Friday, February 3, 2017


EGYPT wametinga Fainali ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, nah ii ni mara yao ya 9 kufanya hilo na kuikuta Rekodi ya kucheza Fainali nyingi baada ya Jana huko
Stade de I'Amitie, Libreville Nchini Gabon kuibwaga Burkina Faso 4-3 kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano kufuatia Sare ya 1-1 katika Dakika 120.
Kipa Vterani wa Egypt, Essam El Hadary, mwenye Miaka 44, ndie alikuwa Shujaa kwa kuokoa Penati ya Bertrand Traore na kuwapa Egypt ushindi.

Katika Mechi hiyo, Egypt walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 65 la Mohamed Salah na Burkina Faso kusawazisha Dakika ya 72 kupitia Aristide Bance.
Kwenye Fainali, Egypt watapambana na Mshindi kati ya Ghana na Cameroon wanaopambana Leo huko Libreville, Gabon.
VIKOSI:
BURKINA FASO:
Koffi, Yago, Dayo, B. Koné, Y. Coulibaly, Kaboré, I. Touré, R. Traoré (Diawara 80'), B. Traoré, Bancé (A.Traore 102'), Nakoulma.

EGYPT:
El-Hadary, El Mohamady (Gaber 106'), Hegazy, Gabr, Fathy, Hamed, M. Salah, I. Salah, Said, Trezeguet (Sobhi 85'), Kahraba (Warda 76')

AFCON 2017

RATIBA
Robo Fainali
Jumamosi Januari 28

Burkina Faso 2 Tunisia 0 [RF 1]
Senegal 0 Cameroon 0 [Penati 4-5] [RF 2]

Jumapili Januari 29

Congo DR 1 Ghana 2 [RF 3]
Egypt 1 Morocco 0 [RF 4]
Nusu Fainali
Jumatano Februari 1
Burkina Faso 1 Egypt 1
Alhamisi Februari 2
2200 Cameroon v Ghana
Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4
2200 Burkina Faso v Aliefungwa NF 2
Fainali
Jumapili Februari 5

2200 Egypt v Mshindi NF 2

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog