Mtu wangu wa nguvu January 12 katika
pitapita zangu mtandaoni nikakutana na list ya majina ya utani ya mastaa
watano wa soka. Katika maisha kila mmoja anaweza akawa na jina la utani
ambao huenda kapewa na familia yake au washikaji zake mtaani au kwa
sababu ya umahiri wake uwanjani ndio anaweza kujkuta kapewa jina.
January 12 naomba nikusogezee majina ya utani ya mastaa hawa wa soka Messi, Ribery, Torres, Robben na Kroos.
5- Toni Kroos huyu kutokana na umahiri wake uwanjani, kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Carlo Ancelotti aliwahi kumtunga jina na kumuita “The professor” hii inatokana na uwezo na akili yake ya kuumiliki mpira uwanjani.
4- Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya Liverpool na Chelsea vya Uingereza Fernando Torres alipewa jina la utani la “El Nino” ambalo lina maana ya kuwa mtoto, Torres ambaye ana umri wa miaka 31 amerudi kwenye klabu yake iliyomlea ya Atletico Madrid, lakini wakati ana umri wa miaka 16 akiwa Atletico
alikuwa akicheza mpira kwa kiwango cha juu kutokana na wengi kutokuwa
wamelishika jina lake na muonekano wake wa kitoto wakawa wanamuita “El Nino”
3- Franck Ribery huyu jina lake la utani anaitwa “Scarface” jina ambalo alipewa kutokana na sura yake kuwa na makovu na mikunjo usoni. Makovu ya Ribery yalitokana na ajali aliyowahi kuipata wakati akiwa na umri wa miaka miwili, makovu ambayo yapo usoni kwake hadi leo.
2- Mshindi wa tuzo ya tano ya Ballon d’Or Lionel Messi yeye jina lake la utani anaitwa “La Pulga” ambalo limetokana na kimo chake ambacho kimekuwa kikiwasumbua wapinzani, licha ya kuwa hana umbo kubwa sana.
1- Winga wa kimataifa wa Uholanzi Arjen Robben yeye
kutokana na uwezo na mbio zake uwanjani na uwezo wake wa kujirusha
uwanjani pale anapokuwa kafanyiwa faulo uwanjani, alipewa jina la mdachi
anayepaa “The Flying Dutchman” .