Wednesday, January 11, 2017


 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe  na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka pamoja na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8 wengine katika picha ni  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Luhaga Mpina, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CCM Simiyu Titus Kamani na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Bariadi kabla ya kufungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi, katika mkoa wa Simiyu.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Bariadi mara baada ya kumaliza kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8.


Tiemoue Bakayoko, MonacoTiemoue Bakayoko kusajiliwa na Man United?


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (Kushoto) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Mwanamuziki wa nyimbo za Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Dar es Salaam leo, kabla ya kwenda kuliwakilisha Taifa kwa kufanya shoo wakati wa ufunguzi wa michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON 2017). Wapili kulia ni Balozi wa DStv, Lucas Mhavile ‘Joti’.
You might also like:



MASHINDANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yataanza Jumamosi Januari 14 huko Gabon na kushirikisha Nchi 16 zilizogawanywa Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.

AFCON, ambayo Fainali yake itakuwa Februari 5, itachezwa kwenye Viwanja Vinne vya Miji ya Libreville, Franceville, Oyem na Port Gentil.
Viwanja vitakavyotumika ni Stade de l’Amitié huko Libreville, Gabon, unaochukua Watu 38,000, ambako Kundi A ndio litacheza Mechi zake, na kingine cha Kundi B ni Port Gentil Stadium, Port Gentil, wenye kuchukua Washabiki 20,000, Kundi C lipo Stade de Franceville Mjini Franceville wenye uwezo wa Watu 20,000 wakati Kundi D litakuwa huko Oyem Stadium ulioko Assok Ngomo, Gabon, uwezo 20,000.

Mabingwa Watetezi wa Afrika ni Ivory Coast lakini safari hii watawakosa Wachezaji wao wakubwa, wale Ndugu Toure, yaani Yaya na Kolo, ambao wamestaafu, na Majeruhi Yao Gervinho.



MAKUNDI:
KUNDI A:
Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea-Bissau
KUNDI B: Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe
KUNDI C: Ivory Coast, DR Congo, Morocco, Togo
KUNDI D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda

Ivory Coast walitwaa Ubingwa wa Afrika huko Equatorial Guinea Mwaka 2015.

Wenyeji Gabon wapo Kundi A pamoja na Burkina Faso, Cameroon na Guinea-Bissau iliyotinga Fainali kwa mara ya kwanza.
Jirani zetu Uganda wapo kundi D pamoja na Ghana, Mali na Egypt ambao wanarejea kwenye Fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu watwae Ubingwa Mwaka 2010.

