Monday, June 22, 2015




Afisa Mtendaji Mkuu wa  EAG Group Imani Kajula Akimwelezea Jambo Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (Aliyekaa) Wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Club Hiyo Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu
Simba Sports Club leo hiiimezindua tovuti yake Ili kukuza  mawasiliano  na  wadau wake mbalimbali  hususani; wanachama, wapenzi, vyombo  vya  habari na wadau wengine muhimu. 
Akizungumza  wakati  wauzinduzi  huo  Rais  wa  Simba Evans Aveva  alisema ‘’Katika dunia na zama  za utandawazi  tovuti  ndio  na  mitandao   ya   jamii   ndio  njia  kuu ya mawasiliano. Sisi  tuliliona  hili  na  leo  hii  nafurahi  kuwa  Simba Sports Club itazindua  rasmi  tovuti  yake  ambayo  itakuwa  jukwaa  kuu la mawasiliano  na utoaji wa taarifa zake za  club ya   Simba. Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu  tovuti yetu’’. 
AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekeleza ji wa Masokona Biashara wa Simba alisema ‘’Tovuti hii sio tuitaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbalibali pia  itatumika  kwa  ajili  ya uuzaji  wa  vifaa  vya  Simba, Bidhaa  mbalimbali  mpya  na  muhimu  zaidi  kuwaunganisha   wanachama, mashabiki  na wapenzi wa  Simba  kutumia   mitandao  ya  jamii  iliyo   rasmi  ya  Simba Sports Club’’. 
Mkutano   huo  wa  wandishi  wa  habari   ulitumika  kutaarifu   Wanachama, Wapenzina  Vyombo   vya   habari   juu   ya  kocha   mpya   wa   Simba. Alizungumza  wakati  wakumtambulisha   kocha   mpya   wa   Simba, Rais   Aveva   alisema ‘’Baada ya kupitia  vyeti  na  maombi   ya  makocha   mbalimbali, Napenda  kuwa taarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia  kwenye  mkataba  wa   kuifundisha   na   kocha Dylan Kerr raia   wa   Uingereza. Ni kocha   mwenye    uzoefu   wa   zaidi   ya   miaka 30, akiwa  amefanya  kazi  Nchi  mbalimbali  zikiwemo    Uingereza, Scotland, Vietnam   na    AfrikayaKusini’’. 
Aliendelea  kusema ‘’Tunaamini   ujuzi   na   uzoefu wake wa  ukocha na pia kama mchezaji wa kiwango cha juu  utakuwa   chachu   ya   kuifanya   Simba    ifanye    vizuri’’


.
Baraka Da prince ambaye ni mshindi wa tuzo ya msanii bora chipukizi mwaka 2015 kwenye tuzo za KILI, time hii anakuja na collabo atakazo washirikisha wasanii wa Afrika Mashariki, Nigeria na Ghana.
Akizungumza na millardayo.com amesema ‘Kuna nyimbo nyingi zinakuja ambazo nimewashiriki kama Jose Chameleone, Jaguar na msanii kutoka Nigeria lakini siko tayari kumtaja jina lake ila mashabiki wake tayari kwa ujio wangu mpya,kwasasa niko Mwanza kwa wazazi ila mipango yangu ya kuachia single mpya mpaka nikirudi Dar es Salaam baada ya mwezi wa Ramadhani kuisha ndio kila kitu kitakuwa tayari hewani’alisema Baraka.


Droo za Mechi za Raundi ya Kwanza ya Mtoano na ile ya Pili za EUROPA LIGI kwa ajili ya Msimu mpya wa 2015/15 zimefanyika Leo huko Nyon, Uswisi na kuhusisha Klabu 102 ambazo ni nyingi kupita wakati wowote.
West Ham ya England, ambayo ilimaliza Ligi Kuu England ikiwa Nafasi ya 12 na kuingizwa EUROPA LIGI kwa sababu ya kuongoza Tebo ya Uchezaji wa Haki, itacheza na FC Lusitans ya Andorra katika Raundi ya Kwanza ya Mtoano.
Mshindi wa Mechi hii atatinga Raundi ya Pili ya Mtoano na kucheza na Mshindi kati ya Birkirkara FC ya Malta na Ulisses FC ya Armenia.

Klabu 38 zimehusika na Droo hiyo.
RAUNDI YA KWANZA YA MTOANO
Mechi kuchezwa Julai 2 na Marudiano Julai 9

Víkingur Reykjavík (ISL) v NK Koper (Slovenia)
Newtown AFC (WAL) v Valletta FC (MLT)
Glenavon FC (NIR) v FC Shakhtyor Soligorsk (BLR)
NSÍ Runavík (FRO) v Linfield FC (NIR)
FK Atlantas Klaipėda (LTU) v PFC Beroe Stara Zagora (BUL)
FK Spartaks Jūrmala (LVA) v FK Budućnost Podgorica (MNE)
FC Progrès Niederkorn (LUX) v Shamrock Rovers FC (IRL)
Cork City FC (IRL) v KR Reykjavík (ISL)

University College Dublin AFC (IRL)* v F91 Dudelange (LUX)
FC Sheriff (MDA) v Odds BK (NOR)
FC Dinamo Tbilisi (GEO) v Qäbälä FK (AZE)
FC Differdange 03 (LUX) v Bala Town FC (WAL)
Brøndby IF (DEN) v AC Juvenes/Dogana (SMR)
Debreceni VSC (HUN) v FK Sutjeska (MNE)
FK Crvena zvezda (SRB) v FC Kairat Almaty (KAZ)
FC Aktobe (KAZ) v Nõmme Kalju FC (EST)
Go Ahead Eagles (NED)* v Ferencvárosi TC (HUN)
NK Domžale (SVN) v FK Čukarički (SRB)
FK Kukësi (ALB) v FC Torpedo Zhodino (BLR)
KF Renova (MNE) v FC Dacia Chisinau (MDA)
KF Shkëndija (MKD) v Aberdeen FC (SCO)
MTK Budapest (HUN) v FK Vojvodina (SRB)
FC Ordabasy Shymkent (KAZ) v Beitar Jerusalem FC (ISL)
FC Flora Tallinn (EST) v FK Rabotnicki (MKD)
FC Dinamo Batumi (GEO) v AC Omonia (CYP)
FK Trakai (LTU) v HB Tórshavn (FRO)
Glentoran FC (NIR) v MŠK Žilina (SVK)
Alashkert FC (ARM) v Saint Johnstone FC (SCO)
FK Olimpic Sarajevo (BIH) v FC Spartak Trnava (SVK)
Víkingur (FRO) v Rosenborg BK (NOR)
Skonto FC (LVA) v Saint Patrick's Athletic FC (IRL)
Balzan FC (MLT) v FK Željezničar (BIH)
UE Sant Julià (AND) v Randers FC (DEN)
FK Kruoja Pakruojis (LTU) v Jagiellonia Białystok (POL)
KF Laçi (ALB) v İnter Bakı PİK (AZE)
FK Partizani (ALB) v Strømsgodset IF (NOR)
FK Jelgava (LVA) v PFC Litex Lovech (BUL)
FC Lusitans (AND) v West Ham United FC (ENG)*
SJK Seinäjoki (FIN) v FH Hafnarfjördur (ISL)
FC Lahti (FIN) v IF Elfsborg (SWE)
JK Sillamäe Kalev (EST) v HNK Hajduk Split (CRO)
FC Saxan (MDA) v Apollon Limassol FC (CYP)
FC Shirak (ARM) v HŠK Zrinjski (BIH)
VPS Vaasa (FIN) v AIK Solna (SWE)
FK Mladost Podgorica (MNE) v Neftçi PFK (AZE)
NK Celje (SVN) v WKS Śląsk Wrocław (POL)
SP La Fiorita (SMR) v FC Vaduz (LIE)
Birkirkara FC (MLT) v Ulisses FC (ARM)
AUK Broughton FC (WAL) v NK Lokomotiva Zagreb (CRO)
FC Botoşani (ROU) v Tskhinvali (GEO)
Europa FC (GIB) v ŠK Slovan Bratislava (SVK)
Droo za Raundi za Kwanza na za Pili za Mtoano za UEFA CHAMPIONS LIGI kwa Msimu mpya wa 2015/16 imefanyika Mchana huu huko Nyon, Uswisi.
Klabu 38 zimehusika na Droo hiyo.
DROO KAMILI:
Raundi ya Kwanza ya Mtoano:

Lincoln FC (Gibraltar) v FC Santa Coloma (Andorra)
Crusaders FC (Northern Ireland) v FC Levadia Tallinn (Estonia)
FC Pyunik (Armenia) v SS Folgore (San Marino)
B36 Tórshavn (Faroe Islands) v The New Saints FC (Wales)

Mechi kuchezwa Juni 30/Julai 1 na Marudiano Julai 7/8
Raundi ya Pili ya Mtoano:

Hibernians FC (Malta) v Maccabi Tel-Aviv FC (Israel)
APOEL FC (Cyprus) v FK Vardar (Macedonia)
Qarabağ FK (Azerbaijan) v FK Rudar Pljevlja (Montenegro)
FK Sarajevo (Bosnia) v KKS Lech Poznań (Poland)
NK Maribor (Slovenia) v FC Astana (Kazakhstan)
FC BATE Borisov (Belarus) v Dundalk FC (Ireland)
HJK Helsinki (Finland) v FK Ventspils (Latvia)
FC Midtjylland (Denmark) v Lincoln FC (Gibraltar/FC Santa Coloma (Andorra) 

Molde FK (Norway) v FC Pyunik (Armenia)/SS Folgore (San Marino)
Malmö FF (Sweden) v FK Žalgiris Vilnius (Lithuania)
Celtic FC (Scotland) v Stjarnan (Israel)
FK AS Trenčín (Slovakia) v FC Steaua Bucureşti (Roumania)
FK Partizan (Serbia) v FC Dila Gori (Georgia)
PFC Ludogorets Razgrad (Bulgaria) v FC Milsami Orhei (Moldova)
CS Fola Esch (Luxembourg) v GNK Dinamo Zagreb (Croatia)
KF Skënderbeu (Albania) v Crusaders FC (Northern Ireland)/FC Levadia Tallinn (Estonia)
B36 Tórshavn (Faroe Islands)/ The New Saints FC (Wales) v Videoton FC (Hungary)
Mechi kuchezwa Julai 14/15 na Marudiano Julai 21/22
Washindi wa Raundi ya Pili ya Mtoano watasonga Raundi ya Tatu ya Mtoano na itafuatia Raundi ya Mwisho ya Mchujo na kisha Hatua ya Makundi.



Simba SC imeingia mkataba na kocha Dylar Kerr Raua wa England kuifundisha klabu hiyo kongwe nchini ambayo ilimaliza Ligi ikiwa katika nafasi ya tatu.

Kerr atasaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa Simba mkataba ambao una kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kama atafanya vizuri.

Kocha huyo anakuja Simba SC akitokea klabu ya Ligi Kuu ya Vietnam, Hai Phong aliyojiunga nayo Januari mwaka 2014.

Amezaliwa January 14 mwaka 1967 katika kitongoji cha Valletta nchini England

Kerr amewahi kucheza katika ligi kuu ya England hususani vilabu vya Sheffield Wednesday na Leeds United akicheza kama beki wa kushoto.


Kipa wa Chelsea Petr Cech anakaribia kuhamia Arsenal kwa mujibu wa ripoti za kuaminika huko England.
Cech, mwenye Miaka 33, ameshaafikiana maslahi yake binafsi na Arsenal na kilichobaki ni kusawazisha mvutano kati ya Chelsea na Arsenal kuhusu Ada ya Uhamisho huku pande hizo mbili zikikubaliana kuendelea na mazungumzo.
Cech amebakiza Mwaka mmoja katika Mkataba wake na Chelsea na ameruhusiwa rasmi na Mmiliki wa Klabu hiyo, Roman Abramovich, kuhamia Klabu yeyote anayotaka baada ya kusugua Benchi Msimu uliopita akiwa Kipa Namba mbili nyuma ya Thibaut Courtois.

Cech alijiunga na Chelsea Mwaka 2004 akitokea Klabu ya France Rennes na kuidakia Chelsea Mechi 333. Ingawa Cech mwenyewe anapendelea kubakia London na hivyo kujiunga na Arsenal, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho hataki hilo na alipendelea Kipa huyo wa Kimataifa kutoka Czech Republic ahamie kwa Mabingwa wa France Paris Saint-Germain.
Lakini Karata ya Trufu ya Mmiliki Roman Abramovich ndiyo imemtoa kapa Jose Mourinho na kumpa mtaji Kipa Mkongwe Petr Cech.

England, wakicheza Mechi yao ya pili ya Fainali za Mashindano ya Mataifa ya Ulaya kwa Vijana chini ya Miaka 21, EURO U-21, Leo wameifunga Sweden 1-0 huko Ander Stadium, Olomouc Nchini Czech Republic. 

Katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi B England walifungwa 1-0 na Portugal lakini Leo mkombozi wao alikuwa Jesse Lingard, Chipukizi wa Manchester United, alieingizwa Dakika ya 55 kumbadili Pritchard na kufunga Bao pekee na la ushindi kwa Shuti kali kufuatia Kona.
England watamaliza Mechi yao ya mwisho ya Kundi C kwa kucheza na Italy hapoKikosi cha Timu ya England U21Kikosi kikiomba kabla ya MtanangeHarry Kane akiachia shuti kaliJesse Lingard kwenye mbio kuukimbiza mpira
Jesse Lingard akifunga bao
Kwenye raha za kupata baoWakimpongeza mwenzao



Kipa wa Manchester United David de Gea amewaambia wachezaji wenzake katika kilabu hiyo ya Old Trafford kwamba anataka kuihama kilabu hiyo na kujiunga na Real Madrid.
Kulingana na gazeti la mail online,hatma ya kipa huyo katika klabu ya Manchester United haijulikani huku Madrid ikiwa na hamu ya kumsajili kipa huyo aliyeisaidia manchester United kupanda hadi nafasi ya nne.

Raia huyo wa Uhispania amewaambia wenzake kwamba anataka kurudi katika klabu ya Madrid kabla ya kuanza kwa msimu ujao.


Arsenal itapuuzilia mbali hamu ya Manchester City ya kutaka kumsajili kiungo wake wa kati Jack Wilshere kwa kumpatia mkataba mwengine wa miaka mitano pamoja na kuongeza mshahara wake mara mbili ya anavyopata.
Kulingana na gazeti la the Mirror, Manchester City ambayo ilishindwa kutetea taji lake la ligi msimu uliopita ina hamu ya kuimarisha safu yake ya kati kwa kununua wachezaji wa Uingereza katika uwanja wa Etihad na Wilshere ni miongoni mwa wachezaji inaowalenga pamoja na Raheem Sterling wa Liverpool na Fabian Delph wa Aston Villa.
Lakini the Gunners wako tayari kumzuia Wilshere mwenye umri wa miaka 23 ambaye amekuwa kiungo muhimu cha timu hiyo na taifa lake.

Baada ya kukaa nje kwa miaka miwili na jeraha,Wilshere ameonyesha kwamba yuko imara kwa mara nyengine tena baada ya kuifungia Uingereza mabao 2 dhidi ya Slovenia katika mechi ya kufuzu kwa michuano ya Ulaya.
Iwapo Manchester City itashindwa kumpata Wilshere basi Sterling atakuwa windo lake.
Lakini Arsenal inajua hatari ya kumkosa mchezaji huyo na tayari imeanza mazungumzo ya kumpatia mkataba mpya.
Wilshere bado ana miaka mitatu ya mkataba wake katika uwanja wa Emirates lakini Arsenal iko tayari kuimarisha malipo yake na kufikia pauni 100,000 kwa wiki ili kuhakikisha kuwa anasalia.


Hii Ndio Ratiba ya Bongo Star Search 2015 ... Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam. ‪#‎JukwaaNiLako‬ ‪#‎KuwaOriginal‬ Save The Date!
 

 Share artwork hii kwenye page yako ukiambatanisha na hashtag hii #JukwaaNiLako
Mwenye LIKES nyingi zaidi atajishindia zawadi mbalimbali kutoka Bongo Star Search. Mshindi atatangazwa siku ya Jumatano. ‪#‎BSS2015‬


Hii ndio ratiba ya Bongo Star Search 2015 ... Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam. Follow BSS2015 Twitter @BstarSearch | Instagram @BongoStarSearch | Facebook www.fa


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;

1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

waliotembelea blog