Saturday, October 31, 2015


KIVUMBI cha Ligi Kuu Tanzania Bara, kinaendelea tena leo kwenye viwanja vitano tofauti, huku miamba ya soka Yanga na Simba ikirejea tena kusaka pointi tatu. Yanga ambayo kabla ya mechi ya Jumatano iliyotoka sare ya mabao 2-2 na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage Shinyanga ilikuwa na pointi 19 sawa na Azam FC ikiongoza ligi hiyo, ilijikuta ikipata matokeo hayo ambayo yaliwapa majonzi mashabiki wao.
Majonzi hayo yaliongezeka zaidi Alhamisi baada ya Azam kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, hivyo Azam kuipiku Yanga kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 22 ikiiacha Yanga nafasi ya pili na pointi zake 20.
Kutokana na hali hiyo, leo Yanga itashuka Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora kuivaa Kagera Sugar, ikiwa na dhamira moja ya kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo. Kama Yanga ikishinda leo itafikisha pointi 23 na itaombea Azam FC ambayo kesho itacheza na Toto Africans Uwanja wa Azam Chamazi ipate matokeo mabovu.
Yanga inapewa nafasi ya kushinda leo kutokana na mwenendo mbaya wa wenyeji wao Kagera Sugar, ambao tangu kuanza msimu huu wameshinda mchezo mmoja na kupoteza mitano kati ya tisa waliyocheza.
Leo utakuwa mtihani wa pili kwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mohammed Adolf Rishard, tangu akabidhiwe timu akirithi mikoba ya Mbwana Makatta aliyeachia ngazi kutokana na matokeo mabaya. Ni wazi Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm naye ataingia uwanjani kuhakikisha vijana wake wanaibuka na ushindi ili kuwapa furaha mashabiki wao.
Hata hivyo pamoja na mwanzo mbaya wa Kagera Sugar, lakini timu hiyo inaweza kuzinduka na kufanya maajabu kwa kuifunga Yanga, kwani inakikosi bora cha wachezaji waliodumu kwa muda mrefu na timu hiyo akiwemo nahodha wake George Kavila na Paul Ngwai.
Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikizidi kujivunia safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Mzimbabwe, Donald Ngoma mwenye mabao saba na Amissi Tambwe ambao wamekuwa wakipambana kuhakikisha timu yao inafanya vizuri kwa kufunga mabao mengi.
Kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba inawakaribisha Majimaji ya Songea huku kocha wake Dylan Kerr, akijivunia ushindi wa bao 1-0, walioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga na timu hiyo kufikisha pointi 18 na kupanda hadi nafasi ya nne.
Mshambuliaji Hamisi Kiiza amekuwa tegemeo kwa kocha Kerr, katika upande wa mabao baada ya kufunga bao lake la sita Jumatano iliyopita ukiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu kurejea uwanjani baada ya kukosa mechi tatu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Pamoja na kuonesha kiwango cha chini kwenye mchezo uliopita, lakini Simba wanapewa nafasi ya kushinda mchezo wa leo kutokana na udhaifu wa wapinzani wao Majimaji waliopo nafasi ya 10 wakiwa na pointi 11.
Rekodi zinaonesha Majimaji imekuwa hatari msimu huu inapocheza nyumbani uwanja wa Majimaji Songea, lakini mambo huwa tofauti inapokuwa ugenini na takwimu zinaonesha imepoteza mchezo mmoja nyumbani na kushinda mitatu, huku ikifungwa michezo mitatu na miwili ikitoka sare.
Mechi nyingine za leo, Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo, itakuwa nyumbani Uwanja wa Manungu kucheza na Mwadui FC ya Shinyanga na Prisons itakuwa nyumbani Uwanja wa Sokoine kuchuana na Ndanda FC ya Mtwara na Coastal Union itakuwa Uwanja wa Mkwakwani ikicheza na Mbeya City.

LIONEL MESSI WENDA AKAIKACHA SPAIN, KWENYE MIKAKATI YA KUJIFUNZA LUGHA YA KIINGEREZA! CRISTIANO RONALDO NAE YALE YALE...MAN UNITED, PSG KWENYE SAHANI MOJA ZIKIMHITAJI!

MCHAMBUZI wa kuheshimika wa Soka la Spain amedokeza kuwa Mastaa wakubwa Nchini humo, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, wako mbioni kutimka na ipo nafasi kubwa kwao kutua Ligi Kuu England.
Akiongea na Jarida la talkSPORT, Guillem Balague, Mwandishi na ambae pia ni Mchambuzi wa Sky Sports' kwenye Shoo yao Revista de la Liga, amesema upo mkakati kwa Ronaldo kuihama Real mwishoni mwa Msimu huu lakini si kurudi Manchester United bali kwenda Paris Saint-Germain.
Licha ya mwenyewe Ronaldo, mwenye Miaka 30, kutoboa hivi karibuni kuwa atastaafu akiwa na Real, Balague amekiri Ronaldo anaihusudu Man United lakini ipo dili ya yeye kuhamia PSG.
Balague ameeleza: “Ataondoka Real. Upo mkakati toka Watu wake kuondoka mwishoni mwa Msimu na PSG wanazo pesa na Real wako tayari kumwachia. Ronaldo anaihusudu Man United .. Mashabiki, hali ilivyo Old Trafford na Klabu, lakini sasa Klabu ipo kwingine. Je Man United watalipa Euro Milioni 125 pamoja na kumlipa yeye Milioni 20 kila Mwaka wakati huu? Kwanini watumie pesa hizo?”
Wakati huo huo, Guillem Balague pia ametoboa kuwa Lionel Messi sasa anajifunza Kiingereza kwa ajili ya uwezekano wa kuhamia Ligi Kuu England.
Messi, mwenye Miaka 28, amekuwa akihusishwa na kuhamia Chelsea, Manchester United na Manchester City hasa kwa vile hana raha huko Barcelona hasa baada ya kuandamwa na Kesi ya Ukwepaji Kodi Mahakamani Nchini Spain.
Balague ameeleza: “Bado hajaamua kuhamia, anafikiria kuhusu hilo. Ameshasikia kutoka Sergio Aguero na Cesc Fabregas jinsi England ilivyokuwa nzuri. Kuna mvuto wa changamoto mpya. Sasa Messi anakomaa na pia hufuatilia Ligi Kuu England. Sasa anajifunza Kiingereza akijitayarisha na Uhamisho.”
Balague amesisitiza mara kadhaa Klabu kubwa za Ulaya zimejaribu kumnunua Messi huko nyuma zikiwemo Mahasimu wa Barca, Real Madrid, na hata Arsenal.


Mchambuzi huyo amefafanua: “Wakati ule dili za kuhama Gerard Pique na Cesc Fabregas zilipokubaliwa [Pique kwenda Man United na Fabregas kwenda Arsenal] Watatu hao walikuwa Timu moja na Messi pia alifuatwa kuhamia Timu ya Wenger..Arsenal!”
Maisha yake yote ya Soka Messi amekuwa na Barcelona na kutwaa Mataji makubwa 25 pamoja na Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon d’Or, mara 4 ingawa katika Miaka Miwili iliyopita Ronaldo amempiku na kuitwaa.
Hivi sasa Messi yupo nje ya Uwanja akijiuguza Goti aliloumia Mwezi Septemba lakini anatarajiwa kurudi kilingeni hapo Novemba 21 kwenye El Clasico dhidi ya Real Madrid.


Dar es Salaam. Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka atapanda ulingoni mjini Manchester Uingereza Novemba 7 kupambana katika pambano lisilokuwa la ubingwa.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security Limited, Juma Ndambile amesema kuwa Cheka anatarajia kuondoka wiki ijayo kwa ajili ya pambano hilo.
Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka, alisema kuwa tayari msaidizi wake, Rashid Nassoro yupo nchini Uingereza akiwa na mabondia wengine wawili huku akikamilisha maandalizi ya mwisho ya pambano hilo.Kwa mujibu wa Ndambile, Cheka anaweza kupambana na mpinzani wake wa awali, Martin Murray au bondia mwingine kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.
“Maandalizi yanaendelea vizuri na msaidizi wangu, Rashid Nassoro, kwa sasa yupo Uingereza akikamilisha masuala ya pambano hilo, kuna vitu fulani fulani vilikuwa havijakamilika, ila pambano ni Novemba 7 na leo jioni nitajua lini tutaondoka Tanzania,” alisema Ndambile ambaye kwa sasa yupo Kenya kikazi.Alisema kuwa Cheka kwa sasa yupo mkoani Morogoro akiendelea kujiandaa na pambano hilo na kama unavyojua, akishinda, atapata ofa kubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
Alisema kuwa Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la ubingwa

“Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato, nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.
Alisema kuwa Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.
Wakati huo huo; Bondia Benki Mwakalebela ambaye alitakiwa kupanda jukwaani jana usiku, hakuweza kufanya hivyo baada ya pambano lake kuhairishwa dakika za mwisho.


Barclays Premier League
PosLogo &TeamPWDLGDPts
1Manchester CityManchester City107121622
2ArsenalArsenal107121022
3West Ham UnitedWest Ham United10622920
4Manchester UnitedManchester United10622720
5Leicester CityLeicester City10541319
6Tottenham HotspurTottenham Hotspur10451817
7Crystal PalaceCrystal Palace10505115
8SouthamptonSouthampton10352314
9LiverpoolLiverpool10352-214
10West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion10424-314
11EvertonEverton10343013
12Swansea CitySwansea City10343013
13WatfordWatford10343-213
14Stoke CityStoke City10334-312
15ChelseaChelsea10325-411
16Norwich CityNorwich City10235-79
17BournemouthBournemouth10226-108
18SunderlandSunderland10136-86
19Newcastle UnitedNewcastle United10136-106
20Aston VillaAston Villa10118-84


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Oktoba 31

15:45 Chelsea v Liverpool
18:00 Crystal Palace v Man United
18:00 Man City v Norwich
18:00 Newcastle v Stoke
18:00 Swansea v Arsenal
18:00 Watford v West Ham
18:00 West Brom v Leicester

Jumapili Novemba 1
16:30 Everton v Sunderland
19:00 Southampton v Bournemouth

Jumatatu Novemba 2

23:00 Tottenham v Aston Villa


Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain watazikosa Mechi kadhaa za Arsenal kama ilivyothibitishwa na Meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger.
Wachezaji hao Wawili waliumia Jumanne iliyopita kwenye Mechi ya Raundi ya 4 ya Capital One waliyofungwa 3-0 na Sheffield Wednesday.
Oxlade-Chamberlain aliumia Dakika ya 5 tu ya Mechi hiyo alipopata tatizo la Musuli za Pajani na kubadilishwa na Walcott ambae nae ilibidi atolewe Dakika ya 19 baada kuumia Musuli za Mguuni.
Ingawa bado haijathibitika watakuwa nje kwa muda gani, Wenger amethibitisha Wawili hao kuikosa Mechi ya Ligi Kuu England ya Jumamosi Ugenini na Swansea City na pia ile ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI huko Munich watakaporudiana na Bayern Munich.

Mechi nyingine ambayo Wachezaji hao wataikosa ni ile Dabi ya London ya Kaskazini na Mahasimu Tottenham.



Chelsea wana kibarua tena wikendi hii watakapowakaribisha nyumbani Liverpool kwenye Ligi ya Premia Jumamosi.
Vijana wa Jose Mourinho wamekuwa wakiandikisha matokeo mabaya msimu huu, meneja huyo anakabilisha na shinikizo la kubadili mambo.
Chelsea wameshinda mechi moja pekee kati ya sita walizocheza karibuni zaidi katika mashindano yote.

The Blues wamefungwa mabao 19 Ligi ya Premia na ni Norwich (21), Bournemouth na Newcastle (wote wakiwa na 22) ambao wamefungwa mabao mengi zaidi msimu huu.
Ingawa huenda mshambuliaji wao Diego Costa akacheza, bado kuna shaka kumhusu Pedro ambaye anafuatiliwa kwa karibu baada yake kurejelea mazoezi.
Hata hivyo watakuwa bila Branislav Ivanovic na Thibaut Courtois. Nemanja Matic, aliyepigwa marufuku mechi moja atarejea uwanjani baada ya kutimikia marufuku hiyo mechi dhidi ya Stoke katika League Cup.
Upande wa Liverpool, meneja wao mpya Jurgen Klopp ataweza kumtumia Christian Benteke lakini Daniel Sturridge bado anauguza jeraha, Kolo Toure vilevile.
Akizungumza na wanahabari leo Mourinho amesema: “Matokeo sasa yamekuwa kila kitu (hasa kwenu wanahabari). Ni jambo la kushangaza kwamba miezi michache iliyopita nilishinda mechi nyingi na nikawa bingwa wa Uingereza, watu walikuwa wakisema kuna mambo muhimu zaidi kushinda matokeo.”
Kwa upande wake, Klopp amesema Chelsea bado ni hatari.
“Sina uhakika kwamba ni rahisi kucheza dhidi ya Chelsea leo kuliko mwaka jana. Mbona iwe hivyo?”

Liverpool walishinda mechi tatu mfululizo Stamford Bridge mwaka 2011 lakini hawajashinda hata mechi moja tangu wakati huo.

11218903_963430877028605_2270729444866256425_n
Wafanyakazi wa kampuni ya Screen Masters Limited ya jijini Dar wakiendelea kulipamba basi la Mbeya City. 
12079536_963430803695279_6917505578594463550_n
Basi la klabu ya Mbeya City FC baada ya kupambwa na kampuni ya Screen Masters Limited ya Dar es Salaam tayari kuanza shughuli ya kusafirisha wachezaji wa timu hiyo kwa safari za ndani na nje ya Mbeya kwenye mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara.

12196214_1667951416755226_8732075203516045367_n

Hatua kubwa sana hongera kwa uongozi wa timu,baada ya basi nini kinafuata usichoke kuwa nasubira kikubwa tuendelee kuisapoti timu yetu.
Posted by Mbeya City Fans on Thursday, October 29, 2015



Kocha wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ambaye wengi wamekuwa wakihoji juu ya mahusiano yake na wachezaji wa timu yake pamoja na aina ya mbinu anazotumia kuifundisha timu hiyo, October 30 amejibu kauli za kiungo wa zamani wa timu hiyo Paul Scholes ambaye October 29 aliponda mbinu za kocha huyo.
October 30 Louis van Gaal amejibu juu ya kauli ya Scholes ambaye alilenga kukosoa mfumo wa kocha huyo, Scholes alisema kwa sasa mfumo wa Man United sio mzuri na asingeweza kufurahia kucheza kikosi hicho akiwa chini ya Van Gaal. October 30 Louis van Gaal amemjibu Scholes ambaye ni mchezaji wa zamani wa Man United mwenye heshima klabuni hapo.
2DA584D700000578-3296538-Former_Manchester_United_midfielder_Paul_Scholes_has_criticised_-a-1_1446205312799
Paul Scholes
“Hana mamlaka yoyote hivyo anaweza kusema kila kitu kwa ajili ya faida yake au klabu, sitaki kujitetea kwa sababu siwezi kujitetea, nafikiria Scholes kama nguli wa klabu alipaswa kuongea na kocha au rafiki yake Ryan Giggs au Ed Woodward lakini sio kwa njia aliyoichagua kwa sababu atakuwa akilipwa na BBC au SKY, siku zote huwa na kauli ya kidachi fimbo na mawe ndio inaweza kuvunja mifupa lakini sio maneno”>>> Louis van Gaal
Tukiwa bado katika muendelezo au mfululizo wa mechi mbalimbali za soka, naomba nikusogezee ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara, Uingereza na Hispania zitakazochezwa weekend hii, Ligi Kuu Tanzania bara October 31 na November 1 kutakuwa na jumla ya mechi nane, baada ya hapo Ligi Kuu Tanzania bara itasimama hadi December 12 hii inatokana na kupisha maandalizi ya mechi ya Algeria na michuano ya Kombe la Chalenji. Hii ni ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania, Uingereza na Hispania kwa mechi za October 31 na November 1.
vpl
Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara weekend hii zitachezwa saa 16:00
epl
Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza kwa saa za Afrika Mashariki October 31
  • Chelsea Vs Liverpool  Saa 15:45
  • Crystal Palace Vs Man Utd  Saa 18:00
  • Man City Vs Norwich Saa 18:00
  • Newcastle Vs Stoke Saa 18:00
  • Swansea Vs Arsenal Saa 18:00
  • Watford Vs West Ham Saa 18:00
  • West Brom Vs Leicester Saa 18:00
Jumapili ya November 1
  • Everton Vs Sunderland Saa 16:30
  • Southampton Vs Bournemouth Saa 19:00
Laliga
Ratiba ya Ligi Kuu Hispania kwa saa za Afrika Mashariki Jumamosi ya October 31
  • Real Madrid Vs Las Palmas Saa 18:00
  • Valencia Vs Levante Saa 20:15
  • Villarreal Vs Sevilla Saa 20:15
  • Getafe Vs Barcelona Saa 22:30
  • Real Sociedad Vs Celta de Vigo  Saa 00:05
Jumapili ya November 1
  • Eibar Vs Rayo Vallecano Saa 14:00
  • Espanyol Vs Granada CF Saa 18:00
  • Sporting de Gijón Vs Málaga Saa 20:15
  • Real Betis Vs Ath Bilbao Saa 22:30

Wakiingia katika basi tayari kwa msafara
Watumiaji mbalimbali wa vyombo vya muziki wa msanii Wizkid wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere tayari kwa shoo yao ya leo katika Viwanja vya Leaders.
Huyo mwenye fulana nyeusi anaitwa  Snipes ndio kiongozi wa bendi ya msanii Wizkid.

waliotembelea blog