Sherehe za kuhadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyozaa nchi ya Tanzania zimefanyika leo mjini Dar es Salaam na kupambwa kwa maonyesho mbali mbali ya kijeshi pamoja na halaiki zilizoandaliwa na watoto.
Marais wanne wa nchi za Afrika Afrika Mashariki akiwemo Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi ni miongoni mwa marais waliohudhuria sherehe hizo.
Wengine ni Rais Joyce Banda wa Malawi, Mfalme Mswati III wa Swaziland, mfalme Letsie III wa Lesoto Makamu wa Rais wa Nigeria Mohammed Sambo, Makamu wa Rais wa Zambia Guy Scott, Waziri Mkuu wa Rwanda Piere Habumurenyi, Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki.
Katika maadhimisho yao pia kulikuwa na maonyesho ya silaha mbali mbali za kivita zikiwemo ndege za kivita pamoja na za kiraia.
Hata hivyo kilichovutia ni kikosi cha makomandoo wa jeshi la Tanzania ambao walionyesha umahiri wao kupambana na adui bila kutumia silaha na kuvunja vitu vigumu kwa kutumia kichwa na mikono.
Onyesho jingine lililotia fora zaidi ni askari wa miamvuli ambao waliruka kutoka kwenye ndege umbali wa futi elfu arobaini kutoka usawa wa bahari kwa kutumia miavuli na kutua katikati ya uwanja wa sherehe.
Umati wa watu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea hivi sasa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, maonyesho haya yanajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo maonyesho. Maadhimisho haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoaka mataifa mbalimbali
0 maoni:
Post a Comment