Friday, October 23, 2015

MECHI 10 ZA MWISHO ZA MAN U VS MAN CITY
United 3-2 City - 7 August 2011
United 1-6 City - 23 October 2011
United 3-2 City - 8 January 2012
City 1-0 United - 30 April 2012
City 2-3 United - 9 December 2012
United 1-2 City - 8 April 2013
City 4-1 United - 22 September 2013
United 0-3 City - 25 March 2014
City 1-0 United - 2 November 2014
United 4-2 City -  12 April 2015


MECHI YA LIGI KUU ENGLAND KATI YA WATANI MAN UNITED WATAKAOKUWA NYUMBANI DHIDI YA MAN CITY KESHO JUMAPILI INASUBIRIWA KWA HAMU SANA. TAKWIMU ZA MSINGI, HIZI HAPA, SOMA KWA RAHA ZAKO....





Na Saleh Ally
KAMA ni Mwanaliverpool lazima utakuwa unajua hadithi za wachezaji kama Phil Thomson, Graeme Souness, Alan Hansen ambao waliifanya Liverpool kuanza kusimama katika miaka ya 1930 na baadaye miaka ya 1970 na 1980.


Miaka hiyo ya 1980 kwenda 1990 wachezaji kama akina Ronnie Whelan, Mark Wright halafu kikaja kizazi cha akina Ian Rush, John Barnes na kumaliziwa na akina Paul Ince, Sammy Hyypia, Jamie Redknapp.

Najua watu wengi wa kizazi cha sasa wanamjua zaidi Steven Gerrard, Jammie Carragher ambao walikuwa katika kizazi cha mwisho kilichoiwezesha Liverpool kubeba Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiimaliza AC Milan katika mechi ya kihstoria mwaka 2005 jijini Istanbul, Uturuki.

Katika mechi hiyo, hadi mapumziko, Liverpool ilikuwa imetulizwa mabao 3-0. AC Milan waliona wamemaliza kazi, lakini mpaka dakika ya mwisho, wakatoka vichwa chini.

Tangu mwaka 2005, baada ya Rafa Benitez kuondoka Liverpool imeajiri makocha wanne na inaonekana imeshindwa kabisa kurejea katika ukubwa wake inaoutaka.



Julai Mosi 2010 ilimuajiri Roy Hogdson, ikamtimua Januari 2, 2011, hata mwaka haukutimia. Ikamwajiri Kenny Dalglish siku hiyohiyo.

Dalglish ambaye ni gwiji wa Liverpool alikaa hadi Mei 16, 2012. Tena ilionekana walimvumilia sana kwa kuwa ni mkongwe wao. Hivyo, akakaa mwaka mmoja na miezi kadhaa. Nafasi yake ikachukuliwa na Brendan Rodgers.

Juni Mosi 2012 ndiyo Rodgers alitua, Oktoba 4, mwaka huu, naye kafungashiwa virago. Angalau amekaa miaka mitatu lakini naye ameondoka mikono mitupu!

Kombe la mwisho la Liverpool ni lile walilotwaa msimu wa 2011/12 chini ya Dalglish baada ya hapo, hata ngao tu imekuwa hadithi na kumbukumbu kubwa zaidi hasa ukitaka kuzungumzia ya karibu ni mwaka 2005 wakati Liverpool ikiwa chini ya Benitez ilipotwaa Kombe la FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya pia Uefa Super Cup.

Hii ni Liverpool ya ndoto za mchana! Sasa imemwajiri Kocha Mjerumani, Jurge Klopp ambaye mafanikio yake yanajulikana akiwa na timu ya Borussia Dortmund.

Klopp anauweza mzigo huu wa Mnyamwezi? Tayari ameiongoza katika mechi mbili. Moja ya Ligi Kuu England, sare ya 1-1 dhidi ya Tottenham, pia sare kama hiyo katika Europa League dhidi ya Rubin Kazan.

Mara ya mwisho Liverpool ilipopata nafasi ya kusema ni wagombea ubingwa ni msimu wa juzi waliposhika nafasi ya pili, tena waliokosa ubingwa kidogo wakati huo wakionekana kutegemea zaidi nguvu ya juhudi za Luis Suarez. Msimu uliofuata, kaondoka kwenda Barcelona, msimu huu Liverpool inaonekana taabani!

