Tuesday, December 2, 2014


MENEJA wa Manchester United Louis Van Gaal anaamini ni muhimu kabisa wimbi la ushindi kuendelea watakapocheza na Stoke City Uwanjani Old Trafford Jumanne Usiku katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Licha ya kukabiliwa na majeruhi kibao, Man United wapo Nafasi ya 4 kwenye Ligi baada ya kupata ushindi Mechi 3 mfululizo dhidi ya Crystal Palace, Arsenal na Hull City.
Akiongea kwenye mahojiano kuhusu Mechi na Stoke City, Van Gaal amesema: “Ushindi kwa Klabu kubwa kama Man United ni Muhimu, natumai tutashinda dhidi ya Stoke. Lakini kwenye Ligi Kuu si kila kitu rahisi. Ukiwaona Liverpool wakihangaika kwa Dakika 85 na kufunga Bao moja inaonyesha hilo. Umewaona Arsenal wakisumbuka na West Bromwich kwenye Mechi ambayo wangeweza kufungwa. Ligi Kuu inafurahisha sana, hujui nini litatokea!”

Hata hivyo, Van Gaal amekiri Old Trafford ni safi hasa baada ya Mashabiki wao kuamka na kuipa sapoti kubwa Timu yao.

Kwenye Mechi hii, kila Timu itakosa Masta wao kadhaa ambao ni majeruhi kwa Man United kuwakosa Angel Di Maria. Luke Shaw, Daley Blind na Phil Jones wakati Stoke watawakosa Steve Sidwell, Glenn Whelan, Victor Moses, Robert Huth na Peter Odemwingie.


RATIBA: LEO JUMANNE
Jumanne Desemba 2 

22:45 Burnley v Newcastle
22:45 Leicester v Liverpool
22:45 Man United v Stoke
22:45 Swansea v QPR
23:00 Crystal Palace v Aston Villa
23:00 West Brom v West Ham


KESHO JUMATANO.
Jumatano Desemba 3 
22:45 Arsenal v Southampton 
22:45 Chelsea v Tottenham 
22:45 Everton v Hull
22:45 Sunderland v Man City

waliotembelea blog