Wednesday, July 29, 2015


Manchester United wameshindwa kutetea Taji lao la International Champions Cup baada ya kufungwa 2-0 na Paris Saint-Germain kwenye Mechi yao ya mwisho Usiku wa kuamkia Leo huko Soldier Field, Chicago, USA na kuiacha PSG ikibeba Kombe hilo.PSG walifunga Bao lao la kwanza katika Dakika ya 25 baada Mpira mrefu kutoka kwa Silva kumkuta Kipa David De Gea akiwa nafasi ovyo na Blaise Matuidi kuutokea na kufunga.Dakika 9 baada PSG walifunga Bao la Pili kupitia kupitia Straika wao hatari Zlatan Ibrahimovic aliepokea pasi kutoka kwa Lucas Moura na kumpa Maxwell alietumbukiza Krosi ndani ya boksi na kuunganishwa wavuni na Ibrahimovic.
Hadi Mapumziko PSG 2 Man United 0.
Mechi hii ilikuwa ni mechi ya 4 na ya mwisho kwa Man United wakiwa Ziarani huko USA na walishinda mechi zao 3 za awali kwa kuziangusha Club America ya Mexico (1-0), San Jose Earthquakes ya USA (3-1) na Barcelona (3-1).Katika mchezo huo kukaba ndio ilikuwa nguzo!!
Zlatan Ibra
Michael CarrickDepayNdani ya Uwanja wa Soldier Field, Chicago, United States
Manchester United  mpaka sasa hajapata bao, Paris Saint-Germain wanaongoza bao 2-0 zilizofungwa kipindi cha kwanza dakika ya 25 na Blaise Matuidi na lilie la dakika ya 34 na  Zlatan Ibrahimovic.


SamattaMbwana Samatta ni mshambuliaji wa kimataifa kutokea Tanzania anaeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo alijiunga nayo mwaka 2011 akitokea Simba ya Tanzania na mpaka sasa amekua mmoja kati ya wachezaji mahiri wanaounda safu imara ya ushambuliaji kwa TP Mazembe na timu ya taifa ya Tanzania.
samataSamatta aliingia kwenye headlines siku kadhaa zilizopita baada ya kukataa kusajiliwa na klabu ya Zamalek ya Misri kwa euro milioni 1 kutoka TP Mazembe ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 2.3 za Kitanzania, kila media iliandika hii story nakuonekana kama Samatta amepoteza bahati.
Wakala wa mchezaji huyo Jamal Kasongo amezungumzia suala hilo na mpango wa Samatta licha ya kupewa ofa ya mshahara mkubwa.
Mbwana-2 
“La kwanza ni kweli maafisa wa Zamalek wawili walifika kipindi mimi nipo na Mbwana kipindi yupo katika mechi ya timu ya taifa kimsingi mimi niliweza kukaa nao chini kuweza kufanya nao majadiliano lakini lazima mchezaji ili ufikie malengo uweze kukaa katika mstari, msimamo wa Mbwana na msimamo wangu mimi kama mshauri wake ni Mbwana kuweza kucheza Ulaya”>>>Jamal Kasongo
MbwanaSamata-inaction120712BBP300“Wakatuma tena ofa wako tayari kumnunua TP Mazembe kwa euro milioni 1 na euro milioni 1 ni pesa nyingi na walikuwa tayari wakimuhitaji waweze kumpa mshahara ambao hakuna mchezaji ndani ya Afrika hii anaweza akalipwa lakini bado hili suala lilikuwa gumu kwani lengo kubwa ni Mbwana kucheza Ulaya”>>>Jamal Kasongo
NYASI za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho zitakanyagika kwa mchezo wa miamba ya Jiji, Azam FC na Yanga SC katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Itakuwa mara ya pili, Yanga SC na Azam FC kukutana katika Kombe la Kagame, baada ya mwaka 2012 kukutana katika fainali pale pale Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
Ilikuwa Julai 28, mwaka 2012 katika mchezo uliochezeshwa na refa Thierry Nkurunziza wa Burundi, Yanga SC ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 wafungaji Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 44 na Said Bahanunzi ‘Spider Man’ dakika ya 90 na ushei.
Mabeki wanaoweza kucheza kama viungo pia, Shomary Kapombe wa Azam FC (kulia) na Mbuyu Twite wa Yanga SC (kushoto) wakigombea mpira katika mchezo uliopita uliozikutanisha timu hizo katika Ligi Kuu. 

Iwapo dakika 90 za mchezo zitamalizika kwa sare yoyote, sharia ya mikwaju ya penaltI itachukua nafasi moja kwa moja.
Hadi kufika hatua hii, Azam FC haijafungwa hata bao moja- maana yake ni timu yenye ukuta imara zaidi katika mashindano haya hadi sasa.
Katika mechi za makundi, Yanga SC ilibahatika kupata jumla ya penalti tatu katika mechi mbili na kwa bahati mbaya, walikosa zote. 
Ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 mbele ya Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa kwanza wa Kundi A, Yanga ilipewa penalti dakika za lala salama, lakini Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akaenda kukosa.
Katika mchezo wa pili wa kundi hilo dhidi ya Telecom ya Djibouti, Yanga SC walikosa penalti mbili mfululizo, ya kwanza Amisi Tambwe na ya pili Simon Msuva zote kipindi cha kwanza. Yanga ilishinda 3-0.
Cannavaro, Tambwe na Msuva ni wachezaji wanaoaminiwa zaidi Yanga SC kwa kupiga mikwaju ya penalti, lakini kwa kushindwa kufunga kwenye mechi za makundi, maana yake hali ya kujiamini kwao binafasi imepungua.
Je, tutarajie nini iwapo mchezo utamalizika kwa sare na penalti zikapewa nafasi ya kuamua mshindi? Kesho si mbali, zimebaki saa kadhaa tu. Tuombe uzima ‘Inshaallah’. 



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya hotel ya Bahari Beach jijini Dar,kwenye mkutano wa Wanahabari jioni ya leo.

Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.

Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa (mwenye umvi) akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.

Mh.Edward Lowassa akiwa katika hadhara ya mamia kujibu maswali katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .

Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya kutangaza rasmi azma yake ya kujiunga na ukawa.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.

waliotembelea blog