Klopp kweli ataweza kubadilisha kila kitu kama ambavyo karibu kila shabiki wa Liverpool wa England, Tanzania na duniani kote anavyosubiri kwa hamu?

Jibu hapana, Klopp hawezi kubadili kila kitu ndani ya Liverpool ambayo inaonekana wazi kwamba ina matatizo mengi. Sawa na kusema kumleta mziba pancha aongeze kasi ya gari ambalo linaonekana kutokuwa na nguvu.

Mziba pancha hawezi kuongeza kasi ya gari, ataziba pancha na kasi itabaki ileile. Kwa kuangalia kawaida tu unaona Liverpool bado haina wachezaji wa kiwango cha kuiinua kutoka ilipo na kufikia kiwango cha kuwa washindania ubingwa wa England au kurudi ndani ya Top Four.

Ukubwa wa Liverpool umebaki jina, lakini ukweli kama atajitokeza mwekezaji na hasa wale wa kiarabu kama tulivyoona Manchester City na Sheikh Mansour bin Zayed bin Sultan au PSG na Nasser Al-Khelaifi, mchezaji tenisi wa zamani wa kimataifa wa Qatar kunaweza kuwa na mabadiliko makubwa.

Kumekuwa na ambao wapo tayari kuinunua na kuwekeza lakini Liverpool wenyewe hawataki hasa kwa wageni na wanaotokea nje ya Ulaya. Kama hivyo, basi wakubali Warusi mamilionea ambao watakuwa tayari kumwaga fedha zao na kuirekebisha.

Matajiri wa mafuta wanaonekana kuwa tayari kumwaga fedha zao kama ilivyo kwa Roman Abramovich kutoka Urusi ambaye ameigeuza Chelsea kuwa timu kubwa wakati haikuwa na umaarufu wa hivyo miaka 10 iliyopita.

Liverpool watakubali mwekezaji awe Sheikh, kutoka Urusi au bilionea mwingine ambaye atakuwa tayari kuwekeza na kununua wachezaji ghali na bora? Kama hawataki, basi watabaki hivi, Klopp atasaidia nafuu, lakini si kumponyesha mgonjwa.


 Meneja  wa Mawasiliano  Efm, Denis Ssebo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kumpata mshindi wa  shindano la kubuni maneno ya Kanga kupitia kipindi cha UHONDO ambacho huruka hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa alasiri, kikiwa na Matangazaji mahiri Dina Marios, kikao hicho kimefanika leo jijini Dar es Salaam, katikati ni mshindi wa shindano hilo Sekela Richard na wakulia ni Matangazaji wa Efm  Radio Dina Marios.
 Matangazaji mahiri Dina Marios, akimkabidhi kitita cha shilingi Kitanzania milioni moja. mshindi wa shindano hilo, Sekela Richard kulia ni Meneja  wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja  wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo
Picha na Emmanue Massaka.

MENEJA  wa Mawasiliano  Efm, Denis Ssebo  shindano hilo halitaishia hapo, kwani baada ya kupata mshindi neno lake la Ushindi  zitatengenezwa  kanga zitakazoandikwa neno hilo ikiwa ni hatua ya pili sasa ya kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi.

Zikishatengenezwa kanga hizo, Efm kupitia kipindi hicho cha Uhondo, itatatoa nafasi kwa  wanawake kutengeneza pesa na kujikwamua kwa kuuza Kanga hizo na  Mwanamke yoyote hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani atachukua kanga hizo na kuziuza ambapo kwa kila doti moja ya kanga atapata asilimia 30% ya pesa.


BAADA ya kuzichapa Man United, Watford na Bayern Munich, Jumamosi Arsenal wana nafasi ya kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza katika Miaka Miwili ikiwa wataifunga Evrton Uwanjani Emirates.
Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii, Arsenal iliifunga Everton 2-0 na safari hii Arsenal wapo kwenye wimbi zuri la ushindi wakitoka kuzichapa 3-0 Man United na Watford kwenye Ligi na 2-0 Bayern Munich kwenye UEFA CHAMPIONS.
Everton wao wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kwenye kipigo cha 3-0 Nyumbani kwao Goodison Park kutoka kwa Man United.

