Mkazi
wa Wazo Hill, Tegeta Mary Joseph (Katikati) akipokea zawadi ya fulana
toka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya
Ubungo, Mbezi na Tegeta Bw. Victor Mhindi (Kulia) wakati wa promosheni
ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani iliyofanyika katika baa ya Family iliyopo
Tegeta jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni
hiyo na Mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni redio E-fm, Gadner Habash.
Mkazi
wa Tegeta Kibaoni na mpenzi wa bia ya Tusker Bi. Leonarda Shayo
akiifurahia zawadi yake ya mfuko na fulana aliyokabidhiwa pale
promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi ndani ya baa
ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki
wa promosheni hiyo ambayo inadhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya
bia ya Serengeti. Akikabidhi zawadi hiyo (Kulia) ni Balozi wa bia ya
Tusker Veronica Mbilinyi na (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni
hiyo Gadner Habash.
Mpenzi
wa bia ya Tusker ambaye pia ni mkazi wa jiji la Mbeya Monalisa
Makangila(Katikati) akipokea zawadi ya fulana na mfuko toka kwa balozi
wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (Kulia) wakati wa promosheni ya
Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini
Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa
na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni
mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio Efm Gadner
Habash.
Mkazi wa
Tegeta, Uwanja wa Upanga ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Max
Richard akijiandaa kupokea zawadi ya fulana toka kwa Meneja Masoko wa
bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella (Kulia) wakati wa promosheni ya
Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika kiwanja cha baa ya Family iliyopo
Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya wiki kwenye
promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker yenye lengo la
kuzihamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli
kwenye utoaji huduma kwa wateja. Promosheni hiyo ya nchi nzima
inaendelea pia katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Moshi, Morogoro na Mbeya.
Mkazi wa
Segerea ambaye pia ni mjasiriamali Frank Ndumbalo (Kulia) akipokea
zawadi yake ya fulana toka kwa Afisa Masoko anayejifunza kwa vitendo
toka Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Josephat Shelukindo wakati wa
kusherekea ushindi wa baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam.
Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki kwenye promosheni ya Tusker
Fanyakweli Kiwanjani Kiwanjani inayodhaminiwa na bia ya Tusker toka
Kampuni ya bia ya Serengeti.