Tuesday, October 20, 2015



Ivan Rakitic akipongezana na  Jordi Alba baada ya kuichapa  BATE Borisov kipindi cha pili

Mlinda mlango  Sergei Chernik akifanyiwa mbaya na Rakitic
Luis Suarez akifanya yake kwa wachezaji wa BATE
Mchezaji wa BATE Borisov Maksim Volodko akimkaba kwa nyuma  Sergi Roberto leo jumanne usiku
Volodko na  Javier Mascherano wakipambana kwenye  Champions League
 Neymar akichuana na  Vitali Gayduchik wa BATE

Rakitic na  Nemanja Nikolic

Mchezaji wa Barca Munir El Haddadi akimiliki mpira

Suarez akigombea mpira wa kichwa

Ivan Rakitic dakika ya 64 alipachika tena bao na Barca kuongoza kwa bao 2-0 dhidi ya Bate.Nemanja Nikolic akichana na Ivan Rakitic wa Barca mapema kipindi cha kwanza abacho kilimalizika 0-0. 
Kipindi cha pili dakika ya 48 Ivan Rakitic aliwapatia bao la kuongoza Barca kwa kufanya 1-0 baada ya kupata ushirikiano safi  kutoka kwa Neymar


Baooo!2-0Ozil akishangilia bao lake la dakika za majeruhi!Balaa!Olivier Giroud dakika ya 77 aliipatia Arsenal bao na kufanya 1-0 dhidi ya Bayern Munich. Dakika ya 90 kwenye muda wa lala salama  Arsenal waliongeza kasi na kuweza kupata bao na mtanange kumalizika 2-0, Bao likifungwa na Mesut Ozil.Alama tatu muhimu!Petr Cech akiokoa langoni mwakeTheo Walcott akijishangaa Kipa wa Bayern Munich Neuer akiokoa shuti langoni mwake katika kipindi cha kwanza kilichomalizika 0-0 dhidi ya Arsenal. 
Kipindi cha pili dakika ya 55 Ramsey aliumia na nafasi yake imechukuliwa na Alex Oxlade-Chamberlain



Willian akiachia shuti

Meneja wa Chelsea  Jose Mourinho kalazimishwa sare na Dynamo Kiev

Cesc Fabregas akipambana na  Yevhen Khacheridi

Diego Costa akifanya yake

Mashabiki wa Chelsea
Piga nikupige dakika 90 hakuna aliyeliona lango la mwenzake! Hapa siyo England!!! Cesc Fabregas akiteta jambo na refa Damir Skomina Nemanja Matic akiangalia mpiraEden Hazard aliachia shuti na kugonga post ya lango

FIFA Leo imetangaza Listi ya Wachezaji 23 ambao watawania Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka 2015, FIFA Ballon d'Or.
Miongoni mwa hao ni Cristiano Ronaldo, ambae ndie alietwaa Tuzo hiyo kwa Miaka Miwili iliyopita huku Lionel Messi akitajwa pia na ambae wengi wanadhani Mwaka huu ni zamu yake.
Mshindi Ballon d'Or huamuliwa kwa Kura inayohusisha Makocha na Makepteni wa Timu za Taifa Wanachama wa FIFA na Wawakilishi maalum kutoka Wanahabari.
Wagombea wote 23 wa Listi hii wanacheza Soka lao Barani Ulaya huku 11 wakitoka La Liga, 5 Ligi Kuu England, 5 toka Bundesliga na mmoja mmoja kutoka Ligi 1 na Serie A.
Klabu inayoongoza kwa kuwa na Wagombea wengi ni Bayern Munich yenye Wachezaji Watano ikifuatiwa na Real Madrid yenye Wanne. 

Kiinchi, Argentina na Germany, ambazo ndizo zilikutana Fainali za Kombe la Dunia za 2014 na Germany kuwa Mabingwa, ndizo zenye Wachezaji wengi wakiwemo Messi, Javier Mascherano, Sergio Aguero, Toni Kroos, Thomas Muller na Kipa Manuel Neuer.
Sherehe ya kutunuku FIFA Ballon d'Or itafanyika Tarehe 11 Januari 11 2016 huko Zurich, Uswsisi.

LISTI YA WACHEZAJI 23:
Sergio Aguero (Manchester City/Argentina)
Gareth Bale (Real Madrid/Wales)
Karim Benzema (Real Madrid/France)
Kevin De Bruyne (Manchester City/Belgium)
Eden Hazard (Chelsea/Belgium)
Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain/Sweden)
Andres Iniesta (Barcelona/Spain)
Toni Kroos (Real Madrid/Germany)
Robert Lewandowski (Bayern Munich/Poland)
Javier Mascherano (Barcelona/Argentina)
Lionel Messi (Barcelona/Argentina)
Thomas Muller (Bayern Munich/Germany)
Manuel Neuer (Bayern Munich/Germany)
Neymar (Barcelona/Brazil)
Paul Pogba (Juventus/France)
Ivan Rakitic (Barcelona/Croatia)
Arjen Robben (Bayern Munich/Netherlands)
James Rodriguez (Real Madrid/Colombia)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal)
Alexis Sanchez (Arsenal/Chile)
Luis Suarez (Barcelona/Uruguay)
Yaya Toure (Manchester City/Ivory Coast)
Arturo Vidal (Bayern Munich/Chile)



Wenger na GuardiolaMSIMAMO/MECHI ZA LEO 


Kocha Mkuu Pellegrini akiwaangalia kiufundi Vijana kazi wakePellegrini akitoa darasaKompany na Kevi De BruyneKikosi cha City MazoeziniMbele ya Kocha wao Pellegrini
Vicent Company na wenzake kwenye mazoezi kujiandaa vyema kwa Uefa Champions


Wachezaji watatu wa Manchester City Sergio Aguero, Kevin De Bruyne na Yaya Toure ni miongoni wa wachezaji 23 walioorodheshwa kushindania tuzo ya Ballon d'Or.
Kiungo wa Chelsea Eden Hazard na mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez pia wamo kwenye orodha hiyo ya kuteua mchezaji bora wa mwaka duniani.

www.bukobasports.comTuzo hiyo ya Ballon d'Or kwa sasa inashikiliwa na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye pamoja na Lionel Messi wa Barcelona, wamekuwa wakishinda tuzo hiyo kwa miaka saba iliyopita. Wawili hao bado wamo kinyang’anyironi mwaka huu.
Mshambuliaji wa Real Madrid kutoka Wales Gareth Bale ndiye mchezaji Mwingereza pekee aliyetajwa kwenye orodha hiyo.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho na mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger nao wamo kwenye orodha ya wakufunzi 10 watakaopigania tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka.
Watamenyana na meneja wa Barcelona Luis Enrique na kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola.
Katika orodha hiyo, La Liga ya Uhispania inaongoza kwa kuwa na wachezaji 11, nayo Bundesliga ya Ujerumani ina wachezaji sita. Serie A ya Italia ina wachezaji wawili.

http://www.bukobasports.comUfaransa inawakilishwa na mchezaji mmoja pekee, kigogo wa Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic.
  1. Sergio Aguero (Argentina/Manchester City)
  2. Gareth Bale (Wales/Real Madrid)
  3. Karim Benzema (France/Real Madrid)
  4. Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid)
  5. Kevin De Bruyne (Belgium/VfL Wolfsburg/Manchester City)
  6. Eden Hazard (Belgium/Chelsea)
  7. Zlatan Ibrahimovic (Sweden/Paris Saint-Germain)
  8. Andres Iniesta (Spain/FC Barcelona)
  9. Toni Kroos (Germany/Real Madrid)
  10. Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich)
  11. Javier Mascherano (Argentina/FC Barcelona)
  12. Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona)
  13. Thomas Muller (Germany/FC Bayern Munich)
  14. Manuel Neuer (Germany/FC Bayern Munich)
  15. Neymar (Brazil/FC Barcelona)
  16. Paul Pogba (France/Juventus)
  17. Ivan Rakitic (Croatia/FC Barcelona)
  18. Arjen Robben (Netherlands/FC Bayern Munich)
  19. James Rodriguez (Colombia/Real Madrid)
  20. Alexis Sanchez (Chile/Arsenal)
  21. Luis Suarez (Uruguay/FC Barcelona)
  22. Yaya Toure (Côte d'Ivoire/Manchester City)
  23. Arturo Vidal (Chile/Juventus/FC Bayern Munich)


www.bukobasports.comKocha wa Chelsea, Jose Mourinho, amejitetea kuwa kinachodhaniwa ni lugha mbovu aliyotumia baada ya kushindwa na Southampton ni kwa kuwa Kiingereza si lugha yake ya mama.
Mourinho alifungiwa mechi moja na kupigwa faini ya Pauni za Uingereza 50,000 na shirikisho la Kandanda la Uingereza. Alidai kuwa maafisa wa kandanda nchini humo wanaogopa kuipa timu yake penalti inayostahili. Madai ya Morinho yalitolewa baada ya tume huru maalimu kutoa sababu za adhabu hiyo kutolewa na FA. Kocha huyo machachari wa Chelsea hakuhudhuria kilichomwadhibu lakini alituma taarifa ya maandishi kujitetea. 
www.bukobasports.comAlikiri kuwa alikosa adabu lakini akakanusha kuwa alitilia shaka hadhi ya refa Robert Madley. Huku akijitetea, Moorinho alisema kuwa makosa yaliyompata ni sawa na yale yaliyowahusu makocha wengine watano wa Premier League. Mbali na kukosoa kiwango cha faini aliyotozwa, Mourinho pia alisema kuwa kupigwa marufuku uwanjani kwa mechi moja, ambako kumeahirishwa kutekelezwa kwa mwaka mmoja, "kulimshangaza". Wenger hakuchukuliwa hatua yo yote alipomsukuma Mourinho katika eneo la wakufunzi katika Stamford Bridge Oktoba mwaka 2014.


Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini amesema bado ana moyo wa kutaka kumrithi Sepp Blatter kama Rais wa shirikisho la Kandanda duniani FIFA, licha ya kupigwa marufuku ya siku 90 ili kupisha uchunguzi wa madai ya ufisadi dhidi unaoendelea dhidi yake. Platini, mpaka sasa anatumikia adhabu baada ya kupokea Pauni za Uingereza milioni 1.35 kutoka kwa Blatter mwaka 2011. 


KIKOSI cha Wachezaji 20 wa Manchester United Leo hii wamesafiri kwenda Moscow, Urusi ambako Kesho Usiku watacheza Mechi yao ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, na CSKA Moscow.Kikosi hicho kimeundwa na Wachezaji 18 ambao ndio walicheza na kuwa Benchi Jumamosi iliyopita huko Goodison Park walipoichapa Everton Bao 3-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Wachezaji Wawili walioongezwa ni Kipa Sergio Romero na Antonio Valencia.

Kwenye Kundi B kila Timu ina Pointi 3 baada ya Mechi 2 na Mechi hizi za 3 ni muhimu katika kufungua njia ya kufuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

Mechi nyingine kali za UCL ambazo zitachezwa Kesho ni ile ya Jijini Manchester Uwanjani Etihad wakati Man City wakiikaribisha Sevilla ya Spain kwenye Mechi ya Kundi D na huko Jijini Paris Nchini France ipo Mechi ya Kundi A kati ya Paris St Germain na Real Madrid.
MAN UNITED WACHEZAJI 20 WALIOKWEA NDEGE NI
De Gea, Romero, Johnstone, Darmian, Smalling, Jones, Rojo, Blind, Carrick, Schweinsteiger, Schneiderlin, Fellaini, Valencia, Pereira, Mata, Herrera, Memphis, Lingard, Rooney, Martial.

Meneja wa Man United Van Gaal

Wayne Rooney

UEFA CHAMPIONS LEAGUE
MAKUNDI
Jumanne Oktoba 20
KUNDI E

BATE Borislov v Barcelona
Bayer Leverkusen v AS Roma

KUNDI F

Arsenal v Bayern Munich
Dinamo Zagreb v Olympiakos

KUNDI G

Dynamo Kiev v Chelsea
FC Porto v Maccabi Tel Aviv

KUNDI H

Valencia v KAA Gent
Zenit Saint Petersburg v Lyon

waliotembelea blog