Thursday, February 13, 2014


Uwanja wa Etihad
Mradi wa kuongezeka idadi ya mashabiki katika uwanja wa Manchester City kutoka mashabiki elfu arubaini na nane hadi elfu sitini na mbili umeidhinishwa.
Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Premier nchini England, itajenga maeneo zaidi ya mashabiki katika uwanja huo.
Mradi huu utajumuisha ujenzi wa maeneo mawili yatakayokuwa na mashambiki elfu nane zaidi.
Ujenzi huo utaifanya uwanja huo wa Etihad kuwa wa pili kwa ukumbwa nchini Uingereza baada ya uwanja wa Manchester United wa Old Trafford.
Madiwani wa baraza la jiji la Manchester, waliidhinisha mradi huo, ambao unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Manchester City ilihamia uwanja huo mwaka wa 2003.
Awali Uwanja huo ulikuwa na idadi ya kuchukua mashabiki elfu thelathini na nane, wakati ilipojengwa mwaka wa 2002, kwa matumizi ya michezo ya Jumuiya ya madola.


Ndege za umoja zizizokuwa na Rubani Goma
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umesema kuwa zaidi ya watu sabaini waliuawa mwisho wa mwezi uliopita na mapema mwezi huu.
Katika mahojiano na BBC, afisa mmoja wa shirika la Monusco, mjini Goma, Ray Tores, amesema kuwa ndege ya wanajeshi wake, iliyokuwa ikifanya uchunguzi, katika eneo hilo iligundua kuwa vijiji vitatu viliteketezwa na kuharibiwa kabaisa.
Amesema kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa watazuru eneo hilo baadaye hii leo ili kufanya uchunguzi zaidi.
Jeshi la kutunza amani la Umoja wa Mataifa limeimarisha juhudi zake katika eneo hilo, hasa tangu ilipoisambaratisha kundi la wapiganaji wa waasi wa M23, Novemba mwaka uliopita.
Bwana Torres, amesema kuwa zaidi ya makundi arubaini ya waasi yanajulikana kuendesha operesheni zao katika eneo hio la Goma.
Manne kati yao yamekuwa yakifanya mashambulio ya mara kwa mara na hivyo kuwa tishio kubwa la usalama.
Umoja wa Mataifa, umesema kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na makundi ya waasi yaliyojihami katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini, ili kuwatia watu wanaoishi katika eneo hilo hofu.
Afisa huyo amesema kuwa wengi wa waliouawa walikuwa na majeraha ya mapanga.
Wanajeshi wa DRC wakishika doria mjini Goma

usa_da187.jpg
Dhoruba kali ya majira ya baridi kali imesababisha zaidi ya watu 300,000 eneo la kusini mashariki mwa Marekani kukosa umeme wakati dhoruba hiyo ikielekea eneo la kati ya Atlantic na sehemu za kaskazini mashariki mwa taifa hili.
Dhoruba imesababisha kunyesha kwa darzeni ya sentimeta za theluji kote katika eneo la Washington DC hapo Alhamis. Wakati katika baadhi ya maeneo ya Washington imeripotiwa kuwepo mpaka sentimeta 46 za theluji.
Serikali kuu imefungwa pamoja na darzeni ya serikali za mji na mashule. Huko North na South Carolina, dhoruba imesababisha barabara ndogo na barabara kuu hazipitiki na kulazimisha madereva kuacha magari yao.

Watabiri wa hali ya hewa wamesema Carolina zote mbili zilitarajiwa kupata zaidi ya sentimeta 20 za barafu na theluji hadi Alhamis asubuhi baada ya kupata mchanganyiko wa theluji na mvua hapo Jumatano.
Hali ya hewa imesababisha maelfu ya safari za ndege kufutwa kwa muda, abiria kukwama kwenye viwanja vya ndege. Darzeni ya vifo vimeripotiwa kusababishwa na dhoruba ikiwemo watu watatu kufariki wakati gari la kubeba wagonjwa lilipoteleza kwenye barabara zilizokuwa na barafu huko Texas.
Chanzo, voaswahili.com


Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema kikosi chake kiko tayari kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia itakayochezwa keshokutwa (Ijumaa) jijini Lusaka.

Akizungumza kwenye hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika leo (Februari 12 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam, Kocha Kaijage amesema wachezaji wake wako vizuri, ingawa hakuwa tayari kutoa ahadi kuhusu matokeo.

“Vijana wako vizuri, lakini sitaki kutoa ahadi. Watanzania watuombee, watuunge mkono ili tuweze kufanya vizuri,” amesema Kocha Kaijage katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi.

Twiga Stars inaondoka na kikosi cha wachezaji 19 na benchi la ufundi lenye watu watano kwa ndege ya Fastjet kwa ajili ya mechi hiyo itakayooanza saa 9 kamili kwa saa za Zambia. Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho chini ya nahodha Sophia Mwasikili ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Happiness Mwaipata, Maimuna Mkane, Mwapewa Mtumwa, Sherida Boniface, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.

