Monday, February 10, 2014

 

 

 







apigwa_ad02a.jpg
Mchumi wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Shadrack Mwanjuguja akidhibitiwa na vijana baada ya kutokea vurugu jana asubuhi katika Kijiji cha Ruanda2 wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Santilya, Mbeya Vijijini. Picha ndogo ni Mkuu wa Polisi Kituo cha Kati, Mbeya, Richard Mchomvu akimsindikiza hospitali Mbunge wa Mbeya Vijijini (CCM), Mchungaji Lackson Mwanjale baada ya kujeruhiwa katika kata hiyo. 
Mikoani. Wabunge wawili, mmoja wa CCM na mwingine wa Chadema, jana walikula vichapo walipokuwa katika harakati za uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika katika kata 27 nchini.
Wabunge hao, Godbless Lema (Chadema) wa Arusha na Mchungaji Jackson Mwanjele wa Mbeya Vijijini walipata vipigo katika matukio tofauti yanayohusiana na uchaguzi huo.
Lema alidai kuwa alinusurika kifo kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa polisi na ilibidi aanguke chini na kujifanya amezirai ili kujiokoa, katika tukio lililotokea jana jioni, eneo la Shule ya Sombetini alipokuwa akielekea katika kituo cha kupigia kura.
Mara baada ya kufika jirani na kituo cha Sombetini, inadaiwa kuwa polisi walisimamisha gari ya Lema na kuanza kumuhoji lakini ghafla ilitokea kutoelewana kipigo kuanza. Katika tukio hilo, Lema alipata kipigo hadi kuangukia katika mfereji na akiwa chini, alionekana kama amezimia hivyo polisi walimuachia na kuokolewa na wafuasi wa Chadema.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Lema alisema bila kujifanya amezirai angeweza kuuawa... "Wamenipiga sijui kosa langu, mimi kama mbunge niliitwa na mawakala wakiomba gari kubeba masanduku na ni kweli nilikuwa nimewasha taa za gari nikishangilia. Kesho naenda kupimwa hospitali kwani nina maumivu kwenye mbavu. Baada ya hapo nitajua cha kufanya kwani walionipiga nawajua."
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana jana kuelezea tukio hilo lakini mmoja wa polisi waliokuwa eneo la vurugu hizo, alisema walilazimika kimdhibiti Lema, kwani alikuwa anafanya fujo jirani na kituo cha kura.
"Hakuna aliyempiga, alianguka mwenyewe kwenye mfereji, tulimtaka aondoke kwa amani akagoma," alisema askari huyo.
Mbeya Vijijini
Mchungaji Mwanjale kwa upande wake, aliumizwa baada ya kupigwa na kundi linalodaiwa kuwa la wafuasi wa Chadema, katika Kitongoji cha Shipongo, Kijiji cha Ruanda, Mbeya wakati yeye na makada wengine wa CCM walipofika hapo wakiwa kwenye gari la chama hicho.
Mbunge huyo alivuja damu nyingi kichwani na mashuhuda wa tukio hilo walisema kabla ya kupigwa, kulikuwa patashika baina ya walinzi wa CCM na wale wa Chadema waliokuwa wakilinda kura katika uchaguzi huo.
Mchungaji Mwanjale inaelezwa kuwa alijiokoa baada ya vijana hao walipomwacha na kuanza kumshambulia Mchumi wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Shadrack Mwanjuguja ambaye alikuwa amefuatana naye.
Baada ya kuponyoka, Mwanjale alikimbilia kwenye nyumba moja iliyopo karibu na vijana hao walimfuata na kugonga kwa nguvu ili waingie ndani, lakini alitoroka kupitia mlango wa nyuma kisha kuruka uzio wa nyumba hiyo huku Mwanjuguja akiwekwa chini ya ulinzi.
Mbunge huyo na mwenzake waliokolewa na polisi wa doria waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) Mbeya, Richard Mchomvu ambaye aliwachukua na kuwapeleka Kituo cha Afya Kilembo kwa ajili ya matibabu.
Daktari wa kituo hicho, Franco Anthony alisema Mchungaji Mwanjale alipigwa na kitu kizito kichwani na kushonwa nyuzi tatu huku mwenzake Mwanjuguja akishonwa nyuzi mbili kichwani.
Baada ya kupata matibabu walikwenda Kituo cha Polisi Mbalizi kufungua jalada la mashtaka. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema watu saba walikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.
Vurugu Bagamoyo
Vurugu ziliibuka katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Magomeni, Bagamoyo na kusababisha polisi kutumia mabomu ya machozi baada ya watu wanaodhaniwa ni wafuasi wa vyama vya CUF na Chadema kuwashambulia wa CCM.
Katika vurugu hizo zilizotokea saa mbili asubuhi, inadaiwa zaidi ya wafuasi 15 wa CCM walijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kuwa watu kadhaa walikamatwa huku polisi wakiendelea na uchunguzi.
Lindi
Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Namikago, Wilaya ya Nachingwea, Valery Kwembe alimtangaza Alferd Mhagama wa CCM kuwa mshindi kwa kura 511 dhidi ya Hamisi Chingole wa Chadema (188), Hamis Malipiche wa CUF (110) na Belisimas Mbinga wa ADC (1).
Katika Kata ya Kiwalala CCM imeibuka mshindi baada ya Sheneni Zahoro kupata kura 1,158 akifuatiwa na wa CUF, Shazil Mosha 803 na Mboga Hassan wa Chadema 90.
Moshi
Katika Kata ya Kiborloni, Moshi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Erasmo Silayo alimtangaza Frank Kagoma wa Chadema kuwa mshindi kwa kupata kura 1,019 dhidi ya 255 za Willy Tulli wa CCM. Mgombea wa UDP, Aidan Mzava aliambulia kura mbili. chanzo MWANANCHI

Soka | Hispania

Gerardo Martino na Lionel Messi 



Barcelona kocha Gerardo Martino alisema Lionel Messi alikuwa akajibu wapinzani wake kwa njia nzuri iwezekanavyo kama Argentina alifunga mabao yake mawili ya kwanza kutoka kucheza wazi katika 10 ligi kuu ya Uingereza kama Barca alishinda 4-1 katika Sevilla siku ya Jumapili.
Sevilla walikuwa wamekwenda mbele mapema juu ya chini ya mvua kubwa katika Sanchez Pizjuan, lakini Messi kuongozwa ufufuo upande wa wake kama yeye kwanza walivuka kwa Alexis Sanchez kwa kifungu nyumbani kusawazisha kabla ya kumaliza mbali faini kukabiliana na mashambulizi kwa stunning nusu-volley tu kabla ya mapumziko .
nne wakati World Mchezaji wa Mwaka mara mbili Tally yake kwa jioni na kumaliza nyingine tamu kutoka kupita Andres Iniesta ya dakika 11 baada ya mapumziko na Cesc Fabregas mviringo mbali bao dakika tatu kutoka wakati.
Messi alikuwa maswali kwa maskini goalscoring aina yake tangu kurudi kutokana na kuumia hamstring mwanzoni mwa mwaka, lakini Martino alisisitiza kuwa mara tu suala la muda kabla ya kurudi kuunda mbele ya lengo.
"Mimi siku zote kusema sawa na heshima kwa Leo. Mimi kamwe kukimbia hatari ya kwenda juu juu pamoja naye.
"Wale wanaofanya kusema kitu hasi juu yake wakati mwingine wala kutambua nini wanachokifanya kuathiri kiburi chake, na wakati wa kufanya hivyo kwa mchezaji bora katika dunia, hii ni nini kinatokea."
Ushindi wakiongozwa Barca nyuma juu ya La Liga kwa tofauti ya mabao juu ya Real Madrid na Atletico Madrid kwa pande zote tatu amefungwa juu ya pointi 57.
Catalans alikuwa kuanza mwishoni mwa wiki mbali nafasi ya juu kwa mara ya kwanza katika ligi mechi 59 zifuatazo mshtuko 3-2 kushindwa nyumbani kwa Valencia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Na Martino ni kuamua si kwa mkono faida kwa jina wapinzani wao tena katika 15 ligi kuu ya Uingereza kwamba bado.
"Kwa kuwa nafasi ya kuokoa na kurejesha kuongoza wiki moja tu baada ya kupoteza ni kumtuliza.
"Sisi kuanza tena sasa na tutaona ambayo ya timu tatu kufanya makosa ya kwanza. Ni matumaini yetu itakuwa si sisi tena."
mchezo pia alikuwa mashuhuri kwa Iniesta kurudi fomu.
Si Spanish kimataifa alikuwa alicheza dakika 90 tangu kushinda 4-0 juu ya Elche juu ya Januari 5, lakini mara bila shaka upande wake bora utendaji katika kiungo kama wao zinalipwa kudhibiti baada ya ufunguzi ngumu.
Hata hivyo, pamoja na mchango wake mwenyewe, Iniesta pia alikuwa na nia ya kumsifu tofauti yaliyotolewa na Messi.
"Leo kamwe huenda kukosa, yeye ni mmoja wa wachezaji wachache katika dunia ambayo katika sekunde chache au katika mita chache unaweza kugeuka mchezo anafanya hivyo wakati wote na alifanya hivyo tena leo.," Aliiambia Kihispania kituo cha TV Mfereji Plus.
"Ni muhimu kwa kushinda leo na kurudi juu ya meza. Tulipoteza uongozi wiki iliyopita na ni vizuri kurudi hivyo haraka. Hali walikuwa si bora lakini sisi imeweza kuchukua pointi tatu.
"Usawa kati ya timu zote ni nzuri kwa ajili ya kila mtu. Sisi kuona nini kinatokea kuja mwisho wa msimu."

tff-july5-20131 aee39
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lipo mbioni kujenga vituo 169 vya michezo katika wilaya 169 za Tanzania.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kuwa licha ya vituo hivyo kufundisha soka pia ni maalumu kwa ajili ya kufundisha vijana juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya.
Hivi karibuni Malinzi alizindua kampeni ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru, ambayo inaratibiwa na Taasisi ya African Inside Out wakati TFF ni washiriki wakuu.
"Katika hili kupitia idara yetu ya ufundi, tupo mbioni kufanya sensa ya vituo vya kukuza na kulea vipaji vya vijana pamoja na vituo vya mpira nchini kote. Utaratibu huu unafanywa kwa kuwekwa vigezo vya kutambuliwa vituo hivyo na TFF itaweka utaratibu wa kusajili na kutoa vyeti vya usajili kwa kituo kitakachokidhi vigezo.
Malinzi alisema kuwa lengo ni kuweka utaratibu nchini wa kusimamia na kuendeleza vituo hivi kitaifa na kwamba ili Tanzania ifundishe mpira unaofanana nchi nzima wanaandaa utaratibu wa kuandaa mitalaa
ya kufundisha mpira.

Alisema mtalaa huo unaandaliwa na idara ya ufundi ya TFF kwa kusaidiana na mtaalamu wa mpira kutoka Uholanzi na kudai kuwa mtalaa huo ukikamilika utakuwa nyezo muhimu ya kufundishia mpira shuleni na kwenye vituo vya kuendeleza soka.
Katika hatua nyingine Malinzi alisema uongozi wake pia umeandaa mpango wa kukutana na wenyeviti wa vyama vya tiba, waamuzi na makocha ili kupanga mikakati ya maendeleo ya kitaaluma.
"Mikakati hii ambayo itajumuishwa katika mpango mama wa maendeleo wa TFF, maandalizi yake yatakamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa." Chanzo: mwananchi
130219091727 arsene wenger 304x171 d nocredit1 ed074
Kocha wa Arsenal, Arsena Wenger, amesisitiza kuwa ''The Gunners'' bado wana uwezo wa kushinda ligi kuu ya Premier msimu huu, lakini amekiri kipigo walichopata katika uwanja wa Anfeild, kimezua maswali kuhusu kikosi chake.
Kabla ya mechi ya Jumamosi Arsenal, ilikuwa katika nafasi ya kwa lakini hakuna aliyetarajiwa kuwa vijana hao wa Wenger watalimwa magoli matano kwa moja.
Wenger anakabiliwa na klibarua kigumu kubadili mtindo huo pale Arsenal itakapocheza na Manchester United siku ya Jumatano katika uwanja wa Emirates.
''Kipigo tulichopewa, kimezua maswali mengi ambayo tunastahili kuyajibu siku ya Jumatano usiku. Naamini bado tunauwezo wa kushinda ligi kuu kwa sababu ukipiga hesabu, inawezekana'' alisema Wenger.
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha dakika ishirini, Arsenal ilikuwa imelazwa magoli manne bila jibu.
Licha ya kurejea kwa mcheza kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, ambaye alikuwa akiuguza jeraha, Arsenal haikuonyesha mchezo wake wa kawaida.
Martin Skrtel, Raheem Sterling na Daniel Sturridge ndio walioifungia Liverpool, huku Mikel Arteta akiipa Arsenal bao lake la kuvutia machozi.
Baada ya kuchuana na Manchester United siku ya Jumatano, Arsenal, itacheza tena na Liverpool katika raundi ya tano ya kuwania kombe la FA kabla ya kutoana jasho na miamba wa Ujerumani Bayern Munich katika mechi ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya. Chanzo: bbcswahili

waliotembelea blog