Tuesday, July 30, 2013


HOFU kubwa imetawala Kanisa Katoliki Parokia ya Uru iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, kutokana na matukio kadhaa yanayoendelea kutokea katika kanisa hilo huku baadhi ya watu wakiyahusisha na imani za kishirikina. 


  Katekista wa parokia hiyo, Lucian Tesha, aliwaambia waamini waliokusanyika katika ibada ya misa ya kwanza kanisani hapo juzi Jumapili kuwa usalama katika kanisa hilo upo shakani na kuwataka kuwa macho.
 

Hali hiyo inatokana na kile alichodai kuwa kuna mtu mmoja (mwanaume) kwamba amekuwa akionekana eneo la kanisa akiweka vitu mbalimbali ambavyo havina nia njema na kanisa hilo la Moyo Mtakatifu wa Yesu.
  
 “Mtu huyu ameonekana kanisani hapa kwa mara ya nne sasa, hatujui anataka nini, lakini amekuwa akiweka vitu mbalimbali katika sanamu ya Bikira Maria na karibu na sakristi ya mapadri…kwa kweli hali hii inatisha.

 "Ninawaomba tunapotoka kanisani hapa tuende kuangalia katika sanamu hiyo, kwani mtajionea vitu hivyo na wakati mwingine hata kadi za pikipiki,” alisema Tesha na kuacha waamini wakinong’ona. 


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kanisani hapo ni kuwa tangu paroko mpya aingie katika parokia hiyo, aliyefahamika kwa jina moja la Kiondo kumekuwa na matukio ambayo si mazuri.
 

“Tangu aingie hapa sanamu ya Mtoto Yesu imeibiwa na watu wasiofahamika… hatujakaa vizuri yanajitokeza haya mauzauza ya watu kuweka vitu visivyofahamika kanisani.
 
“Haifahamiki kama wanampima au la, lakini wengi wanajiuliza ni kwa nini matukio haya hayakuwapo siku zote? Alihoji muumini mmoja.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya makanisa kushambuliwa na hivyo kuwaweka roho juu waamini na mapadri wanapokuwa wakishiriki ibada takatifu

Monday, July 29, 2013


United wakishangiliaManchester United, leo wamemaliza Ziara yao ya huko Asia kwa kucheza Hong Kong na kuichapa Kitchee FC Bao 5-2. Bao za united zilianza kupatikana kipindi cha kwanza dakika ya kumi na sita kupitia mshambuliaji Welbeck Dakika, Fabia akazidi kuichangamkia timu yake kwa kuipachikia bao dakika ya 26, Januzaj kipindi cha pili muda mchache kabla ya mapumziko kisha na timu ya Kitchee kuipuka na mchezaji Lam akaifungia timu yake bao katika dakika ya 53, Alkande akaipachikia bao tena Kitchee dakika ya 69 huku Lingard kijana mtata na mwenye kujituma kwa juhudi zake akamaliza kipindi cha pili kwa kuifungia timu yake ya United bao dakika 80, Hadi Mapumziko, Man United walikuwa mbele kwa Bao 3-0.
Mechi inayofuata kwa Man United ni huko Stockholm, Sweden watacheza na AIK Fotboll hapo Agosti 6.Mashabiki huko Hong Kong wakiipamba Manchester United baada ya kufunga bao 3-0 kabla ya  mapunziko. United wakishangiliwa baada ya kuifunga timu ya Kitchee bao la pili Lam Ka Wai wa Hong Kong akipongezwa dakika ya 53 baada ya kuipatia timu yake bao na kufanya 3-1 kipindi cha pili.Mchezaji wa Kitchee Huang Yang akishindwa kumkaba Anderson wa Man United hapaSmalling akipiga mpira kwa kichwa hapaUwanja ulijaa matope na hapa Smalling kwenye patashika akizuia mchezaji wa Kitchee asipite na mpiraUwanja unavyooneka hapa kimatope matope zaidi!!Evra nae hakusita kuonesha mambo yake hapa mbele ya mchezaji wa Kitchee Tsang Kam KoSmalling akizungukwa hapa!David Moyes kulia akiwa kwenye benchi pamoja na viongozi wasaidiziFabio Da Silva akikimbiza hapa!!Tsang Kam hoi kwa Wilfried Zaha hapa!!Mapema mashabiki wa United walionekana kwa furaha hapa na walionesha furaha ya kushinda tangu mapema
VIKOSI:
Kitchee: Comi, Rodriguez, Rehman, Kei, Alkande, Belencoso, Wai, Annan, Yang, To.
Subs: Jianqiao, Wen, To, Fung, Quankun, Hau, Fai, Paramo, Lam, Deshuai, Lung
Goals: Lam (53), Alkande (69)
Manchester United: Amos, Evra (Buttner HT), Anderson, Smalling, Carrick (Jones 72), Young (Januzaj HT), Welbeck (Lingard HT), Fabio (Rafael 72), Cleverley, Zaha, Keane.
Subs:
Lindegaard, Rafael, Jones, Ferdinand, Giggs, Van Persie, Buttner, Lingard, Januzaj.Goals: Welbeck (16), Smalling (22), Fabio (26), Januzaj (47), Lingard (80)


 Licha ya Taifa Stars kushindwa kufuzu kucheza katika mashindano ya CHAN mwakani baada ya kufungwa na Uganda Cranes 3-1, wadhamini wa Stars, Kilimanjaro Premium Lager wamesema hawajakata tama nab ado wana imani na timu nzima na kocha Kim Poulsen.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya Stars kuwasili, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema licha ya habari hizi kutokuwa njema kwa watanzania, ni vizuri kukubali matokeo na kuangalia picha kubwa na malengo ya muda mrefu.

“Ni vyema tukumbuke kuwa kwenye mpira kuna kushinda na kushindwa,” alisema Bw Kavishe na kuongeza, “Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa sisi kama wadhamini hatujakata tama na bado tuna imani na timu hii na kocha Kim Poulsen kwa hivyo tunawaomba watanzania wasife moyo.”
Alisema wakati walipoanza kuidhamini Taifa Stars mwezi Mei mwaka jana na kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwaka, kwa muda wa miaka mitano, walikuwa na malengo kadhaa ikiwemo kuinua hadhi ya Timu ya Taifa, kuhakikisha wanaingia kambini kwa muda unaotakiwa, wanalipwa vizuri, wanakula na kulala vizuri na kusafiri vizuri.


“Tumejitahidi kufanya mambo haya kwani wachezaji sasa hivi wana DVD zenye maelezo yao, tumewapa suti mpya na za kisasa na pia tumewapa basi jipya la kisasa. Mambo haya yote pamoja na mambo wanayofundishwa na Mwalimu Kim Poulsen yamesaidia kuleta mabadiliko kwa timu ya Taifa,” alisema. 

Alisema kuna mafanikio mazuri ya timu ya taifa ambayo watanzania lazima wayakumbuke kama kuzifunga timu kama Zambia, Cameroon, Morocco na Kenya .

Kwa mujibu wa Meneja huyo walipoanza udhamini Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 145 kwa mujibu wa FIFA lakini sasa imesogea hadi 109. “Haya ni mafanikio makubwa kwani tumesogea hatua zaidi ya 40,” alisema.

Alisema safari ya mafanikio katika mpira ni ndefu na inahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kuongeza kuwa Kocha Kim Poulsen anafanya kazi nzuri ya kuibua vijana.


“Kocha anahitaji kuungwa mkono na sisi sote kuanzia kwa TFF, sisi wadhamini na watanzania wote. Tunahitaji kuangalia picha kubwa,” alisema na kuongeza,”Nawaomba watanzania tuwe wazalendo wakati huu hii ni timu yetu na tunatakiwa kujivunia. Vyombo vya habari pia viwe mstari wa mbele kuonesha uzalendo.”

Alisema mechi dhidi ya Gambia itakayochezwa mwezi wa 9 ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia ni muhimu hata kama Tanzania haisongi mbele kwani itasaidia katika ngazi za FIFA.
William O. Rutta (kulia) akiwa na Shabiki wa Taifa StarsChinja shingo!!
Matajiri wapya katika soko la usajili barani ulaya klabu ya AS Monaco imesema kwamba walipewa ofa ya kumnunua winga wa klabu ya Manchester United Nani. Winga huyo wa timu ya taifa ya Ureno amekuwa njia panda kujua hatma yake ndani ya Old Trafford kabla ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mpaka sasa chini ya manager mpya David Moyes. 

Billionea anayemiliki klabu ya Monaco - Vadim Vasilyev amekiri kwamba United walimpa ofa ya kumsajili  Nani.
Alisema: “Nani tulipewa ofa kumnunua. Ni mchezaji mzuri, lakini hakujawahi kuwa na mazungumo mpaka sasa.”
Monaco wamekuwa na vurugu sana kwenye soko la usajili hivi karibuni, wakiwasajili wachezaji kama Falcao, James Rodriguez  Joao Moutinho kwa bei mbaya sana.



Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni.

Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera

Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba

Rais Kikwete akisalimiana na mama wa Profesa Anna Tibaijuka

Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka akishiriki katika ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete wilayani Muleba

Rais Kikwete akiongea na viongozi wa wilaya ya Muleba baada ya kupokea taarifa ya maendeleo, akiwa na mawaziri watano anaoongozana nao katika ziara hiyo

Mbunge wa Muleba akitoa maoni na kero za jimbo lake

Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiwahakikishia viongozi wa Muleba juu ya mipango ya serikali kuleta meli za abiria mpya mbili katika ziwa Victoria

Rais Kikwete akipata maelezo ya mpango kabambe wa maji wilaya ya Muleba

Rais Kikwete akizindua mradi mkubwa wa maji wilayani Muleba

Ngoma ya utamaduni ikimlaki Rais Kikwete alipowasili katika mkutano wa hadhara

Rais Kikwete akisalimia wananchi

Rais Kikwete akiangalia mazao yatokanayo na uzalishaji mbegu ya kampuni ya Itente ya Muleba

Rais Kikwete akipozi na wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji mbegu ya Itente

Rais Kikwete akifurahia ngoma

Umati wa wananchi Muleba ukimsikiliza Rais Kikwete

Rais Kikwete akiongea na wananchi wa Muleba

Rais Kikwete akihutubia wana Muleba

Sehemu ya umati mkutanoni

Rais Kikwete akiendelea kungea na wananchi

Umati katika mkutano wa hadhara

Umati katika mkutano wa hadhara

Rais Kikwete akijiunga na waumini wa Muleba kusali swala ya Magharibi kabla ya kufuturu

Dua ikisomwa baada ya futari aliyoandaa Rais Kikwete kwa wananchi wa Muleba

Dua ikiombwa baada ya futari

Dua

Wananchi wa Muleba katika futari aliyoandaa Rais Kikwete wilayani Muleba

waliotembelea blog