Tuesday, May 20, 2014


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini marehemu Arthur Mwakapugi huko nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana.Mwakapugi ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 64 alitumikia taifa kwa miaka 30 mfululizo katika nafasi mbalimbali.Marehemu baadaye alisafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake Ilundo wilaya ya Tukuyu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole na kuwafariji familia ya  aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini marehemu Arthur Mwakapugi huko nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana.Mwakapugi ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 64 alitumikia taifa kwa miaka 30 mfululizo katika nafasi mbalimbali.Marehemu baadaye alisafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake Ilundo wilaya ya Tukuyu.Picha na Freddy Maro-IKULU











Hivi ndivyo mamia ya wasanii wa filamu nchini walivyojitokeza kuuaga mwili wa mwigizaji mwenzao, marehemu Adam Kuambiana, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita. Mwili wa Kuambiana uliagwa kwenye viwanja vya Leaders, vilivyoko Kinondoni, Dar es Salaam. Serikali iliwakilishwa na Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni, Dk. Fenella Mukangara

Wanachama-Simba 

HEKAHEKA za uchaguzi wa klabu ya Simba zinaendelea kwa kasi na ifikapo juni 29 mwaka huu rais mpya, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji watapatikana tayari kwa safari nyingine ya miaka minne.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro jana aliweka hadharani majina 41 ya wagombea wa nafasi mbalimbali baada ya zoezi la uhakiki wa fomu kukamilika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hakuna jina lolote lililoenguliwa kwa sasa, lakini Ndumbaro alisema hayo ni majina ya awali na walichokuwa wanaangalia ni kama wagombea wamejaza fomu  vizuri na kuweka viambatanisho vyote.
Kwa wagombea wote walioomba kugombea nafasi zote zilizotangazwa walijaza vizuri fomu zao kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi.
Wakati Ndumbaro anataja majina hapo jana, nilishangaa kusikia maelezo yake kuwa kuna wanachama wa Simba wanamtaka awaache wagombea wote mpaka siku ya uchaguzi na wao ndio wataamua nani anafaa.

IMG_1150 
Na Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar es salaam
WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City fc bado ipo jijini Dar es salaam kujiandaa na safari ya kwenda Sudan kushiriki michuano mipya ya CECAFA Nile Basin inayotarajia kuanza mei 22 mpaka juni 4 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi ameuambia mtandao huu kuwa asubuhi hii wanaendelea na mazoezi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.
“Ninavyozungumza na wewe muda huu tupo hapa Karume. Tunaendelea vizuri na mazoezi yetu. Na mambo yakikaa sawa muda wowote tutaanza safari ya kwenda Sudan”. Alisema Mwalwisyi.

waliotembelea blog