Baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu kuhusu uongozi wa klabu ya Real Madrid kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao January 4, umetangaza rasmi kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Rafael Benitez. Real Madrid walitangaza kumfuta kazi Benitez na Zidane kutajwa kurithi nafasi hiyo kwa muda hadi mwisho wa msimu.
Kufuatia kuteuliwa kwa Zidane kurithi mikoba hiyo, stori zilimfikia mchezaji mwenzake wa zamani David Beckham na
kuonesha furaha yake kwa kupost picha yao ya zamani na ujembe wenye
kuoneshwa kufurahishwa na nguli huyo wa kifaransa kuchukua mikoba hiyoo.
“Unaweza
kumpata mtu bora zaidi yake? mtu ambaye alikuwa bora kiwanjani na watu
wote tunampenda, anachukua nafasi ya kutumikia klabu ambayo mimi na watu
wengine tunaipenda, mtu mwenye passion na siku zote huwa hakubali
kushindwa kwa namna yoyote ile. Kiukweli ni mtu sahihi kwa hiyo kazi”
>>> Beckham
David Beckham na Zinedine Zidane waliwahi kucheza pamoja kwa miaka mitatu katika timu ya Real Madrid, baada ya David Beckham kuhama Man United na kuhamia Real Madrid mwaka 2003. Hata hvyo Jose Mourinho anatajwa kuhusishwa na Madrid kutaka kurudi mwishoni mwa msimu.