Kipindi cha pili dakika za mwishoni dakika ya 80 Arjen
Robben amewakaanga mabeki na kuwafunga pamoja na kipa wao Spain baada
ya kuwazidi mbio na kuachia shuti kali lililofanya mabao kuwa 5-1 dhidi
ya Spain ambao ni Mabingwa Watetezi wa Dunia wa Kombe hili.Historia hii...nimetupia 2!!!
Dakika ya 64 tena Stefan de Vrij
ameoingozea bao la tatu timu ya Netherlands na kufanya matokeo kuwa 3-1
dhidi Spain. Wesley Sneijder ndie alietoa pande hilo lililozaa bao.
Stefan de Vrij aliyefunga bao la tatu huku van persie akimzonga kipa ili bao lifanikiwe...
De Vrij wa Holland akishangilia baada ya kuichakaza bao la tatu Spain kwa kufanya 3-1 akishangilia kwa raha zake...
Kipindi
cha pili dakika ya 53 Arjen Robben alipewa pasi safi na Daley Blind na
kufunga bao la pili kwa timu ya Netherlands na kufanya 2-1 dhidi ya
Spain.Dakika
ya 27 kipindi cha kwanza Xabi Alonso ndie aliyeifungia bao kwa mkwaju
wa penati na kuitanguliza mbele Spain kwa bao 1-0 dhidi ya Netherlands. Dakika
ya 44 mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha dakika 45 mchezaji matata Van
Persie amewatoka mabeki wa Spain na kuruka kwa kichwa maridadi na
kuisawazishia bao kwa kufanya 1-1 timu ya Netherlands. Mpaka dakika za
kipindi cha kwanza zinamalizika timu zote mbili zilikuwa kwenda
kupumzika zikiwa nguvu sawa kwa bao 1-1. Van Persie akitupia.....
VIKOSI:
Spain: Casillas, Azpilicueta, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Alonso, Xavi, Busquets, Silva, Diego Costa, Iniesta.
Subs: De Gea, Albiol, Javi Martinez, Juanfran, Villa, Torres, Fabregas, Pedro, Mata, Koke, Cazorla, Reina.
Holland: Cillessen, Janmaat, Vlaar, De Vrij, Martins Indi, Blind, De Guzman, Sneijder, De Jong, van Persie, Robben.
Subs: Vorm, Verhaegh, Veltman, Kongolo, Kuyt, Clasie, Lens, Fer, Huntelaar, Wijnaldum, Depay, Krul.
Referee: Nicola Rizzoli (Italy)
Mchezaji wa Netherlands Stefan de Vrij kamwangusha kwenye eneo la Hatari Diego Costa
Xabi Alonso akiifungia bao Spain kwa mkwaju wa penati...
Xabi Alonso wa Spain akishangilia bao lake
Asante baba!!!! Wachezaji wa Spain wakimpongeza Alonso.
Fowadi wa Spain Diego Costa akimwendesha difenda wa Holland Stefan de Vrij
Nipishe!!!
Wachezaji wa Spain wakiimba wimbo wao wa Taifa
Wachezaji wa Holland wakijifua wakiwa wao ni kundi B kujiweka sawa na kipute na Spain
Wachezaji wa Holland wakijifua vikali
Wachezaji wa Spain nao wakijiweka sawa kuwakabili Holland
Wachezaji wa Spain wakipasha
Costa kuanza kwenye kipute hiki....
Baada ya muda mfupi ni kipute kuanza...
Jezi za Wachezaji wa timu ya Holland