Wednesday, May 21, 2014



01_a939d.jpg
1_90ea0.jpg
2_a9106.jpg
3_0dd77.jpg
4_b7898.jpg
5_a1af1.jpg



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mteule wa Tanzania nchini Sweden Mhe,Dora Msechu , aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi mteule wa Tanzania nchini Sweden Mhe,Dora Msechu , aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo,baada ya mazungumzo 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi mteule wa Tanzania nchini Sweden Mhe,Dora Msechu , aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo,baada ya mazungumzo

Shirika la kutetea haki za binadamu Human rights watch limeishutumu serikali ya Somalia kwa kuwanyima wafungwa haki za uakilishi wa wakili na kuwashitaki raia wa kawaida chini ya mahakama za kijeshi.
Shirika hilo limesema kuwa mamia ya raia wanahukumiwa kwa sheria kali wasizoelewa. Human rights watch pia imesema kuwa raia wengi wamejikuta matatani baada ya kukamatwa katika msako wa kitaifa unaofanywa na mashirika ya kijasusi ya Somalia na mara nyingie wanazuiliwa kwa muda mrefu bila kufunguiwa mashtaka.
Kuzuiliwa kwa muda mrefu ni tatizo ndogo sana kwa raia hao wa Somalia ikilinganishwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na kutishia usalama wa nchi. Ukipatikana na hatia, hukumu ni kifo.
Licha ya kuwa mashirika ya haki za binadamu yamekuwa yakipinga kutolewa hukumu hii, Somalia ni mojawepo ya nchi chache Afrika ambayo bado inatoa huku hiyo.
Wasiwasi mkubwa ni kwamba, washukiwa hawapewi fursa ya kujitetea. Na wala mahakama hizi za kijeshi hazihitaji ushahidi mwingi kuamua kuwa una hatia.(P.T)
Human rights Watch imetaja katika ripoti yao kisa kimoja ambapo zaidi ya kesi 24 zilisikilizwa na kuamuliwa kwa chini ya siku 4.
Mahakama yajitetea
Lakini akijibu madai hayo, mwenye kiti wa mahakama za kijeshi wa Somalia Liban Cali Yarow ameambia BBC kuwa ni upuuzi mtupu na mwingilio wa jamii ya kimataifa katika mambo yasiyowahusu.
''Haya mashirika ni ya nje, na hayajui mambo yanayofanyika nchini kwetu. Inasikitisha kwamba hawazungumzii matatizo yetu ila wanapiga kelele tunapojaribu kujitatulia wenyewe. Ripoti hiyo imejaa madai yasiyo kweli.''
Human rights watch iliwahoji zaidi ya watu 30 na familia za watu walio shutumiwa, na wengi wao wamesema kuwa mahakama hizo haziwapi wafungwa nafasi ya kujitetea.
Mara nyingine hata kuwalazimisha kukiri mashtaka ambayo hawakufanya na hakuna ruhusa ya kukata rufaa. Hapa ndipo mwisho wa kesi.
Jamii ya kimataifa
Sasa shirika hilo limetoa wito kwa jamii ya kimataifa na hasa wafadhili kushinikiza Somalia kurejesha haki za wafungwa na kuzuia raia kushtakiwa katika mahakama za kijeshi.
Lakini mwenyekiti wa mahakama hiyo Liban Cali Yarow amepuuzilia mbali ripoti ya shirika hilo akisema kuwa imejaa madai ya uongo.
''Ningependa kumsihi yeyote ambaye ana malalamiko juu yetu awasilishe kwetu badala ya kuandika kwenye magazeti. Kuandika tu bila kutushauri ni sawa na kutuwekelea madai ya uongo.'' Amesema Liban Yarow.
Maafisa wa Somalia wametetea hatua ya kuwashtaki washukiwa wa ugaidi katika mahakama za kijeshi wakisema kuwa mahakama za kiraia hazina ulinzi wa kutosha na uwezo wa kusikiliza kesi zenye uzito mkubwa kiasi hicho.



 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na ujembe wa watu kutoka Congo hawapo pichani waliomtembelea ofisini kwake kuwaalika wasanii kutoka Tanzania kushiriki katika sherehe za fiesta nchini Congo kwa lengo la kudumisha amani na mshikamano katika nchi za maziwa makuu. Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akifafanua jambo kwa wajumbe wa maandalizi ya fiesta kutoka Congo walipomtembelea ofisini kwake, kulia ni mratibu wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bw. Faso Mushigo Celestin na katikati ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wapili kushoto akipokea zawadi kutoka kwa wajumbe kutoka Congo waliokuja nchini kuwaalika wasanii wa Tanzania kushiriki fiesta nchini Congo, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiangalia CD iliyorekodiwa matukio mbalimbali ya fiesta ya mwaka jana ilivyokuwa nchini Congo. Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
Picha na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM

Na: Genofeva Matemu 
Wasanii wa muziki nchini waalikwa kushiriki katika sherehe za fiesta nchini Congo zinazotarajiwa kufanyika julai 16 hadi 26 mwaka huu.
Mwaliko huo umetolea na wajumbe kutoka Congo walioshiriki katika siku ya Uanuwai wa Utamaduni duniani iliyoadhimishwa kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam na baadaye kumtembelea Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt Fenella Mukangala  ofisini kwake ambapo walimuomba wasanii wa muziki kutoka Tanzania kushiriki sherehe fiesta zitakazofanyika nchini Congo mwaka huu.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na sherehe hizo Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga amesema kuwa lengo la sherehe za fiesta mwaka huu ni kuwakutanisha wasanii wa Afrika wanaoishi nchi za maziwa makuu ili waweza kupata nafasi ya kupanda mti wa amani ikiwa na lengo la kuziwezesha nchi hizo kuwa na mazungumzo ya amani.
Bi. Gizenga amesema kuwa wanatarajia kupata wasanii wa muziki kutoka nchini Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi pamoja na wasanii wa Congo watakaoshiriki fiesta ndani ya mikoa miwili nchini Congo katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini Goma pamoja na Kivu ya Kusini Bukavu.
“Tumezunguka nchi zilizopo katika maziwa makuu tukiwaomba wasanii wa nchi hizo kushiriki katika sherehe za fiesta nchini Congo ambazo mwaka huu tutahusisha upandaji wa mti wa amani tukizitaka nchi hizo ziwe na mazungumzo ya amani na mshikamano” alisema Bi. Gizenga.
Kwa upande wake waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amewashukuru wajumbe hao kwa mwaliko na kuwahaidi kuwa wasanii kutoka nchini Tanzania watapata fursa ya kipekee hivo ni muhimu kwao kushiriki ili waweze kuiwakilisha Tanzania na kuweza kupata uzoefu kutoka nchi jirani.
Aidha Dkt. Mukangara amesema kuwa ni muhimu kwa Tanzania kushiriki katika sherehe hizo kwani Tanzania ilishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuleta amani ya nchi ya Congo hivyo aina budi kushiriki na kuendeleza amani na mshikamano wa nchi hizo mbili.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi wa Japan, Yoshihiro Suga, wakati alipofika ofisini kwake Jijini Tokyo Japan leo Mei 21, 2014, akiwa katika ziara ya kikazi. Picha na OMR



