Serikali imefuta hatimiliki ya
viwanja 15 vilivyokuwa vinavyomilikiwa na Raia wa Uingereza,
mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, Hermant Patel, Mwenye Uraia wa
Tanzania na Kenya kitendo ambacho ni kinyume cha taratibu na sheria za
nchi zinazozuia raia wa kigeni kumiliki ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi
William Lukuvi amesema anayeruhusiwa kumiliki ardhi nchini ni raia wa
Tanzania pekee na kuongeza kwamba kwa watanzania waishio nje ya nchi na
kuukana uraia wao nao hawataruhusiwa kumiliki ardhi bali watapewa ardhi
kama ilivyo kwa wawekezaji kutoka mataifa mengine.
William Lukuvi amesema mtu akishaukana
uraia wa Tanzania hana haki tena kama raia wa Tanzania, hivyo
ataruhusiwa kumiliki ardhi kama mwekezaji tu na siyo kama raia wa
Tanzania. Lukuvi amesisitiza kuwa ardhi itabaki kuwa ya Watanzania tu na
ameagiza mamlaka zota kuwasaka wale wote ambao wanamiliki ardhi kinyume
na sheria za nchi. Bonyeza Play kutazama video hii hapa chini