AFCON 2017RATIBA
Mechi za Makundi
Jumamosi Januari 14
Kundi A

1900 Gabon v Guinea-Bissau
2200 Burkina Faso v Cameroon

Jumapili Januari 15
Kundi B

1900 Algeria v Zimbabwe
2200 Tunisia v Senegal

Jumatatu Januari 16
Kundi C

1900 Ivory Coast v Togo
2200 Congo DR v Morocco

Jumanne Januari 17
Kundi D

1900 Ghana v Uganda
2200 Mali v Egypt

Jumatano Januari 18
Kundi A

1900 Gabon v Burkina Faso
2200 Cameroon v Guinea-Bissau

Alhamisi Januari 19
Kundi B

1900 Algeria v Tunisia
2200 Senegal v Zimbabwe

Ijumaa Januari 20
Kundi C

1900 Ivory Coast v Congo DR
2200 Morocco v Togo

Jumamosi Januari 21
Kundi D

1900 Ghana v Mali
2200 Egypt v Uganda

Jumapili Januari 22
Kundi A

2200 Cameroon v Gabon
2200 Guinea-Bissau v Burkina Faso

Jumatatu Januari 23
Kundi B

2200 Senegal v Algeria
2200 Zimbabwe v Tunisia

Jumanne Januari 24
Kundi C

2200 Morocco v­­ Ivory Coast
2200 Togo v Congo DR

Jumatano Januari 25
Kundi D

2200 Egypt v Ghana
2200 Uganda v Mali

Robo Fainali
Jumamosi Januari 28

1900 Mshindi Kundi A v Mshindi wa 2 Kundi B
2200 Mshindi Kundi B v Mshindi wa 2 Kundi A

Jumapili Januari 29

1900 Mshindi Kundi C v Mshindi wa 2 Kundi D
2200 Mshindi Kundi D v Mshindi wa 2 Kundi C

Nusu Fainali
Jumatano Februari 1

2200 Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4

Alhamisi Februari 2

2200 Mshindi RF 2 v Mshindi RF 3

Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4

2200 Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2

Fainali
Jumapili Februari 5

2200 Finalist 1 v Finalist 2

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1


HABARI toka England zimebaini kuwa Klabu za Manchester United na Everton zimeafikiana Ada ya Uhamisho ya Pauni Milioni 22 kwa Kiungo Morgan Schneiderlin.
Schneiderlin, mwenye Miaka 27, alisaini Manchester United kutoka Southampton kwa Dau la Pauni Milioni 25 Julai 2015 kwenye wakati wa himaya ya Meneja Louis van Gaal.
Kiungo huyo wa Kimataifa wa France ameichezea Man United Mechi 47 lakini tangu ujio wa Jose Mourinho Msimu huu amecheza Mechi 8 tu na 3 zikiwa za EPL, Ligi Kuu England.
Mara Jana baada ya Man United kuifunga Hull City 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP, Mourinho aligusia Uhamisho wa Schneiderlin na kueleza kuwa Makamu Mwenyekiti Mtendaji Ed Woodward alimweleza kuwa Mchezaji huyo anakaribia kuhama.
Mourinho alisema: "Nasikitika na nina furaha, nasikitika kwa sababu nampenda na angeweza kutusaidia kinamna lakini nina furaha kwa sababu hili ndio alilitaka, anataka kucheza kila Mechi na kuwa muhimu kwenye Timu!"
Ikiwa Uhamisho huu wa Schneiderlin utakamilika, Mchezaji huyo ataungana tena na Meneja Ronald Koeman huko Goodison Park baada ya kuwa wote kwa Miaka Miwili huko Southampton.
Mbali ya Schneiderlin, Koeman pia anamtaka Mchezaji mwingine wa Man United, Memphis Depay, atue Everton.
Lakini kwa Depay, Everton huenda wakaingia mvutano na Klabu nyingine za Ulaya zinazomtaka.
Depay, mwenye Miaka 22, alijiunga Man United Mei 2015 kwa Dau la Pauni Milioni 25 kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi.


EFL CUP
Nusu Fainali
Ratiba/Matokeo:
Jumanne Januari 10

Manchester United 2 Hull City 0

Jumatano Januari 11

22:45 Southampton V Liverpool
Manchester United, ikiongozwa na MenejaJose Mourinho, wamepiga hatua kubwa kuelekea kutwaa Taji kubwa la pili Msimu huu baada ya Jana huko kwao Old Trafford kuichapa Hull City 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi huko England.
Mwanzoni mwa Msimu, Man United walitwaa Ngao ya Jamii.
Juan MataBao za Man United, waliochezesha karibu Kikosi chao chote, zilifungwa na Juan Mata na Marouane Fellaini alieanzia Benchi. Markus HenriksenBao la Mata lilifungwa Dakika ya 56 alipounganisha Kichwa cha Henrikh Mkhitaryan na la pili Dakika ya 87 kupitia Fellaini alieunganisha Krosi ya Matteo Darmian. Wayne RooneyHull City na Man United zitarudiana huko KCOM Stadium hapo Januari 28. Jose MourinhoLeo Jumatano Januari 11 itachezwa Nusu Fainali ya Pili huko Saint Mary kwa Southampton kucheza na Liverpool.
Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.

EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
Jumatano Januari 25

23:00 Liverpool v Southampton

Alhamisi Januari 26
22:45 Hull City v Manchester United [0-2]


Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi Tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, iliyokuwa Bigi Mechi, Dabi ya Kariakoo iliyohamia Amaan Stadium Zanzibar. Ilichezwa Usiku na Simba na Yanga kutoka 0-0 katika Dakika 90 lakini Simba kuibuka kidedea kwa Mikwaju ya Penati 4-2 na kutinga Fainali watakayocheza na Azam FC.
Katika Nusu Fainali nyingine iliyochezwa mapema Taifa Jang’ombe ya Zanzibar ilifungwa 1-0 na Azam FC kwa Bao la Dakika ya 33 la Frank Domayo.

Kwenye Mechi ya Watani wa Jadi, Timu zote zilishambuliana kwa zamu ingawa Yanga walionekana kutawala zaidi bila matunda yeyote na Gemu kuamuliwa kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano.

Katika Penati hizo, Simba walifunga kupitia Kepteni wao Jonas Mkude, Kipa Daniel Agyei, Muzamil Yasin na Bokungu wakati ile iliyopigwa na Mwanjali kuokolewa na Kipa wa Yanga Munishi.

Penati za Yanga zilifungwa na Simon Msuva na Thabani Kamusoko na zile za Kipa Munishi na Mwinyi Haji ziliokolewa na Kipa wa Simba Daniel Agyei.

Fainali ya Mapinduzi Cup itachezwa Ijumaa Januari 13.

VIKOSI VILIVYOANZA:
YANGA:
Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Saidi Juma ‘Makapu’, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke

SIMBA:
Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Juma Luizio, Muzamil Yassin, Mohamed
Ibrahim

Mohamed Ibrahim akimtoka beki wa Yanga wakati mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi leo Usiku katika uwanja wa Amani, Simba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-2

Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akijaribu kumtoka beki wa Yanga Haji Mwinyi kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi leo Usiku katika uwanja wa Amani, Simba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-2­­
KOMBE LA MAPINDUZI
Ratiba/Matokeo:
Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017
KVZ 0 URA 2
Simba 2 Taifa Jang'ombe 1
 

Januari 2, 2017 Azam 1 Zimamoto 0
Yanga 6 Jamhuri 0

Januari 3, 2017
Jang'ombe Boys 2 URA 1
KVZ 0 Simba 1

Januari 4, 2017
Zimamoto 0 Yanga 2
Jamhuri 0 Azam 0

Januari 5, 2017
KVZ 1 Jang'ombe Boys 3
Simba 0 URA 0

Januari 6, 2017
Taifa Jang'ombe 3 KVZ 1

Januari 7, 2017

Jamhuri 0 Zimamoto 2
Yanga 0 Azam 4

Januari 8, 2017

Simba 2 Jang'ombe Boys 0
Taifa Jang'ombe 1 URA 0

Januari 10, 2017
Nusu Fainali

Azam FC 1 Taifa Jang’ombe 0
Simba 0 Yanga 0 [Penati 4-2]

Ijumaa, Januari 13, 2017
FAINALI

Saa 2: 15 Usiku
Azam FC v Simba


Mabingwa Watetezi wa Kombe la Mapinduzi Cup URA, kutoka Nchini Uganda wakiwa na butwaa baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Timu ya Taifa ya Jangombe katika mchezo wao wa mwisho kuwania kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ya 11 ya Mapinduzi Cup inayofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Timu ya Taifa ya Jangombe itaungana na Timu za Yanga, Simba na Azam katika mchezo wa Nusu Fainali utakaofanyika siku ya Jumanne katika uwanja wa Amaan Zanzibar. kwa mechi mbili jioni na usiku
Katika mchezo wa jioni wa michuano hiyo hatua ya nusu fainali itazikutanisha Timu ya Taifa ya Jangombe na Azam utachezwa kesho jioni na wakati wa usiku nyasi za uwanja wa Amaan zitapata kishindo cha mchezo wa watani wawili Simba na Yanga zitaumana kuwania nafasi ya kucheza fainali tarehe 13-1-2017. kuhitimisha michuano hiyo ya kumi na moja ya Mapinduzi Cup,








FAINALI za Kombe la Dunia zitapanuliwa na kushirikisha Nchi 48 kutoka 32 za hivi sasa.
Mabadiliko hayo yamepitishwa Leo huko Zurich, Uswisi kwa Kura nyingi na yataanza kwenye Fainali za Mwaka 2026 ambazo bado hazijapata Mwenyeji.
Fainali zijazo zitachezwa huko Russia Mwaka 2018 na zinazofuata ni huko Qatar Mwaka 2022 na zote zitakuwa na Timu 32 tu.
Kwenye Mfumo wa Timu 48 kwenye Fainali, Mechi za Awali zitakuwa za Makundi 16 ya Timu 3 kila moja ambayo yatatoa Timu 32 kwenda Raundi ya Mtoano.

Kwa Mfumo huo mpya Jumla ya Mechi kwenye Fainali zitakuwa 80 kutoka 64 za sasa lakini Bingwa wa Dunia atacheza Mechi 7 tu kama ilivyo sasa ambazo zote zitakamilika ndani ya Siku 32.
Hii ni mara ya kwanza kwa FIFA kuongeza idadi ya Timu kwenye Fainali za Kombe la Dunia tangu zilipopanuliwa Mwaka 1998 na kuwa za Timu 32 kutoka 24.
Kwa mujibu wa tafiti za FIFA upanuzi huu utafanya Mapato yaongezeke na kuwa Pauni Bilioni 5.29 na kuleta Faida kuwa Pauni Milioni 521.

FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA - Timu 48:
-Makundi: Mechi 2

-Raundi ya Mtoano ya Timu 32
-Raundi ya Mtoano ya Timu 16
-Robo Fainali
-Nusu Fainali
-Fainali

waliotembelea blog