Leo
Messi amefunga magoli matatu kwenye mechi kati ya Barcelona na Osasuna,
magoli haya yamemfanya afikishe jumla ya magoli 371 akiwa na Barcelona
na kumfanya awe mfungaji bora wa klabu hiyo. Kabla ya mechi ya
leo Paulino Alcantara ndiye alikuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi
kuliko wote lakini magoli matatu ya Messi yamemfanya Muargentina huyu
kuwa kinara wa kufunga magoli kwenye historia ya klabu ya Barcelona.
Kwasasa Messi anaitafuta rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi
kwenye ligi ya Hispania ambayo bado inashikiliwa na Telmo Zarra mwenye
magoli 251 akiwa amemzidi Messi kwa magoli 18. Ikumbukwe magoli 371 ya
Messi yanajumuisha mechi zote za Barcelona ikiwemo mechi za ligi, Uefa,
Copa na mechi za kirafiki. Lakini magoli ya ligi pekee Messi ameshafunga
233 tu wakati mtani wake Cristiano Ronaldo ana magoli 171.
Messi akiondoka na mpira kama ukumbusho baada ya kufunga magoli matatu kati ya saba dhidi ya Osasuna.