Wakati huo huo, timu ya Azam imeondoka leo alfajiri (Februari 12 mwaka huu) kwenda Beira, Msumbiji kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi Ferroviario da Beira itakayochezwa Jumamosi. Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, James Mhagama.

Naye mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Nassib Ramadhan ataongoza msafara wa timu ya Yanga inayoondoka kesho mchana kwenda Comoro kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine itakayochezwa Jumamosi.


  Mgeni Rasmi katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo,uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo,uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo ambaye ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,akizungumza na washiriki wa Kongamano hilo (hawapo pichani) wakati ufunguzi wake uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuja kuzungumza na Washiriki wa Kongamano hilo,jijini Mwanza leo.
Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania,Mh. Thamduycse Chilliza (katikati) akifatilia Kongamano hilo sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC),Julieth Kairuki (kushoto).Kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Afrika Kusini,Terry Govender.
Waheshimiwa Mawaziri wakishiriki pamoja na Wajumbe wa Kongamano hilo,kuimba wimbo wa Taifa.
Baadhi ya waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Wadau wa Bodi ya Utalii.

 
 
 
Fainali ya kombe la ligi nchini Hispania (Copa del Rey) inatafanyika tarehe 19 April 2014 na safari hii itawakutanisha vigogo wa La Liga Real Madrid na Barcelona. Mechi hii inatarajiwa kuwa ni ngumu na kuvutia kwani Madrid na Barca ni wapinzani wa jadi nchini Hispania na ikizingatiwa pia makocha wa timu hizi wote ni wageni na wanahitaji kutwaa vikombe wakiwa na timu zao mpya. Real Madrid imefika fainali baada ya kuwafunga Atl. Madrid kwenye nusu fainali kwa jumla ya magoli 5-0, wakati Barcelona wameitoa klabu ya Real  Sociedad kwa jumla ya magoli 3-1. 
 
 
 

 
 
KESHO KUFANYA YAKE NDANI YA KAHAMA NEY WA MITEGO

Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Marsha Bukumbi akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 mshindi wa shindano la Championi Mahela, Kizito George Chuma (kushoto).
Kizito George Chuma akiwa ameshika mfano wa hundi yake ya milioni 10.
 
Kizito George Chuma akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 na Global Publishers Ltd.
Meneja wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati) akimtambulisha mshindi wa milioni 10 za shindano la Championi Mahela kwa wanahabari (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Global Publishers Ltd, Marsha Bukumbi (wa kwanza kushoto) akipozi na mshindi wa milioni 10 pamoja na wakala wa Magazeti ya Global aliyejishindia pikipiki aina ya Skymark kutoka kampuni ya Shinyanga Emporium.


Mkurugenzi wa Kamapuni ya Shinyanga Emporium, Ritesh Monami (kushoto) akimkabidhi pikipiki wakala wa magazeti ya Global Publishers Ltd, Majid Hamis.
Timu ya Championi ikipozi na mshindi wa milioni 10.

Msanifu Kurasa wa Global, Huruma Bujiku (aliyekaa) akimuonyesha mshindi wa milioni 10 namna gazeti linavyoandaliwa. Aliyesimama kulia ni Meneja Masoko wa Global, Benjamin Mwanambuu.
...Kizito akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Ojuku Abraham.
Mhariri wa Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Mohamed Kuyunga (kulia) akimpongeza Kizito kwa kulamba M10.
Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Amani na Risasi Jumamosi, Erick Evarist (kushoto) akimkpongeza Kizito. Kizito akisalimiana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka (kushoto).
Kizito akifurahia jambo na Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Aziz Hashim (kulia). Kushoto ni Walusanga Ndaki.
Emmanue Okwi
Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Uganda na timu ya Young Africans leo ameruhiswa ramsi kuanza kuitumikia timu yake katika michezo ya Ligi Kuu na Mashindano ya klabu Bingwa Barani Afrika kufuatia shirikisho la soka nchini TFF kuiandikia barua klabu ya Young Africans.
Okwi ambaye alisajiliw aa Young Africans mwishoni mwa mwaka jana na kucheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya, alisimamishwa na Shirikisho la Soka la Nchini TFF wakati wakisubiria kupata udhibitisho wa usajili wake kutoka FIFA.
Mara baada ya barua hiyo, Okwi anatarajiwa kuungana na wenzake mwishoni mwa wiki mara timu itakaporejea kutoka Visiwa vya Comoro na ataanza kuonekana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting siku ya jumamosi Februari 22 mwaka huu.
Uongozi wa Young Africans unawashukuru wanachama, wapenzi na wadau kwa ujumla kwa kuwa wavumilivu wakati wa suala na hili na hatimaye limepatiwa ufumbuzi.



waliotembelea blog