Saturday, April 26, 2014

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo ametunuku nishani na Tuzo kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa na watumishi wa umma wapatao 86 waliotoa mchango wao katika kuulinda na kuudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka Hamsini 50.
Mama Maria Nyerere akipokea nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Maria Nyerere Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungnao Daraja nne.

Mama Fatma Karume akipokea Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Abeid Aman Karume Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Fatma Karume nishani ya kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja Nne wakati wa hafla ya kutunuku nishani na tuzo za miaka 50 Muungano zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Mh.Benjamin William Mkapa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) wakati wa sherehe ya kutunuku nishani na tuzo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Kwanza Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia alikuwa Mwenyekiti Tume ya kurekebisha Katiba  Mhe. JajiJoseph Sinde Warioba wakati wa Sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana Picha zote na Freddy Maro

 Waziri Mkuu na Mgeni Rasmi wa Mkesha wa Muungano Mizengo Pinda akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuongoza mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye mkesha huo.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana na kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Iddi 
 Wageni waaliwa ikiwemo Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika za Kimataifa.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Mwansoko (katikati) akiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Joyce Fisoo (wa pili kushoto) na watumishi wengine wa Wizara hiyo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kujumuika katika Mkesha wa Muungano.Kulia kwake ni mwenyeji wake 
Kikindi cha Taifa cha Taarabu kikitumbuiza wananchi waliohudhuria kwenye mkesha na wimbo Maalum unaojulikana kama Muungano Wetu.  
 Kikundi cha Burudani kutoka Tanga kikuburudisha hadhira 
 Mzee Yusuf na Kundi lake la Jahaz Morden Taarabu.


 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akiwaaga baadhi ya wageni waalikwa na kuondoka baada ya kuongoza Mkesha wa Muungano.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Iddi, akitoa salamu zake kwa wananchi.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akitoa neno kwa wananchi.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akijiandaa kubofya kitufe cha kuashiria kuzaliwa upya kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 Maandishi Maalumu yakihamasishana kuashiria kutimia kwa Miaka 50 ya Muungano.
 Fashfash na fataki zikamiminika kwenye anga ya viwanja vya Mnazi Mmoja. 
 Profesa Mwansoko akizungumza na Televisheni One.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akiwaaga baadhi ya wageni waalikwa na kuondoka baada ya kuongoza Mkesha wa Muungano.



Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress akikaribishwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh siku ya Alhamisi April 24, 2014 alipotembelea Ubalozi huo na kujitambulisha kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula (hayupo pichani)
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress kwa Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi huyo alipotembelea Ubalozi huo siku ya Alhamisi April 24, 2014 jijini Washington, DC.
Mhe. Mark Childress akipokea zawadi toka kwa Balozi Liberata Mulamula.



Vijana wakiwa kwenye matembezi ya Uzalendo yalioratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM katika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ambapo vijana hao walianzia matembezi kutoka ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke mpaka kwenye viwanja vya sabasaba na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhani Madabida muda mchache kabla ya kupokea matembezi ya Uzalendo yaliofanywa na vijana mbali mbali .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshikilia picha ya  Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein akiwa ameshikilia picha ya  Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume baada ya kuzipokea kutoka kwa vijana waliofanya matembezi ya Uzalendo.


hqdefault_744f4.jpg
photo_f8ce8.jpg
Kocha wa zamani wa timu ya Barcelona Tito Vilanova amefariki dunia usiku huu akiwa hospitarini alipokuwa amerazwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani ya koo.(AWADH IBRAHIM)


0L7C0250 888b4

0L7C0297 5e5bb


Sherehe za kuhadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyozaa nchi ya Tanzania zimefanyika leo mjini Dar es Salaam na kupambwa kwa maonyesho mbali mbali ya kijeshi pamoja na halaiki zilizoandaliwa na watoto.
Marais wanne wa nchi za Afrika Afrika Mashariki akiwemo Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi ni miongoni mwa marais waliohudhuria sherehe hizo.
Wengine ni Rais Joyce Banda wa Malawi, Mfalme Mswati III wa Swaziland, mfalme Letsie III wa Lesoto Makamu wa Rais wa Nigeria Mohammed Sambo, Makamu wa Rais wa Zambia Guy Scott, Waziri Mkuu wa Rwanda Piere Habumurenyi, Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki.
Katika maadhimisho yao pia kulikuwa na maonyesho ya silaha mbali mbali za kivita zikiwemo ndege za kivita pamoja na za kiraia.
Hata hivyo kilichovutia  ni kikosi cha makomandoo wa jeshi la Tanzania ambao walionyesha umahiri wao kupambana na adui bila kutumia silaha na kuvunja vitu vigumu kwa kutumia kichwa  na mikono.
Onyesho jingine lililotia fora zaidi ni askari wa miamvuli ambao waliruka kutoka kwenye ndege umbali wa futi elfu arobaini  kutoka usawa wa bahari kwa kutumia miavuli na kutua katikati ya uwanja wa sherehe.


IMG-20140426-WA0034_af1cd.jpg
IMG-20140426-WA0035_686a4.jpg
Umati wa watu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea hivi sasa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, maonyesho haya yanajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo maonyesho. Maadhimisho haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoaka mataifa mbalimbali

waliotembelea blog