Friday, August 8, 2014




azam-xi-v-yanga-11
KIKOSI cha pili cha mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc kitakabiliana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa leo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini , uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hii itakuwa mechi nzuri kwa timu zote kuangalia uwezo wa wachezaji waliowasajili na wale waliopandishwa kutoka timu za vijana.
Afisa habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga alisema wanauchukulia mchezo huo kwa uzito wa hali ya juu kwasababu ni nafasi nzuri kwa wachezaji wao kuonesha uwezo mbele ya timu bora ya Mtibwa Sugar.



1407452428918_wps_2_Manchester_City_FC_via_Pr
Manchester City wanamtaka Sergio Aguero asaini mkataba mpya kabla ya kuanza msimu mpya.
MANCHESTER City wanatumaini kuwa Sergio Aguero atasaini mkataba mpya utakaomfanya alipwe paundi laki mbili na elfu 10 kwa wiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Mabingwa hao wa England wameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa Argentina yupo katika mipango yao ya baadaye pamoja na nahodha Vincent Kompayn na mazungumzo yanaendelea vizuri.
Barcelona na Real Madrid wameweka wazi siri ya kuvutiwa na mshambuliaji huyo mwenye miaka 26, lakini City wanafanya haraka ili kumuongezea mkataba wa miaka mitano.

Mwimbaji wa Injili, Upendo Nkone akiwapa matumaini wananchi waliohudhuria Usiku wa Matumaini muda huu ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
 
Upendo Nkone akiwapa burudani wapenzi wa Gospel ndani ya Tamasha la Matumaini 2014.
 
Umati wa watu ndani ya Tamasha la Matumaini 2014.
 
Nkone akizidi kufanya yake pamoja na vijana wake.
 
Baadhi ya wanahabari na wadau wakifuatilia tamasha hilo.

 
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,


Hussein Shariff, Manyika Peter Manyika, Mohammed Hussein, Abdi Banda, Elius Maguli, Saad Kipanga watatambulishwa kesho katika Tamasha la ‘ Simba Day’ katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tamasha hilo la kila mwaka ambalo hufanyika tarehe 8, Agosti ya kila mwaka lilianza kufanyika kwa mara kwanza msimu wa kiangazi mwaka 2009 chini ya waasisi, Mzee Hassani Dalali na aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo, Mwina Kaduguda kwa lengo la kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya za klabu huku pia lengo kiuchumi likiwemo .
Wachezaji hao wazawa wataungana na wachezaji wapya wa kigeni, Paul Kiongera raia wa Kenya, Mrundi, Pierre Kwizera, na washambuliaj raia wa Botswana, Jerome  Ramathakwane na Ousainou Manneh kutoka nchini Gambia katika mchezo maalumu dhidi ya Zesco ya Zambia. Ambao watajaribiwa kwanza na kocha Zdravko Logarusic kabla ya kusajiliwa.
Hussein Sharrif 'Casillas' naye atambaulishwa kesho

Tamasha hilo litafanyika kesho Agosti 9, kufuatia siku ya leo kuwa na Tamasha la Matumaini na mashabiki wa Simba watapata fursa ya kuona na kununua jezi mpya za klabu hiyo ambazo watazitumia msimu ujao. Simba imejipanga kuhakikisha inaimarisha zaidi kikosi chake ndiyo maana wamekuwa ‘ busy’ kusaka wachezaji wakati huu dirisha la usajili likikaribia kufungwa.
WACHEZAJI SABA WA KIGENI
Donald Musoti, Amis Tambwe, Joseph Owino, Kiongera, Kwizera, Jerome, na Manneh watakuwepo uwanjani siku ya kesho. Wachezaji hao wote ni raia wa kigeni na wamekuja kwa ajili ya kuifufua Simba baada ya kuwa na misimu miwili mibaya katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Simba inaweza kuwasaini wachezaji wote hao kama mwalimu Logarusic ataridhika na viwango vyao kwa sababu sheria ya wachezaji wa kulipwa itabadilishwa na kufikia wachezaji saba.
Abdi Banda atatambulishwa kesho 'Simba Day'

Hii ni mara ya kwanza kwa Tamasha la Simba Day kuwa na wachezaji saba wa kigeni na ni wakati mwafaka kwa mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza uwanjani siku ya kesho kwa lengo la kwenda kuitazama timu yao mpya ambayo inasukwa katika mtindo wa kimataifa.
Ligi kuu inataraji kuanza kutimua vumbi lake, Septemba 20, hivyo baada ya Tamasha hilo timu itakuwa na muda mrefu wa kujiandaa na kutengeneza timu kabambe ambayo itaweza kutoa ushindani kwa timu za Yanga SC, Azam SC, Mbeya City ambazo zimeoneka kufanya usajili makini zaidi licha ya kumaliza katika nafasi tatu za juu msimu uliopita.
Wachezaji kama nahodha Nasorro Masoud ‘ Collo’, Amri Kiemba, Issa Rashid, William Lucian, Jonas Mkude, Said Ndemla, Miraji Adam, Abdallah Seseme, Ibrahimu Twaha, Ramadhani Singano, Haroun Chanongo, Uhuru Suleimani, Ivo Mapunda wataungana na wachezaji wapya waliosajiliwa klabuni hapo siku ya kesho huku mwanamuziki nyota nchini, Diamond Platnumz akitaraji kutumbuiza kabla ya zoezi la utambulisho wa wachezaji kuanza. Itakuwa siku ya aina yake kwa wapenzi wa klabu hiyo.
NI SIKU NZURI KWA KUSAIDIA UJENZI WA UWANJA WA KLABU
Wiki iliyopita Simba ilianza kufanya mazoezi katika uwanja wake wa wazi huko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na juzi wanachama wa tawi la ‘ Home Boys Wazo Hill’ waliahidi kutoa tani 10 za mifuko ya saruji ili kusaidia uendelezaji wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo ambao unaendelea. Simba inaweza kutumia Tamasha hilo kuwaunganisha wanachama wake ambao walikuwa katika tofauti miaka ya karibuni kutokana na uongozi mbaya wa utawala uliopita. Kila mwanachama wa Simba anaweza kujitolea kwa namna anavyoweza kwa sababu wanachama ndiyo sehemu muhimu ya kuijenga klabu  hivyo ushirikiano ni muhimu kuanzia kwa viongozi, wanachama, wachezaji na benchi la ufundi. Simba Day ina maana kubwa na wanachama wanaweza kutumia nafasi yao kusaidia kwa hali na mali klabu yao. Kila la heri Tamasha la Simba Day…..


Wary: Arsenal boss Arsene Wenger admits there are dangerous teams in Friday's Champions League draw
Wasiwasi: Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger alikiri kuwa kuna timu hatari katika droo ya UEFA iliyofanyika leo ijumaa.

ASERNAL watakabiliana na Besiktas  katika mchezo wa raundi ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA).
Arsene Wenger alikwepa kukutana na Athletic Bilbao, Lille , FC Copenhagen, Standard Liege, lakini sasa atachuana na timu hiyo ya Uturuki ambayo siku za karibuni ilimsajili Demba Ba kutoka Chelsea kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni  4.7.
Besiktas ilimaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita, lakini imefuzu kucheza UEFA baada mabingwa Fenerbahce kufungiwa kucheza mechi za michuano ya ulaya kwa kosa la kupanga matokeo ya mechi ya nyumbani.
Always there: Arsenal will be looking to secure their 17th successive season in Europe's elite competition
Arsenal atacheza michuano ya ulaya kwa mwaka wa 17 mfululizo 
Suspended: Defender Bartosz Bereszynski came of for the final few minutes of Celtic's defeat
Amefungiwa: Beki Bartosz Bereszynski alitolewa dakika za mwisho katika kipigo cha Celtic
Agony and ecstasy: Legia Warsaw's players celebrate at full time as Stefan Johansen is left dejected
Wachezaji wa Legia Warsaw wakishangilia baada ya dakika tisini, huku Stefan Johansen akiacha hoi.

Arsenal watasafiri kwenda Uturuki kucheza mechi ya kwanza Agosti 19 au 20 mwaka huu na mechi ya marudiano itapigwa Emirates Agosti 26 au 27.
Kiungo wa Asernal mwenye asili ya Uturuki, Mesut Ozil alifurahishwa na droo na kuandika kwenye mtandao wa Twita akisema: 'Droo nzuri! tayari tunaangalia mbele kuelekea mechi dhidi! @Besiktas! #Turkey #Ä°stanbul #Arsenal #AFC #UCLdraw'.
Wakati huo huo, leo asubuhi, Celtic wamepewa nafasi ya kusonga mbele baada ya kubainika kuwa klabu ya Legia Warsaw ilimchezesha mchezaji asiyekuwa na vigezo.
Kamati ya nidhamu ya UEFA ilikutana na kutoa maamuzi kabla ya droo mjini Nyoni na kuamua kuwa Celtic wanatakiwa kupewa ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa pili na inamaanisha wamesonga mbele kwa magoli ya ugenini.
DRAW NZIMA HII HAPA

