Mabingwa Watetezi Chelsea leo hii wamefungwa Bao 3-1 wakiwa kwao Stamford Bridge na Liverpool na kuzidisha presha kwa Meneja wao Jose Mourinho.
Nascimento Ramires aliipa Chelsea Bao la Kwanza katika Dakika ya 4 baada ya kuunganisha Krosi ya Cesar Azpilicueta.
Dakika ya 48 Liverpool walisawazisha kwa Bao la Philippe Coutinho aliepokea pasi ya Roberto Firmino na kuachia kigongo cha Mguu wa Kushoto toka Mita 18.
Haftaimu Chelsea 1 Liverpool 1.
Kipindi cha Pili Liverpool waliongezi Bao 2 kupitia Coutinho na Christian Benteke na kumpa Meneja wao mpya Jurgen Klopp ushindi mtamu huku hali ikizidi kuwa tete kwa Jose Mourinho
Jose akibaki mdomo wazi hii leo baada ya kuchapwa bao 3-1 na LiverpoolPhilippe Coutinho akiifungia bao la pili Liverpool na kufanya 2-1, Bao la Chelsea lilifungwa mapema dakika ya 4 na Ramires nao Liverpool walifunguka na kuongeza mashambulizi na kupata bao mbili kupitia kwa Coutinho dakika ya 45 kipindi cha kwanza na lile la dakika ya 74. Bao la tatu lilifungwa na Christian Benteke aliyeingia kipindi cha pili na kuipa bao la tatu na kufanya 3-1 dhidi ya Wenyeji Chelsea na kwenye Uwanja wao Stamford Bridge.2-11-1
VIKOSI:
Chelsea: Begovic, Zouma, Cahill, Terry, Azpilicueta, Mikel, Ramires, Willian, Oscar, Hazard, Diego Costa.
Akiba: Amelia, Baba, Matic, Fabregas, Kenedy, Falcao, Remy.
Liverpool: Mignolet, Clyne, Skrtel, Sakho, Moreno, Lucas, Can, Milner, Lallana, Coutinho, Firmino.
Akiba: Bogdan, Lovren, Benteke, Allen, Ibe, Teixeira, Randall.
Refa: Mark Clattenburg