2:15 AM
Unknown
Kipa
mkongwe nchini, Ivo Mapunda amejiunga na Azam FC. Ivo atapewa mkataba
wa mwaka mmoja na Mtedaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema kipa
huyo amesajiliwa baada ya pendekezo la Kocha Stewart Hall. “Kocha
alisema anataka kipa mzoefu nasi tukampa nafasi hiyo,” alisema. “Lakini
mkataba hauwezi kuzidi mwaka mmoja kwa kuwa huenda Ivo atakuwa na
mipango yake mingine,” alisema. Ivo aliomba kufanya mazoezi na kikosi
cha Azam FC baada ya kuachwa na Simba katika hatua za mwisho kabisa za
usajili baada ya uongozi wa Msimbazi, kusema alikuwa akiwasumbua licha
ya kuwa wameishampa fedha