FULL CHAMPIONS LEAGUE PLAY-OFF ROUND DRAW

Maribor vs Celtic
Red Bull Salzburg vs Malmo
Aalborg vs APOEL
Steaua Bucharest vs Ludogoret
Slovan Bratislava vs BATE
Besiktas vs Arsenal
Standard Liege vs Zenit
Copenhagen vs Bayer Leverkusen
Lille vs Porto
Napoli vs Athletic Bilbao
Ties to be played on the 19/20 and 26/27 August 


Agreed: Barcelona look to have beaten Manchester United to signing Thomas Vermaelen
Wamekubaliana: Barcelona wameonekana kuwapiku  Manchester United katika kumsajili, Thomas Vermaelen.


BARCELONA imekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15 ili kuinasa saini ya beki wa Asernal, Thomas Vermaelen, na taarifa hizi ni pigo kubwa kwa mashetani wekundu, Manchester United waliotaka kumsajili.
Kilichobaki sasa ni makubaliani binafsi kati ya wakala wa Vermaelen  na wakatalunya hao kabla ya kukamilika kwa dili hilo.
Jana jumatano, Barcelona walimtuma Raul Sanllehi kufanya makubaliano mjini London na wamefikia sehemu nzuri.
Wakatalunya wametoa ofa ya miaka mitano, huku kukiwepo kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi na mshahara wa beki huyo utakuwa paundi elfu themanini.

New surroundings? Barcelona look set to sign Vermaelen on a four-year deal worth £80,000 a week
Mazingira mapya? Barcelona wanaonekana kuelekea kumsajili Vermaelen kwa mkataba wa miaka minne na mshahara wa paundi elfu 80.
Preference: Thomas Vermaelen is set to disappoint Barcelona and current club Arsenal by joining Man United
Hakuna kwenda: Arsenal walitaka kumuuza Vermaelen Man United kwa  kubadilishana na Chris Smalling.  


 

Divas wa Skylight Band Aneth Kushaba (wa kwanza kushoto) na Digna Mbepera(wa pili toka kushoto) wakilianzisha Burudani kwa nguvu zoteee ndani ya Thai Village masaki.Kila ijumaa Bendi yako mahiri na isiyoshikika Skylight Banda wanakuwa Thai Village wakikupa burudani ya nguvuuuu na suprizeee kibaooooo,Usikose Ijumaa Hii.
Divas wa Skylight Band Aneth Kushaba (wa kwanza kushoto) na Digna Mpera(wa pili toka kushoto) wakiimba kwa umakini kabisa ili kuwapa ile kitu roho inapenda mashabiki wao
Digna Mbepera akipiga Vocal Kaliii kabisa na kwa madaha ili kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Anaitwa Mkali wa Sauti ya mtetemo Mary Lucos akiimba Vizuri kabisa ili kuwapa burudani mashabiki wake ndani ya Thai Village
Tamu ya warembo Sam Mapenzi akizitiririsha Sauti kaliiii na zenye utamu kwa wapenzi na mashabiki wa Skylight Band.
Le Meneja Her Self Aneth Kushaba akiwa na furahaa sana kuona mashabiki wao wanapata kile wanachokiitaji kutoka kwao na si kingine ni burudani iliyokwenda shule.
Babaa ya Kongo Sony Masamba Akizipiga zile za kikongo kwa umakini kabisaaaaa ndani ya Thai Village ili kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
Uniongozeeeee bila neema zako siwezi kwendaaaaaa,kwa mkono wako kweliiiiiiii umenibarikiiiiii Le Meneja Her Self Aneth Kushaba akiimba kwa Hisiaaaa kali…Nyimbo za kusifu zinahusika pia.
Baraka zakooo ziweee na Mimiiiiii kwa mkono wakooo kweliii umenibarikiiiiiiiii Le Meneja Her Self Aneth Kushaba(katikati)akiimba kwa upoleeee kabisaaa kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
Hashimu Donode Akizipigaaa Sauti kali na zenye mpangilio ndani ya Thai Village
Aneth Kushaba(wa kwanza kushoto)akiwa na Digna Mbepera (wa pili toka kushoto) wakiimba kwa kupokezana kwa rahaaaa zaooo,yote ikiwa ni kuwapa burudani mashabiki wao.



