Pale ninaposikia tetesi za kuhama kwangu, huwa sifikirii chochote. Huwa nasikiliza kisha naendelea na shughuli zangu. Nina furaha sana kuwepo Barca na wachezaji wenzangu.’
Neymar, 23, anatarajia kuongezewa mkataba wa miaka 5 huku akiwa kipengele cha kuuzwa endapo timu inayomtaka italipa kiasi cha €250million (£182m).