Ikiwa Arsenal wataifunga Everton basi watakaa kileleni mwa Ligi pengine hadi Jumapili wakati Dabi ya Manchester ikichezwa huko Old Trafford kati ya Man United na Man City ambao wana nafasi ya kuishusha Arsenal toka kileleni.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Oktoba 24

17:00 Aston Villa v Swansea
17:00 Leicester v Crystal Palace
17:00 Norwich v West Brom
17:00 Stoke v Watford
17:00 West Ham v Chelsea
19:30 Arsenal v Everton

Jumapili Oktoba 25
15:00 Sunderland v Newcastle
17:05 Bournemouth v Tottenham
17:05 Man United v Man City 

19:15 Liverpool v SouthamptonSmalling akishangilia bao lake kwenye mchezo uliowakutanisha City na Man 



JUMAPILI ya Oktoba 25, 2015, Tanzania inafanya Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge pamoja na kumpata Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uchaguzi ni nini? Zipo tafsiri mbalimbali lakini mojawapo na iliyo wazi ni kwamba, hii ni njia ya kidemokrasia inayotumiwa na watu katika kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba au utaratibu waliojiwekea wenyewe.
Huu ni Uchaguzi Mkuu wa Tano kufanyika tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza tena mwaka 1992, lakini ni wa 11 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964.
Uchaguzi wa mwaka huu una umuhimu wa kipekee kwa sababu kadha wa kadha, mojawapo ikiwa umri wa miaka 23 tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza.
Huu ni umri mkubwa, na kwa hakika vijana wengi waliojitokeza kujiandikisha safari hii ni wenye umri wa kati ya miaka 18-35, ikimaanisha kwamba wengi wao walizaliwa kuanzia mwaka 1992. Hawa wanatengeneza asilimia 57 ya wapigakura wote.
Umuhimu mwingine ni kwamba, kulinganisha na uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, safari hii demokrasia imekua na kupanuka kiasi cha kushuhudia wapigakura 22.75 milioni, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini tangu tupate Uhuru.
Kwa upande mwingine, hamasa imeongezeka, upinzani umeimarika zaidi na uhuru wa habari umepanuka ukiwamo ukuaji wa sekta ya habari na mawasiliano, hususan mitandao ya kijamii.
Haya yote yanatokea kutokana na kuwapo kwa amani na utulivu, sifa ambazo zimeendelea kuitambulisha vyema Tanzania hata katika jumuiya za kimataifa.
Uchaguzi Mkuu ni gharama kubwa kifedha, rasilimali watu na muda, na kama mambo yatakwenda mrama maana yake nchi itakuwa imeingia hasara kwa kupoteza fedha, lakini pia itaingia kwenye machafuko ambayo yatatowesha amani iliyodumu kwa miaka mingi.


REFA Mark Clattenburg ndie atasimamia Dabi ya Jiji la Manchester Jumapili Oktoba 25 Uwanjani Old Trafford wakati Manchester United wakiwavaa Manchester City.
Clattenburg, mwenye Miaka 40, ndie aliesimamia Dabi iliyopita Uwanjani Old Trafford wakati Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal, ilipoinyuka City Bao 4-2 Mwezi Aprili kwa Bao za Ashley Young, Marouane Fellaini, Juan Mata na Chris Smalling

Msimu huu, Clattenburg ameshachezesha Mechi 2 za City, ambazo waliifunga Watford na nyingine kufungwa na Tottenham, na Mechi 1 ya Man United waliyoifunga Southampton 3-2.
Kwa Msimu huu, Refa huyo ameshachezesha Gemu 11 na kutoa Kadi za Njano 11 na Kadi Nyekundu 2.