Beaming: Wilson holds the Senior Cup after his brilliant display
Grabbing the cup: The United teenager was the best player on the pitch at Ewen Fields
Bingwa: James Wilson akiwa amebeba kombe la 'Manchester Senior Cup' baada ya kuingoza United kushinda mabao 4-1 dhidi ya Cit.



KINDA wa Manchester United,James Wilson amemkumbusha Louis van Gaal umuhimu wake kwa kufunga mabao yote manne katika ushindi wa 4-1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Manchester City.
Timu hizo mbili hasimu zilikutana jana usiku katika mchezo wa fainali wa kombe la 'Manchester Senior Cup'.
Wilson  alifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Hull City msimu uliopita chini ya kocha wa muda Ryan Giggs, lakini hakuchukuliwa na Van Gaal katika ziara ya hivi karibuni ya maandalizi ya msimu nchini Marekani.
Lakini katika mechi ya jana iliyotazamwa na Manuel Pellegrini, Wilson alionesha kiwango kikubwa na kubeba kombe hilo la 'Senior Cup' baada ya kufunga mabao mawili katika kila kipinidi na kuifanya United ishinde ikitokea nyuma.
Four-midable talent: James Wilson was the hero for United, scoring four times after City went ahead
Vipaji vya hali ya juu: James Wilson alikuwa shujaa wa  United, akifunga mara nne baada ya Man City kutangulia kupata bao la kuongoza.
Fiery encounter: Typically considering the two teams playing, there were some enthusiastic challenges
Katika mechi hiyo vijana walipeana changamoto kubwa na kuonesha jinsi gani wamebarikiwa kucheza soka.
Bright start: Jordi Hiwula, centre right, leaps on Devante Cole, right, after the latter set him up to score for City
Mwanzo mzuri: Jordi Hiwula, katikati kulia, akimpanda Devante Cole, kulia, baada ya kuifungia Man City bao la kuongoza
Shielding the ball: Andreas Pereira of United tries to steal the ball from City midfielder Pablo Maffeo

Kikosi cha Manchester City: Gunn, Bossaerts, Maffeo, Bryan (Smith-Brown 46), Angelino, Glendon, Ntcham (Horsfield 53), Fofana, Cole, Pozo (Ambrose 68), Hiwula
Wachezaji: O'Brien, Bytyqi.
Mfungaji wa goli: Hiwula.
Kikosi cha Manchester United: J Pereira; Vermijl, McNair, Thorpe, Varela; Janko, Pearson, Rothwell, Lawrence; A Pereira; Wilson
Wachezaji wa akiba: O'Hara, Harrop, Goss, Willock, Evans
Mfunagi wa magoli: Wilson (4).
Watazamaji: 3,261.




 Na Baraka Mpenja
MICHUANO ya Kombe la Kagame inaanza kutimua vumbi leo hii Agost 8 hadi 24 mwaka huu mjini Kigali nchini Rwanda,  ambapo timu 14 zitawania taji linaloshikiliwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi.
Wawakilishi wawili wa Tanzania katika michuano hiyo, KMKM ya visiwani Zanzibar na mabingwa Tanzania wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc watashuka dimbani leo katika mechi za ufunguzi.
KMKM watacheza mechi ya ufunguzi ya kundi A dhidi Altabara ya Sudan kusini katika uwanja wa Nyamirambo.
Wana Lambalamba, Azam fc waliopo kundi moja A  timu hiyo ya Zanzibar, watajitupa uwanjani jioni kuoneshana ufundi na wenyeji Rayon Sport katika dimba la taifa, Amahoro mjini Kigali.
Azam fc waliokwenda Kigali na kikosi kamili gado wanatazamiwa kutoa upinzani mkubwa wa Rayon ambao watakuwa na faida kubwa ya mashabiki.
Baada ya mechi ya Azam, usiku katika dimba hilo hilo, mchezo mmoja wa kundi B utachezwa baina ya timu ya zamani ya kocha wa Simba sc, Zdrvako Logarusic na KCCA ya Uganda.
Kesho Agosti 9 mwaka huu katika dimba la Amahoro  mechi mbili za kundi C na moja ya kundi B zitapigwa.
Mapema itaanza mechi ya mabingwa Vital’O ya Burundi dhidi ya Benadir ya Somalia ikifuatiwa na mechi ya jioni baina ya Police ya Rwanda na El Merreikh ya Sudan.
Baadaye usiku maafande wa jeshi, APR ya Rwanda watachuana na Flambeau ya Burundi.
Azam fc watashuka dimbani tena Agosti 10 mchana kuchuana na KMKM ya Zanzibar, mchezo wa kundi A.