Serikali ya Japan imeelezea nia yake ya kuendelea kuchangia bajeti ya Tanzania na kufafanua kuwa, inafanya hivyo kwa kutambua kuwa Tanzania ni mshirika mkubwa wa maendeleo na kwamba ni nchi yenye kutia matumaini katika kupiga hatua za kimaendeleo.
Akizungumza jana katika Ofisi yake jijini Tokyo, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Japan Mheshimiwa Yoshihide Suga alisema, serikali ya Japan inaifahamu Tanzania kama mshirika wa maana katika maendeleo na kwamba inafahamu mchango wa Tanzania katika kuendeleza ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki. Katibu Mkuu huyo pia aliongeza kuwa, Tanzania imemudu kudumisha amani kwa kipindi kirefu huku ikipiga hatua za kimaendeleo na kwamba watu wake wamebakia wamoja kwa miaka mingi licha ya kuwa na tofauti za kitamaduni, kijiografia na kidini.
Kauli hiyo ya Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Japan, imetolewa kufuatia mkutano wake na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambaye yupo jijini Tokyo kwa ziara ya kikazi. Katibu huyo alisema, “tunaifahamu Tanzania kama nchi muhimu inayodumisha amani. Nchi yenu imeweza kudumisha Muungano kwa miaka 50, Japan inawapongeza sana. Tunafahamu mnafanya kazi kubwa katika kuwaendeleza wananchi wenu na sisi kama ndugu na rafiki zenu tuko tayari kabisa kushirikiana nanyi.”
Katibu Mkuu Suga alieleza pia kuwa, Tanzania ni nchi iliyo thabiti katika ukanda wa Afrika Mashariki na inayo nguvu katika kuhakikisha ukanda huu unaendeleza utengamano hali ambayo inachangia kuwepo maingiliano ya wananchi wa ukanda wa Afrika Mashariki sambamba na kutanua fursa kwa wawekezaji kutoka nje ya Afrika.
“Mko thabiti katika mambo mengi na hasa kuweza kumudu kuwa na amani na utulivu, mnategemewa sana na nchi za Afrika Mashariki na kwa hali hii sisi tupo tayari kuendelea kutenga fedha katika bajeti yetu kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya Tanzania katika ushirikiano wa serikali na sekta binafsi (PPP),” alisema.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimueleza Katibu Mkuu Suga kuwa, Tanzania inapokea kwa heshima kubwa mchango wa Japan kwa kutambua hali yake ya utulivu na kwamba anatumia ziara yake Japan kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.

“Tuna kazi kubwa mbele yetu katika kuwaendeleza Watanzania. Hatuwezi kufanya kazi hiyo peke yetu, hivyo basi nitumie nafasi hii kukuomba Mheshimiwa Katibu Mkuu kutusaidia kuhamasisha wawekezaji kutoka Japan ili waje kushirikiana nasi katika kuiendeleza Tanzania. Urafiki kati yenu na sisi ni wa siku nyingi na tungetegemea sasa tuubadili na utazame fursa za kuchangiana kiuchumi na hasa katika kuwekeza kwa kubadilishana teknolojia pamoja na mtaji,” Makamu wa Rais alisema.
Mheshimiwa Makamu wa Rais yuko nchini Japan kwa ziara ya kikazi na tayari amefanikiw akukutana na wakuu wa makampuni mbalimbali makubwa duniani yenye makao yake makuu nchini Japan na kisha kutumia nafasi hiyo kuelezea fursa za uwekezaji nchini Tanzanja sambamba na kubainisha umuhimu wa sekta binafsi kushiriki katika kusaidia maendeleo ya nchi zinazoendelea zilizopo Afrika, Tanzania ikiwa ni kipaumbele.





























Leo imetimia miaka 18 tangu ndugu zetu walipopata ajali na Meli ya MV. Bukoba 21 May 1996, na wengi kupoteza maisha! Ni tukio kubwa lililoua watu wengi nchini na kuacha huzuni kubwa kwa Watanzania. Comment R.I.P kwao ili waendelee kupumzika kwa aman..


Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2014/2015) unaanza Juni 15 hadi
Agosti 3 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa
mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.

Kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai
30 mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 4 na 11 mwaka
huu. Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 12 hadi 14 mwaka huu.

Usajili hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 14 na 29 mwaka huu. Kupitia na kutangaza
majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 4 mwaka
huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 5 na 6 mwaka huu.

Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu,
na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 24 mwaka huu).



Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) chenye watu 25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).

Mechi hiyo itachezwa Jumamosi (Mei 24 mwaka huu) katika Jiji la Kaduna kwenye Jimbo la Kaduna ambalo lipo katikati ya Nigeria. Msafara wa timu hiyo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi unaondoka kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Ngorongoro Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza iliyofanyika nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.

Mwamuzi Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Atasaidiwa na Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.

TIMU YA U15 YAWASILI GABORONE
Timu ya Tanzania ya umri chini ya miaka 15 imewasili salama jijini Gaborone, Botswana kwa ajili ya michezo ya Afrika ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Mei 22 mwaka huu dhidi ya Mali.

Kikosi hicho cha wachezaji 16 chini ya Kocha Abel Mtweve kimetua jijini Gaborone jana (Mei 19 mwaka huu) jioni kwa ndege ya South African Airways. Michezo hiyo itamalizika Mei 30 mwaka huu.

Wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.

Nchi nyingine zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland.

Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambazo nazo zilikuwa zishiriki kwenye michezo hiyo zimejitoa dakika za mwisho.

10357474_634079413340945_8148690486284095511_nMechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe iliyochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 63,345,000.
Mapato hayo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 yametokana na washabiki 11,079 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000.
 
Mgawo wa mapato hayo ni asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 9,662,796.61, gharama za kuchapa tiketi sh. 6,000,000, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 7,152,330.51, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 9,536,440.68 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa pamoja wamepata sh. 30,993,432.20.


 
Nini matarajio ya africa katika Kombe la Dunia ?
Timu za Africa Zitafanya Vizuri  Brazil. Na kuna sababu za kusema haya kwani Tunaubora unaostahili . Katika michuano mikubwa ya Ulaya Kuna mchezaji Mmoja kutoka Africa katika ligi za ulaya , Na wachezaji hao wanacheza kwa kiwango kikubwa . Tatizo kubwa Africa ni kuwa Viongozi hawatuheshimu .Ni mpaka Tuheshimiwe  ,Na hatuwezi kuheshimika na watu wengine kama hatueshimiki afrika  .Mimi ndio Nasema , Na ninasema kuwa Africa itasema  Brazil.

Je unaionaje  Ivory Coast, Inaiwakilisha africa kama Timu bora katika Bara ?

Kila Mmoja ana maoni kuhusu  Côte d’Ivoire Ni mmoja kwenye Makaratasi .Ukitazam katika hilo hauwezi kuona kuona usawa katika timu za Africa , Ninachosema kuwa Tembo wa afrika watatakiwa kuonyesha kile ambacho waafrika wanatarajia kutoka kwao. Ni wakati wa wao kuonyesha kuwa wanatakiwa kufanya Kweli katika michuiano hiyo. Watatakiwa kuonyesha kweli wanataka kushinda . Na nina aamini kuwa kizazi hiki kitatakiwa kuonyesha kile ambacho waafrika wanataka .

Ukiwa Nahodha na kupangwa Kundi na  Brazil, Huoni kama ni balaa limekuja kwenu ?
Tunamuheshimu kila Mtu na kila Adui yetu tunameshimu na hatudharau mtu  Na timu zote zilizo kundini Tunaziheshimu  . Ni kweli  Brazil tunajua kuwa wapo kwao Brazil itakuwa na Nguvu kubwa kwani wapo kwao na wanamashabiki wao, Hatutawahofii . Katika maisha yangu tumecheza nao mara kadhaa . Tuliwafunga Brazil  2000 katika mashindano ya Kule Sydney. na kulikuwa na  Ronaldinho katika timu yao na wengi wengineo. Eto’o Haogopi . Cameroon Haiogopi .

ded5f-kagera-sugar1 

WAKATI dirisha la usajili wa ligi kuu soka Tanzania bara likiwa njiani kufunguliwa, wakata miwa wa Kaitaba, `Wanankulukumbi` Kagera Sugar wamegoma kufanya usajili wao kwa mfumo  wa majaribio .
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange amesema tayari wameshapata wachezaji 30 na tayari wameanza mazungumzo ya awali na baadhi ya wanandinga hao.
“Siku zote sisi hatufanyi usajili kwa kuwafanyia majaribio. Unajua ukumuita mtu afanye majaribio, daima anajipanga vizuri sana”.
“Kila mchezaji anajiandaa kwasababu anajua anafanya usaili. Unaweza kumchagua na kumwingiza katika timu, halafu tatizo likaanzia hapo

article-2634352-1E0DB02200000578-824_634x421 
Diego Costa akiwa mjini Belgrade kwa lengo la kuonana na mganga wa kienyeji.
 MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade nchini Serbia kumuona `Mganga wa miujiza`,  Marijana Kovacevic  ili amtibu na kurejea uwanjani haraka kwa ajili mchezo mkubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
Mganga huyo wa Serbia anawatibu wachezaji wenye matatizo ya misuli kwa kuwawekea placenta na Costa anataka kuichezea Atletico Madrid kwenye mechi ya fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid jumamosi ya wiki hii.

waliotembelea blog