Wednesday, September 23, 2015


 Mkazi wa Wazo Hill, Tegeta Mary Joseph (Katikati) akipokea zawadi ya fulana toka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ubungo, Mbezi na Tegeta Bw. Victor Mhindi (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani iliyofanyika katika baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo na Mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni redio E-fm, Gadner Habash.



 Mkazi wa Tegeta Kibaoni na mpenzi wa bia ya Tusker Bi. Leonarda Shayo akiifurahia zawadi yake ya mfuko na fulana aliyokabidhiwa pale promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi ndani ya baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo ambayo inadhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. Akikabidhi zawadi hiyo (Kulia) ni Balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi na (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner Habash. 





 Mpenzi wa bia ya Tusker ambaye pia ni mkazi wa jiji la Mbeya Monalisa Makangila(Katikati) akipokea zawadi ya fulana na mfuko toka kwa balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio Efm Gadner Habash.
Mkazi wa Tegeta, Uwanja wa Upanga ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Max Richard akijiandaa kupokea zawadi ya fulana toka kwa Meneja Masoko wa bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika kiwanja cha baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker yenye lengo la kuzihamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye utoaji huduma kwa wateja. Promosheni hiyo ya nchi nzima inaendelea pia katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Moshi, Morogoro na Mbeya.
Mkazi wa Segerea ambaye pia ni mjasiriamali Frank Ndumbalo (Kulia) akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Afisa Masoko anayejifunza kwa vitendo toka Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Josephat Shelukindo wakati wa kusherekea ushindi wa baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Kiwanjani inayodhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog