KIUNGO
wa kimataifa wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger atawasili Uwanja wa
Ndege wa Manchester kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 15
kuhamia Manchester United kutoka Bayern Munich.
Nahodha
huyo wa Ujerumani, ambaye ameongozana na mpenzi wake, nyota wa tenisi,
Ana Ivanovic, atakwenda moja kwa moja kufanyiwa vipimo vya afya na
kufanya makubaliano ya maslahi binafsi kabla ya kukamilisha uhamisho
wake Old Trafford.
Schweinsteiger anatarajiwa kwenda Manchester United katika ziara ya Amerika kucheza Kombe la Mabingwa wa Kimataifa.
Bastian Schweinsteiger akiwa kwenye ndege kuelekea mjini Manchester kukamilisha usajili wake