Monday, August 31, 2015



Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Oliver Giroud ambaye wengi wamekuwa wakimlaumu kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuwa hawezi kutwaa ubingwa akiwa na mshambuliaji huyo pekee, wengi walikuwa wakishinikiza Wenger amsajili Karim Benzema.
August 31 Oliver Giroud amekutana na maswali ya waandishi wa habari kuhusu klabu yake ya Arsenal kuhusishwa kutaka kusajili mshambuliaji mpya. Oliver Giroud ana majibu haya kuhusiana na Arsenal kutaka kumsajili mfaransa mwenzake Karim Benzema na yeye mtazamo wake kuhusu usajili huo.
gun__1412060818_social_giroud
“Ni kweli kila mwaka huwa kuna tetesi za kusajiliwa mshambuliaji mpya, kuna msimu ambao tulimsajili Sanchez, Welbeck na wengine lakini tulikuwa tukizungumza kuhusiana na Suarez, ni kawaida kwa klabu kuna mengi ya kutarajiwa, najua mashabiki wanataka tusajili kwa fedha nyingi”>>> Giroud
“Hilo sio swali ninalopaswa kujibu mimi, kocha anajua vizuri nini anafanya, wakati mwingine hutakiwi usajili tu ili mradi na wakati mwingine kuna kuwa hakuna mchezaji unaye muhitaji, tukiachana na hayo itakuwa vizuri kama Karimu angesajiliwa”>>> Giroud
Olivier-Giroud-Karim-Benzema-601898
Klabu ya Arsenal ya Uingereza ilikuwa ikihusishwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anakipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema, ambapo Arsenal walikuwa wapo tayari kutoa pound milioni 50 ili kumpata staa huyo kabla ya siku kadhaa nyuma, staa huyo kuthibitisha kuwa hayupo tayari kuondoka Real Madrid.



Tukiwa tunaelekea kufungwa kwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Uingereza, nimeona nikukumbushe wachezaji watano waliowahi kusajiliwa kwa fedha nyingi saa chache kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Mesut Ozil – 2013

Ikiwa saa kadhaa zilikuwa zimesalia kabla ya dirisha la usajili kufungwa Uingereza mwaka 2013, klabu ya Arsenal iliridhia kutoa pound milioni 42.4 kumsajili kiungo wa Kijerumani aliyekuwa katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Mesut Ozil na kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.
Arsenal-2014-Season-in-Pictures

Fernando Torres na David Luiz 2011

Baada ya misimu mitatu ya mafanikio katika klabu ya Liverpool Fernando Torres mwaka 2011 alijiunga na klabu ya Chelsea ya London kwa pound milioni 50 kwa wakati huo ilikuwa ni rekodi kubwa ya usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu Uingereza. Lakini Torres alishindwa kuonyesha makali yake Chelsea kwani alicheza mechi 110 na kufunga goli 20. Siku hiyo hiyo aliyosajiliwa Torres ndio siku aliosajiliwa beki wa Kibrazil David Luiz akitokea Benfica ya Ureno.
Roberto Di Matteo

Dimitar Berbatov 2008

Mwaka 2008 klabu ya Manchester United ilikamilisha uhamisho wa pound milioni 30.75 kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Bulgaria Dimitar Berbatov kutokea klabu ya Tottenham Hotspur, hata hivyo uhamisho huo ambao ulifanywa na Man United ilikuwa ni sawa na wao walivyozidiwa kete na Chelsea kwa Pedro kwani Berbatov alikuwa ajiunge na Man City kabla ya Ferguson kumdaka Uwanja wa ndege.
Dimitar-Berbatov

Andy Carroll na Luis Suarez – 2011

Mwaka 2011 kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool  Kenny Dalglish aliwasajili kwa pamoja Andy Carrol kutokea klabu ya Newcastle United na Luis Suarez akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi.
Andy-Carroll

Andrei Arshavin – 2009

Andrei Arshavin mshambulaiji wa kimataifa wa Urusi aliyetua katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa pound milioni 15 Zenit, licha ya Arshavin kushindwa kutamba katika klabu ya Arsenal na kitu pekee kikubwa alichowahi kufanya ni kuifunga Liverpool magoli manne.
Image_5_for_Arsenal_00_Fulham_gallery_98738532
Hiyo ndio kumbukumbu ambayo nimekukumbusha mtu wangu kwani hadi sasa tunategemea kuona lolote likitokea katika masaa machache yaliosalia ili kufungwa kwa dirisha la usajili la Ligi Kuu Uingereza.



Mtoto wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na nahodha wa klabu ya Manchester United Kai Rooney alionekana mwenye furaha, katika mapumziko ya mwisho wa wiki na mama yake mzazi Coolen Rooney wakiwa Hispania kwani alipata bahati ya kukutana na wachezaji wa FC Barcelona.
CNuEGMjWIAA71TR
Kai Rooney ambaye ni mtoto wa Wayne Rooney alionyesha kuwa na furaha kupata bahati ya kukutana na Lionel Messi, Suarez, Neymar na Pique hivyo mama yake aliamua kuiweka picha aliyopiga mtoto wake na mastaa hao katika mtandao wa twitter na kumshukuru beki wa zamani wa Man United

waliotembelea blog