WIKIENDI hii Ligi Kuu England ina Mechi kali ikiwamo Dabi ya Jiji la La Manchester wakati Manchester United wakiwa Nyumbani Old Trafford kuikaribisha Manchester Cityhapo Jumapili.
Lakini Jumamosi, Arsenal, ambao wako Nafasi ya Pili kwenye Ligi Kuu England wakiwa na Pointi 19 sawa na Man United na Pointi 2 nyuma ya Vinara Man City, wana nafasi ya kutwaa uongozi ikiwa watashinda Nyumbani kwao Emirates wakicheza na Everton.
Timu zote hizi za kileleni, City, Arsenal na Man United, zimetoka kwenye Mechi za Kati-Wiki za UEFA CHAMPIONS LIGI za Makundi yao.
Akiongelea Dabi yao, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema ushindi dhidi ya City ni muhimu ili kusisitiza azma yao ya kuwemo kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa Msimu huu.
Nao Arsenal wanatoka kwenye wimbi zuri la ushindi baada ya kuzichapa Man United na Watford 3-0 kila mmoja kwenye Mechi za Ligi na kisha Juzi kuifunga Bayern Munich 2-0 kwenye Mechi yao ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.
Ikiwa Arsenal wataifunga Everton watakaa kileleni mwa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza kwa karibu Miaka Miwili na kubakia hapo hadi Jumapili ambapo Dabi ya Manchester itaamua kama watabaki huko juu au wataporomoshwa.


Dakika ya 37 Emre Can aliwasawazishia bao Liverpool kwa kufanya 1-1 na mtanange kwenda mapumziko wakiwa sare, Kipindi cha pili pamoja na Timu ya Rubin Kazin kucheza kwa pengo la mchezaji mmoja aliyetolewa  kwa kadi nyekundu, Liverpool hawakuweza kuifunga timu hiyo na hatimaye waliweza kusawazisha tu na mtanange kumalizika kwa dakika 90 kwa nguvu sawa ya bao 1-1.Marko Devic akipongezwa na wenzie baada ya kuwafungulia bao kwa kufanya 1-0 dhidi ya Liverpool.Marko Devic akimnyamazisha Kocha wa Liverpool Klopp
VIKOSI:
Liverpool XI:
Mignolet, Clyne, Skrtel, Sakho, Moreno, Can, Allen, Milner, Lallana, Coutinho, Origi
Akiba: Bogdan, Toure, Benteke, Firmino, Lucas, Ibe, Randall
Rubin Kazan XI: Ryzhikov; Kuzmin, Nabiullin, Kverkvelia, Kambolov, Carlos Eduardo, Ozdoev, Karadeniz, Georgiev, Devic, Kanunnikov
Akiba: Lemos, Portnyagin, Haghighi, Bilyaletdinov, Cotugno, Dyadyun, Akhmetov


www.bukobasports.com
LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Alhamisi Oktoba 22

JKT Ruvu   0 v Mtibwa Sugar 0
Mwadui FC 3 v Mgambo JKT 1
Mbeya City 1 v African Sports 0
Ndanda FC  0 v Azam FC 1

VPL, Ligi Kuu Vodacom, imeendelea tena Leo kwa Mechi 4 na 

Azam FC wameikamata Yanga kileleni kwa Pointi baada ya kuifunga Ndanda FC Bao 1-0.
Bao pekee la Azam FC lilifungwa Dakika ya 70 na Shomari Kapombe kwenye Mechi iliyochezwa huko Nangwanda Mtwara.
Ushindi huu umewafanya Azam FC wafikishe Pointi 19 sawa na Vinara Yanga lakini wao wanakaa Nafasi ya Pili kwa vile Yanga wana Goli nyingi.
Huko Mwadui, Shinyanga, Wenyeji Mwadui FC wameichapa Mgambo Shooting Bao 3-1 kwa Bao 2 za Jerry Tegete na Jamal Mnyate huku Abuu Daudi akiwapa Mgambo Bao lao pekee.

Kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, JKT Ruvu ilitoka 0-0 na Mtibwa Sugar wakati huko Sokoine, Mbeya, Bao la Geofrey Mlawa limewapa Mbeya City ushindi wa Bao 1-0.

LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Jumatano Oktoba 21

Yanga 4 v Toto Africans 1
Stand United 3 v Majimaji 0
Tanzania Prisons 1v  Simba 0
Coastal Union 1 v Kagera Sugar 0

waliotembelea blog