Sunday, December 13, 2015


Kila mtu ana kipaji chake katika maisha..wapo waliotamani kufanya hivi lakini mwisho wa siku wakajikuta wanafanya kitu kingine kabisa mbacho hawakudhamiria kufanya.
Kwa mchezaji wa Manchester City na timu ya Taifa ya Ivory Coast Yaya Toure kumbe endapo mambo yasingemnyookea kwenye soka basi angekuwa mcheza karate.
Huo ndio mchezo ambao kiungo huyo alikuwa ameanza kucheza wakati akiwa bado mdogo na huenda mpaka sasa angebaki kwenye mchezo huo endapo baba yake mzazi asingemkataza akihofia angepata majeraha kupitia mchezo huo.
Wakati akiwa mdogo katika kipindi cha wiki moja, alifanya vyema na aliweza kuteuliwa kushiriki katika mashindano makubwa yaliyofanyika Kenya ambayo hata hivyo hakwenda kutokana na baba yake kumzuia.
Kiungo huyo amekuwa na mafanikio makubwa kupitia soka na juzi alifanikiwa kushinda tuzo ya BBC aambayo huyolewa kila mwaka kwa mchezaji bora Afrika.



Michuano ya klabu Bingwa Dunia ilianza December 10 2015 katika ardhi ya Japan, hii ni michuano ambayo inatafuta Bingwa wa Dunia kwa ngazi ya vilabu, kwa upande wa bara la Afrika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio ilikuwa inawakilisha bara hili.
Generated by IJG JPEG Library
TP Mazembe ambayo inachezewa na watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ilianza kucheza michuano hiyo December 13 katika hatua ya robo fainali dhidi ya klabu ya Sanfrecce na kukubali kipigo cha goli 3-0, huu ni mchezo ambao watanzania wengi walikuwa wanautazama, kwani Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu  wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kushiriki michuano hiyo.
Generated by IJG JPEG Library
Sanfrecce walianza kupata goli la kwanza dakika ya 44 kupitia kwa Shiotani ikiwa ni dakika moja imesalia kabla ya kwenda mapumziko. TP Mazembe walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha ila dakika ya 56 kipindi cha pili Chiba akapachika goli la pili kwa Sanfrecce, licha ya TP Mazembe kutokata tamaa, goli la dakika ya 78 la Asano ndio lilihitimisha safari ya TP Mazembe kwenda hatua ya nusu fainali.
Generated by IJG JPEG Library
Generated by IJG JPEG Library

waliotembelea blog