 


BAADA ya kutolewa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kwa jina la kombe la Kagame, Yanga sc imesema maisha mengine yanatakiwa kuendelea kama kawaida.
Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu alisema wamesikitishwa kutolewa Kombe la Kagame, lakini hali hiyo haiwafanyi washindwe kuendelea na mipango mingine ya kuiandaa timu kwa ajili ya michuano iliyopo mbele yao.
 Njovu alisema wachezaji waliotakiwa kwenda Kagame wanaendelea na mazoezi kama kawaida na wale waliokuwa timu za taifa za nchi mbalimbali (Tanzani, Rwanda na Uganda) walipewa mapumziko na wataripoti kesho jumamosi kwenye mazoezi ya timu yanayoendelea uwanja wa shule ya sekondari  Loyola, Mabibo, jijini Dar es salaam.

“Maisha yanatakiwa kuendelea kama kawaida. Wale wachezaji waliotakiwa kwenda Kagame, mnaona wanaendelea na mazoezi kama kawaida na wale waliokuwa timu ya taifa wamepewa mapumziko mpaka jumamosi.” Alisema Njovu.
“Jumamosi wachezaji watafanya mazoezi. Wachezaji wote waliokuwa na timu za taifa watakuwepo, halafu watakuwa na kikao na mwalimu kupanga mikakati ya michuano iliyopo mbele yetu”
“Michuano iliyopo mbele yetu ilikuwa Kagame, lakini kwasababu tumetolewa, sasa michuano iliyopo mbele yetu ni ligi kuu, wataanza kupanga mikakati mara moja na kuingia kambini”
Baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika mashariki na kati CECAFA iliwatoa Yanga kushiriki kombe la Kagame baada ya kukataa kutuma kikosi cha kwanza.
Awali Yanga ilituma kikosi cha pili cha wachezaji 20, lakini CECAFA ikakitaa na kuitaka klabu hiyo kuthibitisha kutuma kikosi cha kwanza, lakini wanajangwani hawakufanya hivyo na wakatupwa nje ya michuano.
Baada ya tukio hilo, CECAFA waliwasiliana na TFF na kulitaka Shikirikisho hilo kuchagua timu nyingine na zali likawaangua Azam fc.



On the score sheet: Ryan Giggs slots home a goal in front of a 12,000 crowd to the AJ Bell Stadium but couldn't stop his side suffering a 5-1 defeat
Mtaalamu: Ryan Giggs alifunga bao pekee la kufutia machozi katika kichapo cha mabao 5-1.
Midfield maestro: Paul Scholes keeps his composure in game against the side he now co-owns one year after retiring from professional football
Kiungo mwalimu: Paul Scholes akimiliki mpira kuonesha kuwa ujuzi hauzeeki.
Wing wizard: Manchester United's new assistant manager Ryan Giggs performs a trademark dribble past Salford City opponent
Winga mchawi: Kocha mpya msaidizi wa Manchester United, Ryan Giggs akimpiga chenga mpinzani wake wa  Salford City
On managerial duties: Former Manchester United star Rio Ferdinand
Majukumu ya ukocha: Nyota wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand

MAGWIJI wa Manchester United wale wa kikosi cha mwaka 1992 ‘Class of 92’ walishindiliwa kipigo kizito cha mabao 5-1 dhidi ya timu ya daraja la chini ya Salford City jana usiku.
Salford ni timu ambayo inamilikiwa na magwiji, Paul Scholes, Nicky Butty na Gary na Phil Neville.
Mchezo huo ulikuwa wa hisani na ulitazamwa na mashabiki  wapatao 12,00 katika dimba la Aj Bell Mjini Eccles.
Katika mchezo huo, Mkongwe Ryan Giggs ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa Manchester United alimtamanisha kocha wake mkuu Louis Van Gaal kwa kufunga bao moja la kufutia machozi katika kipigo hicho cha mbwa mwizi.
Pamoja na kuzidiwa kasi na vijana wa timu hiyo kutokana na umri kuwa mkubwa, lakini nyota hao wa zamani wa Man United walionesha kiwango kizuri na kudhihirisha kuwa ujuzi hauzeeki.
Rio Ferdinand aliyesafiri kuwafundisha magwiji hao kama kocha msaidizi, alishindwa kuwanusuru na kichapo.

waliotembelea blog