Wednesday, December 7, 2016


Serikali imefuta hatimiliki ya viwanja 15 vilivyokuwa vinavyomilikiwa na Raia wa Uingereza, mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, Hermant Patel, Mwenye Uraia wa Tanzania na Kenya kitendo ambacho ni kinyume cha taratibu na sheria za nchi zinazozuia raia wa kigeni kumiliki ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi amesema anayeruhusiwa kumiliki ardhi nchini ni raia wa Tanzania pekee na kuongeza kwamba kwa watanzania waishio nje ya nchi na kuukana uraia wao nao hawataruhusiwa kumiliki ardhi bali watapewa ardhi kama ilivyo kwa wawekezaji kutoka mataifa mengine.
William Lukuvi amesema mtu akishaukana uraia wa Tanzania hana haki tena kama raia wa Tanzania, hivyo ataruhusiwa kumiliki ardhi kama mwekezaji tu na siyo kama raia wa Tanzania. Lukuvi amesisitiza kuwa ardhi itabaki kuwa ya Watanzania tu na ameagiza mamlaka zota kuwasaka wale wote ambao wanamiliki ardhi kinyume na sheria za nchi. Bonyeza Play kutazama video hii hapa chini

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog