Saturday, October 12, 2013

VODACOM PREMIER LEAGUE: LIVE MATCH - KAGERA SUGAR 1 vs YANGA 2, ..Second Half!


Kikosi cha Kagaera Sugar kilichoanza

Kikosi cha Yanga

Waamuzi wa mtanange huu

Waamuzi na Timu Kapteni wakiteta jambo muda mfupi kabla ya mpira kuanza

Benchi la Yanga kushoto ni Kocha mkuu

Benchi la Kagera Sugar

Dakika ya 2 Mpira ukirushwa kama kona na Kipa kuupangulia kwa adui na Hatimaye Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa akafanikiwa kuipatia bao na hapa walikuwa wanashangilia bao hilo. Mpaka Mapunziko Yanga ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar. Habari na www.bukobasports.com

wachezaji wa yanga wakishangilia ushindi

  Yanga wanapofunga kufurahia  goli
  Ushindi..jamani..

  Ngassa


washabiki wa bk
 Tanzania ikitajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zenye amani na utulivu, imebainika kuwa Watanzania ni miongoni mwa watu wasio na furaha na waliokata tamaa hapa duniani.
Ripoti inayoonyesha orodha ya nchi zenye furaha duniani ya mwaka 2013 (World Happiness Report 2013), imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kati ya nchi 156 zilizofanyiwa utafiti huo.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na kundi la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa (UN), kati ya mwaka 2010 na 2012, inaonyesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 151 ikiburuta mkia pamoja na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Benin na Togo.
Upatikanaji wa huduma za jamii, mtazamo wa watu kuhusu rushwa, umri wa kuishi, ukosefu wa kazi, pato la taifa na ukarimu wa watu katika nchi husika, ni baadhi ya vigezo vilivyoangaliwa wakati wa kuandaa taarifa hiyo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alieleza kushtushwa na ripoti hiyo kwa maelezo kwamba ni asilimia 11.7 tu ya Watanzania wasio na ajira na kwamba wale wanaofanya kazi, wanapata huduma zote za msingi, ikiwa ni pamoja na kwenda likizo na mishahara inayolingana na taaluma zao.
“Watanzania wana furaha, kwa upande wa wafanyakazi wanapata haki zao zote wanazostahili, sijui ni vigezo vipi wametumia…kwa mujibu wa takwimu za 2006 ni asilimia 11.7 ya Watanzania ndio waliokuwa hawana kazi, lakini wakati huo idadi ya watu ilikuwa ndogo, hivi sasa imeongezeka,” alisema Kabaka na kuongeza:“Usafiri ndiyo tatizo linalowasumbua wafanyakazi wengi kwa kuwa wanachelewa kwenda kazini.”
Naye, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Salum alisema pamoja na vigezo vingine vilivyotumika kutambua furaha ya Watanzania, umaskini ndiyo unaoweza kuwa chanzo cha Tanzania kushika nafasi za mwisho.
“Inategemea na vigezo vingine walivyovitumia, nakubali kuwa Tanzania ni maskini pengine hali hiyo imeifanya nchi kushika nafasi ya mwisho,” alisema Salum.
Nchi zilizoongoza
Taarifa hiyo imezitaja nchi tano; Denmark, Norway, Uswisi, Netherlands na Sweden kuwa ndizo zinazoongoza kwa watu wake kuwa na furaha zaidi duniani, huku Angola ikishika nafasi ya kwanza Afrika na ya 61 duniani ikifuatiwa na Algeria (73), Libya (78), Ghana (86), Zambia (91), Lesotho (98), Morocco (99) na Swaziland (100).
Kwa upande wa Afrika Mashariki, wananchi wa Uganda ndio walionekana kuwa na furaha zaidi kwani nchi hiyo imeshika nafasi ya 120 wakifuatiwa na Kenya (123), Tanzania (151), Rwanda (152) na Burundi (153).
Ripoti hiyo inabainisha kuwa kati ya mwaka 2005 na 2012, nchi 60 duniani ziliongeza viwango vya furaha kwa watu wake, kati ya hizo 16 zikiwa barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

 Wahamiaji haramu 16 kutoka nchini somalia wamekamatwa Mkoani morogoro wakiwa wamejificha  katika  lori la mizigo lililosheni chokaa  likitokea jijini dar es salaam kuelekea mkoani mbeya
Kupatikana kwa wahamiaji haramu hao kunatokana na ushirikiano wa  wananchi  ambao umesaidia kukamatwa kwa wahamiaji hao huku wakidai kuwa baadhi yao walikosa hewa kufuatia kujificha katika mizigo hiyo
 Kwa upande wake afisa uhamiaji mkoa wa Morogoro Hamprey Minja amesema kuwa dereva wa gari hilo amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo amesema kuwa  vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti kwa kiasi kikubwa maeneo ya mipaka kwa ajili ya kudhibiti matukio ya wahamiaji haramu hali inayopelekea wahamiaji hao kutumia njia nyingine ikiwemo ya kujificha katika magari ya mizigo
 Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewaweka chini ya ulinzi wahamiaji hao ikifanya taratibu za kuwafikisha mahakamani kujibu mashtaka ya kuingia nchini bila kibali
Nick Cannon na Kim Kardashian



Tupac Shakur na Jada Pinkett
Kati ya zote hawa ndo waliyoniacha hoi!!

Rihanna na Lewis Hamillton aliyekuwa mpenzi wa mda mrefu wa Nicole Schezinger


Eddie Murphy na Toni Braxton 



Tyra Banks na Will Smith



Nilipigwa a butwaa baada ya kugundua kuwa wasanii hawa walikuwa wapenzi hapo awali, unadhani wanamatch? Toa maoni yako hapa....


waliotembelea blog