Klabu ya Manchester United bado ipo katika kinyang’anyiro cha kuwania Kombe laEUEFA Europa, kombe ambalo ni la pili kwa ukubwa barani Ulaya baada ya Kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya, Man United usiku wa February 18 walikuwa wageni wa FC Midtjylland, walikubali kipigo cha goli 2-1. Magoli ya FC Midtjylland yalifungwa na Pione Sisto dakika ya 44 na Paul Onuachu dakika ya 77 wakati goli la pekee la Man Unitedlilifungwa dakika ya 37 na Memphis Depay.