Tuesday, July 22, 2014


Na Boniface Wambura, Dar es salaam



Kikosi cha Taifa Stars kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Mbeya ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji. 
Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini Julai 31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto.
Wakati huo huo, mechi ya michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh. 158,350,000 kutokana na washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000. 
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama za mchezo sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 74,432,095.

Tunawashukuru washabiki wote waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.


CECAFA KAGAME CUP 2014
9TH – 25TH AUGUST 2014 – RWANDA
FIXTURE
GROUP A                                             GROUP B                                                             GROUP C
RAYON FC (RWA)                             APR (RWA)                                                         VITAL ‘O’ (BRD)
YOUNG AFRICANS (TZ)                  KCCA (UG)                                                          EL MEREIKH (SUD)
COFFEE (ETH)                                     FLAMBEAU DE L’EST (BRD)                           POLICE (RW)
ATLABARA (S.SUD)                        TELECOM (DJB)                                                   BANADIR (SOM)
KMKM (ZNZ)                                    GOR MAHIA (KEN)                                                                     
Method of qualification (Group A1, 2, 3, Group B 1, 2, 3 Group C 1, 2 qualifies to quarter finals
DATE
NO.
TEAMS
GROUP
VENUE
TIME (TBD)
Fri. 8th Aug
1
AtlabaraVs KMKM
A
 NYAMIRAMBO
2
Rayon VsYanga
A
AMAHORO
3
GorMahiaVs KCCA
B
AMAHORO
Sat. 9th Aug
4
Vital ‘O’ VsBanadir
C
AMAHORO
5
Police Vs El Mereikh
C
AMAHORO
6
APR Vs Flambeau
B
AMAHORO
Sun. 10th Aug
7
KMKM Vs Young
A
AMAHORO
8
Telecom Vs KCCA
B
NYAMIRAMBO
9
Coffee Vs Rayon
A
AMAHORO
Mon . 11th Aug
10
BanadirVs El Mareikh
C
NYAMIRAMBO
11
GorMahiaVs Flambeau
B
‘’
12
Vital ’O’ Vs Police
C
‘’
Tue. 12th  Aug
13
KMKM Vs Coffee
A
‘’
14
YangaVsAtlabara
A
‘’
Wed. 13th Aug
15
APR  Vs Telecom
B
‘’
16
KCCAVs Flambeau
B
‘’
Thur. 14th Aug
17
Coffee VsAtlabara
A
18
Rayon  Vs KMKM
A
19
Police VsBanadir
C
Fri 15th Aug
20
Flambeau Vs Telecom
B
21
APR VsGormahia
B
22
El MareikhVs Vital ‘O’
C
Sat 16th Aug
23
Coffee VsYanga
A
24
Rayon VsAtlabara
A
Sun 17th Aug.
25
Telecom VsGormahia
B
26
KCC Vs APR
B
Mon 18th Aug
REST DAY
Tue. 19th Aug
QUARTER FINALS
27
C1 Vs B3
NYAMIRAMBO
28
A1 Vs B2
‘’
Wed 20th  Aug
29
A2 Vs C2
‘’
30
B1 Vs A3
‘’
Thu 21st  Aug
REST DAY
Fri. 22nd Aug
SEMI FINALS
31
32
Winner 27 Vs Winner 28
Winner 29 Vs Winner 30
AMAHORO
Sat. 23rd Aug
REST DAY
Sun. 24th Aug
3rd Place playoff  & Finals
33
34
Loser 31 Vs Loser 32
Winner 31 Vs Winner 32
AMAHORO
(NOTE: KICK OFF TIMES TO BE DECIDED BETWEEN CECAFA,FERWAFA AND SUPERSPORT BECAUSE OF LIVE TRANSMISSION).
Rogers Mulindwa
CECFA MEDIA MANAGER

                                                 +256 772 751 829/+256 701 520 115


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

KUMEKUCHA! Ndivyo unaweza kusema!. Baraza la vyama vya soka kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati, CECAFA limetoa ratiba ya michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati,maarufu kwa jina la `Kagame Cup` itakayofanyika mwaka huu, mjini Kigali nchini Rwanda kuanzia Agost 8.
Mabingwa wa Tanzania msimu wa 2012/2013, Dar Young Africans wataanza kampeni ya kusaka taji hilo Agosti 8 mwaka huu dhidi ya Rayon katika dimba la  Amahoro mjini Kigali.
Hii itakuwa mechi ya kwanza ya mashindano kwa kocha mkuu wa Wanajangwani, Mbrazil Marcio Maximo aliyetua Yanga mwaka huu baada ya Mholanzi Hans van Pluijm kumaliza mkataba wake na kutimkia Saudi Arabia sambamba na aliyekuwa msaidizi wake Charles Boniface Mkwasa `Master`.
Andrey Coutinho (kushoto) akipasha moto misuli

Pia wachezaji wawili raia wa Brazil, Gleison Santos Santana na Andrey Coutinho watacheza mechi yao ya kwanza siku hiyo wakiwa kwenye uzi wa njano au kijani.
Mechi nyingine siku ya ufunguzi itawakutanisha Atlabara dhidi ya KMKM ya Zanzibar kwenye uwanja wa Nyamirambo, wakati Gor Mahia ya Kenya itacheza dhidi ya KCCA.
Agosti 10 mwaka huu, Yanga watacheza mechi ya pili ya kundi A dhidi ya Watanzania wenzao, KMKM ya Zanzibar. Na Agosti 12 mwaka huu Maximo ataiongoza tena Yanga kupepetana na Atlabara.
Agosti 16 Yanga itaoneshana kazi na Coffee katika mchezo wa mwisho wa kundi A.
Robo fainali ya kombe la Kagame itaanza kutimua vumbi Agosti 19 mwaka huu.
Afisa habari wa CECAFA , Rogers Mulindwa katika taarifa yake mchana huu amesema muda wa kuanza kwa mechi utapangwa kwa makubaliano kati ya CECAFA, shirikisho la soka nchini Rwanda (FERWAFA) na kituo cha luninga cha Supersport ambacho kitarusha moja kwa moja michuano hiyo.
Michuano ya Kagame ndio sababu kubwa ya shirikisho la soka Tanzania TFF,  kusogeza mbele michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara hadi septemba 20 mwaka huu kwa lengo la  kuwasubiri Yanga.
Awali ligi kuu ilitakiwa kuanza kushika kasi Agosti 24 mwaka huu, lakini kutokana na sababu tofauti kubwa ikiwa ni hiyo ya Kagame, ratiba akapigwa teke.
Yanga kwasasa wanaendelea na mazoezi ya kujiweka fiti kuelekea katika michuano hiyo katika uwanja wa shule ya Sekondari Loyola.
Kocha Maximo alisema ataitumia michuano ya Kagame kuona kikosi chake ili kujua mapungufu yako wapi na kuyarekebisha kabla ya kuanza ligi kuu.
Hata hivyo wachezaji wa Yanga waliopo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinachojiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Msumbuji wiki mbili zijazo, hawapo kwenye Mazoezi hayo.
Wachezaji walipo Taifa stars ni Deogratius Munish `Dida`, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub `Cannavaro`, Saimon Msuva na Mrisho Khalfani Ngassa.
Pia nyota wake wa kimataifa, Emmanuel Okwi, Khamis Kiiza `Diego` (Uganda) na Haruna Niyonzima (Rwanda) wapo  katika majukumu ya timu zao za taifa katika michuano ya mtoana kusaka tiketi ya kucheza michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, AFCON mwakani nchini Morroco.

waliotembelea blog