Friday, February 3, 2017


MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND ULIVYO KWA SASA:
PosLogo &TeamPWDLGDPts
1ChelseaChelsea2318233256
2Tottenham HotspurTottenham Hotspur2313822947
3ArsenalArsenal2314542647
4LiverpoolLiverpool2313732446
5Manchester CityManchester City2314451946
6Manchester UnitedManchester United2311931242
7EvertonEverton2310761037
8West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion23968233
9Stoke CityStoke City23788-629
10BurnleyBurnley239212-829
11West Ham UnitedWest Ham United238411-1128
12SouthamptonSouthampton237610-527
13WatfordWatford237610-1227
14BournemouthBournemouth237511-926
15MiddlesbroughMiddlesbrough234910-721
16Leicester CityLeicester City235612-1421
17Swansea CitySwansea City236314-2421
18Crystal PalaceCrystal Palace235414-919
19Hull CityHull City234514-2717
20SunderlandSunderland234415-2216


EGYPT wametinga Fainali ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, nah ii ni mara yao ya 9 kufanya hilo na kuikuta Rekodi ya kucheza Fainali nyingi baada ya Jana huko
Stade de I'Amitie, Libreville Nchini Gabon kuibwaga Burkina Faso 4-3 kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano kufuatia Sare ya 1-1 katika Dakika 120.
Kipa Vterani wa Egypt, Essam El Hadary, mwenye Miaka 44, ndie alikuwa Shujaa kwa kuokoa Penati ya Bertrand Traore na kuwapa Egypt ushindi.

Katika Mechi hiyo, Egypt walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 65 la Mohamed Salah na Burkina Faso kusawazisha Dakika ya 72 kupitia Aristide Bance.
Kwenye Fainali, Egypt watapambana na Mshindi kati ya Ghana na Cameroon wanaopambana Leo huko Libreville, Gabon.
VIKOSI:
BURKINA FASO:
Koffi, Yago, Dayo, B. Koné, Y. Coulibaly, Kaboré, I. Touré, R. Traoré (Diawara 80'), B. Traoré, Bancé (A.Traore 102'), Nakoulma.

EGYPT:
El-Hadary, El Mohamady (Gaber 106'), Hegazy, Gabr, Fathy, Hamed, M. Salah, I. Salah, Said, Trezeguet (Sobhi 85'), Kahraba (Warda 76')

AFCON 2017

RATIBA
Robo Fainali
Jumamosi Januari 28

Burkina Faso 2 Tunisia 0 [RF 1]
Senegal 0 Cameroon 0 [Penati 4-5] [RF 2]

Jumapili Januari 29

Congo DR 1 Ghana 2 [RF 3]
Egypt 1 Morocco 0 [RF 4]
Nusu Fainali
Jumatano Februari 1
Burkina Faso 1 Egypt 1
Alhamisi Februari 2
2200 Cameroon v Ghana
Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4
2200 Burkina Faso v Aliefungwa NF 2
Fainali
Jumapili Februari 5

2200 Egypt v Mshindi NF 2

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1


2-1Stefan Savic is proving a problem at the back for Atletico MadridMabingwa Watetezi wa Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, Barcelona usiku  wameichapa Atletico Madrid Bao 2-1 huko Estadio Vicente Calderon Jijini Madrid katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali.
Timu hizi zitarudiana Wiki ijayo huko Nou Camp na Mshindi kucheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine kati ya Deportivo Alaves na Celta Vigo ambao Leo wanacheza Mechi yao ya Kwanza.

Atletico forward Antoine Griezmannheads to score a goalKwenye Mechi ya Jana, Luis Suarez ndie aliifungia Barca Bao la Kwanza katika Dakika ya 7 alipokokota Mpira toka Mstari wa Kati na kufunga kilaini.
Barcelona's Lionel Messi celebrates a goal with Luis Suarez
Dakika ya 33 mzinga wa Lionel Messi kutoka nje ya Boksi uligonga Posti na kutinga na kuwapa Barca Bao la Pili.
Dakika ya 59, Antoine Griezmann akaipa matumaini Atletico baada ya kufunga Bao pekee kwao.
Barcelona's Luis Suarez scores their first goalLA LIGA
Copa del Rey – Nusu Fainali
Jumatano Februari 1

Atletico Madrid 1 Barcelona 1

Alhamisi Februari 2

2300 Celta Vigo v Deportivo Alaves

Mechi za Pili
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Februari 7

2300 Barcelona v Atletico Madrid [2-1]

Jumatano Februari 8
2300 Deportivo Alaves v Celta Vigo
Ligi Kuu England imeendelea Jana kwa Mechi 3 na Manchester City kuibuka washindi wakubwa kwa kuicharaza West Ham 4-0 wakati Manchester United ikitoka 0-0 na Hull City na Stoke City na Everton kutoka 1-1.
Huko London Stadium Jijini London, Wenyeji West Ham walibandikwa Bao 4-0 na Man City kwa Bao za Kevin De Bruyne, David Silva, Gabriel Jesus na Yaya Toure.
Matokeo hayo yamewabakisha City Nafasi ya 5.
Huko Old Trafford, Kipa wa Hull City Eldin Jakupovic aliikosesha ushindi Man United kwa kuokoa Bao za wazi kadhaa na hasa michomo ya Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba.
Matokeo hayo yamewabakisha Man United Nafasi ya 5 ingawa hawajafungwa katika Mechi zao 14 zilizopita za Ligi lakini Sare hii ya 3 mfululizo ndio inawatafuna na kuwabakisha Nafasi hiyo ya 6 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 5 City na Liverpool zinazofungana kwa Pointi.

Huko Britannia Stadium, Wenyeji Stoke City na Everton zilitoka Sare 1-1 na Wafungaji walikuwa Peter Crouch kwa Stoke na Ryan Shawcross aliejifunga mwenyewe kuisawazishia Everton.

Kwa Crouch, hilo lilikuwa Bao lake la 100 la Ligi. 


EPL – Ligi Kuu England

RATIBA
Jumamosi Februari 4

1530 Chelsea v Arsenal
1800 Crystal Palace v Sunderland
1800 Everton v Bournemouth
1800 Hull City v Liverpool
1800 Southampton v West Ham United
1800 Watford v Burnley
1800 West Bromwich Albion v Stoke City
2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough

Jumapili Februari 5

1630 Manchester City v Swansea City

1900 Leicester City v Manchester United



Emmanuel Adebayor amejiunga na Timu ya Istanbul Basaksehir

waliotembelea blog