Sunday, May 31, 2015



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia) nao wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.

Kundi la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.


Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bibi Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano

Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano

Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano

Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (katikati) kwa pamoja na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu Bw. Macdonald Mwakasendile (kushoto) wakirekodi matukio

Rais Kikwete akifuraia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Zuma pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Museveni mara baada ya kumaliza mkutano.

Rais Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bi.Nkoosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiongozana na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta tayari kwenda kuanza mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi .

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,, Bw. Vervaeke.
....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta




Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyetta akipita kwenye Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili nchini



Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya kumpokea Rais huyo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Rais Museven akipita katikati ya Gwaride la heshima.

Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili nchini

Picha ya Pamoja baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Reginald Philip


Mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa ametangaza rasmi nia ya kuwania urais wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi mbele ya umati wa watu waliofurika uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha na kutaja vipaumbele vyake kuwa ni elimu,kupambana na umaskini,kulinda rasilimali za nchi  na kuwaunganisha watanzania .
Mh.Lowassa ambaye aliingia.uwanjani akisindikizwa na msafara wa pikipiki na magari pia  amesema akipewa fursa atahakikisha  anadumisha muungano.
Amesema ataweka misingi imara ya kuharakisha maendeleo mazuri kwa wananchi  na kuwawezesha vijana kuondoa tabaka la walionacho nawasionacho.
Awali viongozi wa dini na siasa akiwemo Kkingunge Ngombale Mmwiru wameseama Lowassa ana sifa za kiongozi anayefaa kuliongoza  taifa  kwa sasa.
Sherehe hizo zilizohudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka kona mblimbli  nchini burudani kubwa  ilikuwa  ni  Helkopta ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Bw. Joseph Msukuma.
Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Nyomi ya watu waliofurika uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha
Taswira mbalimbali katika picha
 Pichani kulia kabisa anaonekana Mh.Nazir Kalamage
Watu katika hali ya usikivu
Dua kutoka kwa Sheikh
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
Umati mkubwa wa watu
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
Kkingunge Ngombale Mmwiru

 Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa wakati wa mkutano uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
 Mama Regina Lowassa pichani
 Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya Wabunge waliohudhulia mkutano huo, baada hotuba yake. Picha zote kwa hisani ya Othman Michuzi
Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
CREDIT PHOTO:Othman Michuzi

waliotembelea blog