Ikiwa imebakia siku moja kabla ya mchezo unaosubiri kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania kuuona, mchezo wa ngao ya Hisani kati ya Yanga na Azam FC, klabu ya Azam FC imethibitisha kuwakosa nyota wake kadhaa akiwemo Allan Wanga aliyekwenda Kenya wiki moja iliyopita kwa ajili ya msiba wa mama yake.
Lakini pia itamkosa mshambuliaji kutoka Ivory Coast Kipre Bolou ambaye pia ni majeruhi lakini taarifa zilizotoka siku ya Ijumaa August 21 ni kuwa klabu ya Azam FC imeamua kumpeleka nyota huo Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi, kupitia afisa habari wa klabu hiyo Jaffar Iddi Maganga, Bolou atakaa Afrika Kusini kwa wiki mbili.