Wednesday, September 11, 2013

KATIKA ulimwengu wa mastaa wa Kibongo, kuna vijimambo kibao mojawapo ni wale wa kike kujiingiza kwenye mapenzi na kudanganywa kilaini kisha kushiriki mchezo wa kikubwa bila usalama (kinga).
Matokeo yake ni kuzalishwa na kuachwa solemba na sasa wanalea
watoto wao wenyewe bila baba zao. Unajua sababu? Ni ileile, yaani kupenda maisha ya ghali wakati hawana uwezo hivyo kujikuta wakijinasua kwa kujirahisisha kimapenzi kwa wanaume.
Leo Ijumaa Wikienda linakuletea mastaa 10 wa Kibongo waliozalishwa na kuachwa solemba wakilea watoto bila baba zao.
 
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
Alianzia kwenye filamu kisha akajiingiza kwenye muziki. Kwa mujibu wake mwenyewe, aliwahi kukiri kuwa  aliingia kwenye fani hizo kwa ajili ya kujitafutia kipato ili kulea wanaye. Aliolewa ndoa ya kwanza huko kwao Tabora na kuzalishwa mtoto mmoja kisha ndoa ikaota mbawa. Hakukaa muda mrefu akapata mwanaume mwingine ambaye alimpa ujauzito na kuzaa mtoto wa pili. Aliwahi kusema kati ya wanaume hao, hakuna anayemsaidia kulea.

ISABELLA MPANDA

Alianzia kwenye urembo, akatwaa Taji la Miss Ruvuma 2006 na sasa anafanya filamu na muziki. Ana watoto wawili wa kiume ambao amezaa na  wanaume tofauti. Anakiri kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa anaweza kuwapatia malezi bora wanaye kwa msaada kiduchu kutoka kwa wanaume hao.
 
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Alianzia kwenye uigizaji kisha urembo na sasa ameongezea muziki. Amezaa na Mkurugenzi wa Tuesday Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ ambapo walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kike na baada ya hapo mapenzi yakaisha. Kwa kuwa mapenzi yalikwisha, Jini Kabula alibaki na mwanaye akimlea mwenyewe japo Mr Chuz huwa anampiga ‘tafu’.

JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Alianzia kwenye urembo kisha akaingia kwenye filamu na muziki. Ana mtoto mmoja. Anakiri kuwa mtoto huyo alizaa na mwanaume mmoja ambaye hakumtaja kwa jina lakini baada ya hapo waliachana na anaendea kumlea mwanaye peke yake.

NURU NASSORO ‘NORA’

Mwigizaji huyo aliolewa na mwanaume wake wa kwanza ambaye alimzalisha mtoto mmoja wa kiume. Baadaye waliachana na kuanzia hapo hakumsaidia chochote kuhusu matumizi ya mtoto hadi mwanaume huyo alipofariki dunia na sasa anamlea mwanaye mwenyewe.

JACQUELINE DUNSTAN ‘JACK WA MAISHA PLUS’
Alipata umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus II kabla ya kujiingiza kwenye filamu. Aliachwa solemba baada ya kuzalishwa na mwanaume ambaye hadi sasa hana mawasiliano naye na hajui alipo hivyo analea mwanaye mwenyewe akiwa kwa bibi yake mkoani Morogoro.
 
SNURA MUSHI
Alianzia kwenye uigizaji kabla ya hivi karibuni kujikita pia katika tasnia ya filamu. Ana mtoto mmoja wa kike. Anakiri kuwa tangu akiwa mjamzito baba mtoto wake aliingia mitini. Mpaka sasa anamlea mwanaye mwenyewe kupitia sanaa ya filamu na muziki.

FAIDHA OMARI ‘SISTER FAY’

Japo hasikiki sana, mwanzoni alijikita kwenye muziki na hivi karibuni ameongezea nyingine ya uigizaji. Ana mtoto mmoja aliyejifungua mwaka jana. Anakiri kuachwa njia panda na mwanaume aliyemzalisha kwani hadi sasa anamlea mwanaye mwenyewe.
 
MAUNDA ZORRO
Alipata umaarufu kupitia muziki na baadaye akaongezea uigizaji. Ana mtoto mmoja na huwa hapendi kumwanika mwanaume aliyemzalisha ambapo mpaka sasa anaishi nyumbani kwa baba yake, mzee Zahir Zorro na hakuna dalili zozote za ndoa.

YVONNE-CHERRY NGATIKWA ‘MONALISA’
Mwigizaji huyu legendary pia ni Mtangazaji wa Radio Times FM. Alijaliwa kupata mtoto na prodyuza wa filamu za Kibongo, George Otieno ‘Tyson’ ambaye alikuwa ni mume wake wa ndoa. Baadaye waliachana akaolewa tena kwa ndoa ya Kiislam na kupata mtoto mwingine. Mpaka sasa anaishi na watoto wake na anawalea kupitia kazi zake za filamu na utangazaji.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog