Rais
wa klabu ya Simba,Evans Aveva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuwatambulisha katibu mkuu
mpya wa klabu ya Simba bwana Patrick Kahemele (mwisho kushoto) na kocha
mkuu mpya Joseph Omog (pichani kati) ambae ni raia wa Cameroon.Kocha
Omog aliwasili jana usiku hapa jijini..
Pichani
wa tatu kulia ni Katibu mkuu mpya wa Simba Patrick Kahemele akifafanua
jambi na kwamba kuanzia sasa ndiye atakaehusika na masuala ya klabu
hiyo,kwani kwa kipindi kirefu timu hiyo haikuwa na Mtendaji Mkuu ambaye
amekuwa akishugulikia masuala mbalimbali ya kiutendaji kwa ujumla.
Kocha
Mkuu mpya Joseph Omog,ambae ni raia wa Cameroon akifafanua jambo mbele
ya wana habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar.
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KLABU
ya Simba imemtambulisha kocha mpya leo na kuingia nae kandarasi ya
miaka miwili 2016/2018 huku wakimpa nafasi ya kuchagua benchi lake la
ufundi. Raisi wa Simba Evance Aveva amesema kuwa hatua hiyo imekuja
baada ya kupitia sifa za Joseph Omog na kuona atakuwa msaada mkubwa sana
katika kuisaidia timi ya Simba.
Akizungumza
wakati wa utambulisho wa kocha huyo, Aveva amesema huu ni mwanzo mzuri
kwa Simba wana imani ana nafasi kubwa ya kuwasaidia katika namna
watakavyobadilisha na kupata mafanikio kwa timu hiyo. " Ni mategemeo
yetu kuwa kandarasi hii tuliyoingia na Omog itakuwa na mafanikio na
malengo makubwa ya Simba ni kuitoa ilipo na kuirudisha kuwa ya zamani,
". Naye Omog amesema kuwa amekuja Simba kwa ajili ya kuisaidia na
kuijenga na atafanya kazi vizuri na kwa ufanisi mkubwa.
Wakati
huo huo Aveva alimtambulisha katibu mkuu mpya wa Simba Patrick Kahemele
ambaye kuanzia sasa atahusika na masuala ya klabu hiyo na zaidi kwa
kipindi kirefu hakukuwa na mtendaji mkuu ambaye anakuwa anashughulikia
suala la utendaji kiujumla.