Tuesday, July 22, 2014


Morata suffers knee injury in trainingImechapishwa Julai 22, 2014, 2014, saa 4:26 asubuhi
ALVARO Morata ameanza kwa majanga katika klabu yake mpya ya Juventus baada ya kupata majeraha ya goti kwenye mazoezi ya kwanza.
Mshambuliaji huyo wa Kihispania mwenye miaka 21 alijiunga na mabingwa hao wa Seria A siku ya jumamosi kutokea klabu ya Real Madrid.
Nyota huyo alijigonga kwenye mazoezi na alikuwa analalamika maumivu ya goti na kwasasa kinachosubiriwa ni majibu ya vipimo.
“Kwenye mazoezi ya mchana huu (jana), Alvaro Morata ameripotiwa kupata majereha ya goti”. Juventus walithibitisha kwenye mtandao wao rasmi. “Hali yake itatathiniwa kesho (leo)”.
Morata anatarajia kupewa matibabu ya haraka ili atulie katika klabu ya Juve na kupamba na Carlos Tevez na Fernando Llorente kwenye kikosi cha kwanza cha Massimiliano Allegri.

Kocha huyo alirithi mikoba  ya Antonio Conte jumatano na Morata ndiye mchezaji wa kwanza kumsajili na atarajia kuendeleza mafanikio klabuni hapo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog